Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,
Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA. Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.
Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.
Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).
Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).
Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.
Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.
Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu - Bara,
Chama Cha Wananchi CUF,
Igunga - Tabora,
07/09/2011.