Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Mitandao ya kijamii nayo wainunue? -- sina uhakika kwa hilo ila kwa JF hata waje na 100billion tutasema ukweli daima fitna kwetu mwiko.

Hata humu JF wamo wanaonunuliwa. Tena wengi tu. Si unawaona akina Mwita25, FF, MS. Binafsi wala sishangai wala kuogopa. Wamulize Joji Maratu wa ITV baada ya kuripoti uongo kuhusu cdm kwenye mazishi ya Chacha Wangwe!?
 
Inawezekana kabisa ikawa kweli maana tayari wanahabari wapo Igunga kwa kishindo na wamekuwa wakiandika positively kwa CCM na -ly kw aupinzani. tusubiri tuone
 
Kwa mishahara midogo na uzumbukuku wa waandishi wetu,haya yanawezekana kabisa tena kwa laki mbili mbili tu!
 
Narudia tena, ningekuwa punguani ningewezaje kupata GPA ya 4.0?
Zipo mbinu nyingi zinaweza kutumika kupata GPA, hata punguani kama wewe anaweza kutumia mbinu mmojawapo.
 
Msimamizi amesema kama mpaka sa'12 hakuna form itakayokuwa imerudishwa basi hakuna pingamizi litakalokubaliwa! Me nadhani hivi vyama viwili vinategeana, mmoja akipeleka basi na kingine kinapeleka!
Ina maana watakuwa nje ya office ya msimamizi wakitazamana? Loh kazi ipo tena mbichi kabisa!
 
Wote wanaweka pingamizi kumpinga mgombea wa CAF hakupitishwa na kikao rasmi cha chama chake zaidi waliandika barua ya utambulisho na kusainiwa na mtu asiye na mamlaka kichama CAF niwakurupukaji sana ngoja tusubiri.
 
Hii habari ni kweli,ila isichukuliwe kijumla kuhusu magazeti tajwa. niko igunga. Jana nilikaa bar fulani peke yangu kwenye meza wakaja waandishi wawili kukaa,nilisikia wakiulizana kama wamo kwenye mgawo wa hela hizo.mmoja akasema yumo mwingine akasema kuna mtu wake wa karibu kambania.ila walikuwa wakijiuliza kama mpango huo utakubaliwa na mwananchi.yaani yote uliyotaja yameshakubali ila hawajui kama mwananchi watakubali.na walisema siyo rahisi kupenyeza upuuzi pale kwa maneno yao eti ni wazee wa kubalance.tusubiri tuone
 
Ningekuwa sina akili ningepata GPA ya 4.0?

Inaonekana ulikuwa darasa moja na akina Sofia Simba, Ngeleja, JK, Pinda, Makamba Jr, FF, MS, and the like. Na kwa upuuzi uliosomea, ukapata gpa ya 4.0! Na kama ungeacha kutumia masaburi kufikiri, basi ungepata ya 5.0! Idiot....!?
 
Ni kweli huo mpango upo na kwakuwa mimi wameniacha nimeamua kumwaga mboga na subirini ntawawekea pepa ya January iliyopelekwa CC na Nnape na mjue mpango wa kununua wahariri mpaka waandishi pamoja na watakaokuwa newsroom wametengewa fedha kitu kinaitwa get keeprs.
 
MKAKATI WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA KATIKA KAMPENI ZA

UCHAGUZI MDOGO WA
JIMBO LA IGUNGA

UTANGULIZI
Septemba 7, 2011 mpaka Oktoba Mosi, 2011 Chama Cha Mapinduzi kitashiriki katika kampeni za kumnadi mgombea wake wa Ubunge katika jimbo la IgungaKatika kuhakikisha CCM inashiriki vema katika uchaguzi huo tumepitia mambo kadhaa na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati utakaolenga kuwezesha kupatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mdogo.
MKAKATI WA MEDIA.
a) Vyombo vya habari tutakavyoambatana navyo katika kampeni hizo ni pamoja na ITV-1, TBC-1, Channel Ten, Radio Uhuru, na waandishi wa magazeti ya Mwananchi, Mtanzania, Majira, Jambo Leo, Nipashe, Habari Leo na Uhuru na Mzalendo. Lengo ni kuwa na waandishi watakaokuwa wakiwajibika moja kwa moja kwetu.
b) Linahitajika gari moja ambalo litakuwa ni maalum kwa ajili ya waandishi wa habari litakalokuwa na mafuta ya kutosha kwenda kwenye maeneo ya mikutano na kurejea katika vituo vya kutumia habari bila usumbufu wala kuchelewa. (Inapendekezwa Gari hilo litoke moja kati ya magari ya Wilaya zilizo karibu na Igunga)
c) Kuwa na vifaa vitakavyotumiwa na waandishi kutuma habari kwa vyombo vyao vya habari bila usumbufu, kama Modem za mitandao yote pamoja na Laptop 4 na gharama ya vifurushi vya mawasiliano. Hii itasaidia kusimamia kazi watakayokuwa wakiifanya kwa ukaribu zaidi.
d) Kuwa na ufuatiliaji wa habari katika vyombo vya habari moja kwa moja ili kujiridhisha na aina ya taarifa zinazoripotiwa. (Wahariri wahusishwe) ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuratibu uandishi wa makala na Maoni ya wahariri yatakayolenga masuala ya msingi badala ya yale yanayohusu na kuzungumzia watu.

e) Kuhakikisha kuwa habari zote nzuri zinazokijenga chama chetu ziwe zinawafikia wanaigunga mapema bila kuchelewa.

f) Kuhakikisha kuwa online kampeni inafanyika kwa muda wote. Vijana maalumu watumike kwa muda wote kusambaza video na picha za matukio yote kwenye blogs na mitandao ya kijamii.
MKAKATI WA KUWASHIRIKISHA NA KUWAUNGANISHA VIONGOZI WA CHAMA NA WAPIGA KURA (Get people engaged during campaign and Get to voting Strategy)
Chama chetu kina muundo mzuri na madhubuti unaoshuka mpaka ngazi ya shina. Kwa bahati mbaya muundo huo hatuutumii katika kiwango kinachostahili. Katika uchaguzi huu mdogo daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo zima lipatikane na kila mpiga kura wa jimbo hilo afikiwe na ahamasishwe ajitokeze kupiga kura. Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Igunga ni 171,077. Jimbo lina kata 26, matawi 114 na mashina 3707. Ili kuwa na uhakika wa ushindi na kuweza kumfikia kila mpiga kura haina budi kila ngazi ifanye kazi ya kuwafikia na kuwashawishi wapiga kura katika viwango vifuatavyo. Kila shina lazima liwafikie wapiga kura 46. Na kila Tawi linatakiwa kuwafika wapiga kura 1500, na kila Kata lazima ihakikishe kuwa ninawafikia wapiga kura 6579. Kiwango hicho siyo kikomo cha mwisho, kuna kata zipo maeneo ya mjini na zinawapiga kura wengi kuliko nyingine hivyo basi kata hizo lazima zihakikishe kuwa zianwafikia wapigakura wengi iwezekanavyo. Wajumbe wote wa mashina, kamati za utekelezaji za jumuiya zote, kamati za siasa za matawi yote na mabaraza ya Jumuiya wapewe kila mmoja majina ya wapiga kura pamoja na mitaa wanayoishi, wawafuatilie na kuwashirikisha katika shughuli za chama kwa muda wote wa kampeni.
Kazi ya kuwashirikisha wananchi haiwezi kukamilika bila kuhakikisha wanatoka kwenda kupiga kura. Hivyo basi wajumbe wa mashina pamoja na viongozi ambao walishiriki kuwa andaa wananchi katika kipindi cha kampeni wahakikishe kuwa wanawafuatilia nakuwakumbusha watoke waende kupiga kura na kuichagua CCM. Uzoefu wa uchaguzi uliopita umetuonesha kuwa katika hatua hii hatukufanya vizuri na hivyo kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha watu wachache wajitokeze kupiga kura.
HITIMISHOPamoja na kuhitajika kwa masuala mengi na ya muhimu kutekelezwa, haya ni muhimu zaidi katika kuwezesha hayo mengine kutekelezeka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa na msingi wa kitendaji ili masuala mengine yanayohitaji kutekelezwa kitaaluma, yafanywe hivyo. GHARAMA ZA KUFANIKISHA MIKAKATI HIYO
  1. Posho (waandishi wa habari) 40,000/= @17 X siku 25 17,000,000/=
  1. Nauli (Waandishi wa habari) 45,000/=@17 X 2 1,530,000/=
  1. Modem 40,000/=@4modem 160,000/=
  1. Mawasiliano 100,000/=@17 1,700,000/=
  1. Back office (Gate keepers) 200,000/=@ 17 3,400,000/=
  1. Online campaigning 10people@55,000/= X siku 25 13,750,000/=
JUMLA 37,540,000/=
NB: Kutokana na hali ngumu ya uchumi ya chama chetu, inashauriwa maafisa wote wa Idara na Chama ambao wanazo laptop zitumike kufanikisaha usambazaji wa taarifa za kampeni kwa muda wote. Jumla ya lap top tano zinatakiwa kwa ajili ya shughuli hiyo. NAWASILISHA.

Someni kipengele cha kuwaweka wahariri sawa ndipo mtajua nini kinaendelea huko na hapo ujue tayari watu wameshavuta mlungula na walioletwa hapa JF wanalipwa elfu 55 kwa siku hivyo mnapoteza muda kupambana na watu ambao tayari wameshapata malipo.

More to come stay tuned.
 
KWAKAWAIDA TAWALA ZINAZOANGUKA HUWA NA AINA HIYO YA VIASHIRIA,
Tawala zinazopenda kuandikwa vizuri hakika hazina miaka mingi yakuishi, tawala ambazo hazipendi kuambiwa ukweli , daima hupongezwa kwa kilemba cha ukoka, hudhani mambo yanakwenda vyema kumbe yanaharibika.
NI VYEMA KWA USTAWI WA TAIFA CCM WAKIENDELEA KUHONGA MAANA ITAHARAKISHA MAGEUZI NDANI YA TAIFA HILI.
 
kila la heri mgombea wa chadema, natoa wito kwa wana igunga kuungana na kuiangusha CCM, kuhusu Cuf kwani sitayari walishafunga ndoa na ccm kule zanzbar? sitarajii zuri lolote kutoka kwao
 
MKAKATI WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA KATIKA KAMPENI ZA

UCHAGUZI MDOGO WA

JIMBO LA IGUNGA

UTANGULIZI
Septemba 7, 2011 mpaka Oktoba Mosi, 2011 Chama Cha Mapinduzi kitashiriki katika kampeni za kumnadi mgombea wake wa Ubunge katika jimbo la IgungaKatika kuhakikisha CCM inashiriki vema katika uchaguzi huo tumepitia mambo kadhaa na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati utakaolenga kuwezesha kupatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mdogo.
MKAKATI WA MEDIA.
a) Vyombo vya habari tutakavyoambatana navyo katika kampeni hizo ni pamoja na ITV-1, TBC-1, Channel Ten, Radio Uhuru, na waandishi wa magazeti ya Mwananchi, Mtanzania, Majira, Jambo Leo, Nipashe, Habari Leo na Uhuru na Mzalendo. Lengo ni kuwa na waandishi watakaokuwa wakiwajibika moja kwa moja kwetu.
b) Linahitajika gari moja ambalo litakuwa ni maalum kwa ajili ya waandishi wa habari litakalokuwa na mafuta ya kutosha kwenda kwenye maeneo ya mikutano na kurejea katika vituo vya kutumia habari bila usumbufu wala kuchelewa. (Inapendekezwa Gari hilo litoke moja kati ya magari ya Wilaya zilizo karibu na Igunga)
c) Kuwa na vifaa vitakavyotumiwa na waandishi kutuma habari kwa vyombo vyao vya habari bila usumbufu, kama Modem za mitandao yote pamoja na Laptop 4 na gharama ya vifurushi vya mawasiliano. Hii itasaidia kusimamia kazi watakayokuwa wakiifanya kwa ukaribu zaidi.
d) Kuwa na ufuatiliaji wa habari katika vyombo vya habari moja kwa moja ili kujiridhisha na aina ya taarifa zinazoripotiwa. (Wahariri wahusishwe) ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuratibu uandishi wa makala na Maoni ya wahariri yatakayolenga masuala ya msingi badala ya yale yanayohusu na kuzungumzia watu.

e) Kuhakikisha kuwa habari zote nzuri zinazokijenga chama chetu ziwe zinawafikia wanaigunga mapema bila kuchelewa.

f) Kuhakikisha kuwa online kampeni inafanyika kwa muda wote. Vijana maalumu watumike kwa muda wote kusambaza video na picha za matukio yote kwenye blogs na mitandao ya kijamii.
MKAKATI WA KUWASHIRIKISHA NA KUWAUNGANISHA VIONGOZI WA CHAMA NA WAPIGA KURA (Get people engaged during campaign and Get to voting Strategy)
Chama chetu kina muundo mzuri na madhubuti unaoshuka mpaka ngazi ya shina. Kwa bahati mbaya muundo huo hatuutumii katika kiwango kinachostahili. Katika uchaguzi huu mdogo daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo zima lipatikane na kila mpiga kura wa jimbo hilo afikiwe na ahamasishwe ajitokeze kupiga kura. Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Igunga ni 171,077. Jimbo lina kata 26, matawi 114 na mashina 3707. Ili kuwa na uhakika wa ushindi na kuweza kumfikia kila mpiga kura haina budi kila ngazi ifanye kazi ya kuwafikia na kuwashawishi wapiga kura katika viwango vifuatavyo. Kila shina lazima liwafikie wapiga kura 46. Na kila Tawi linatakiwa kuwafika wapiga kura 1500, na kila Kata lazima ihakikishe kuwa ninawafikia wapiga kura 6579. Kiwango hicho siyo kikomo cha mwisho, kuna kata zipo maeneo ya mjini na zinawapiga kura wengi kuliko nyingine hivyo basi kata hizo lazima zihakikishe kuwa zianwafikia wapigakura wengi iwezekanavyo. Wajumbe wote wa mashina, kamati za utekelezaji za jumuiya zote, kamati za siasa za matawi yote na mabaraza ya Jumuiya wapewe kila mmoja majina ya wapiga kura pamoja na mitaa wanayoishi, wawafuatilie na kuwashirikisha katika shughuli za chama kwa muda wote wa kampeni.
Kazi ya kuwashirikisha wananchi haiwezi kukamilika bila kuhakikisha wanatoka kwenda kupiga kura. Hivyo basi wajumbe wa mashina pamoja na viongozi ambao walishiriki kuwa andaa wananchi katika kipindi cha kampeni wahakikishe kuwa wanawafuatilia nakuwakumbusha watoke waende kupiga kura na kuichagua CCM. Uzoefu wa uchaguzi uliopita umetuonesha kuwa katika hatua hii hatukufanya vizuri na hivyo kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha watu wachache wajitokeze kupiga kura.
HITIMISHOPamoja na kuhitajika kwa masuala mengi na ya muhimu kutekelezwa, haya ni muhimu zaidi katika kuwezesha hayo mengine kutekelezeka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa na msingi wa kitendaji ili masuala mengine yanayohitaji kutekelezwa kitaaluma, yafanywe hivyo.GHARAMA ZA KUFANIKISHA MIKAKATI HIYO

  1. Posho (waandishi wa habari) 40,000/= @17 X siku 25 17,000,000/=

  1. Nauli (Waandishi wa habari) 45,000/=@17 X 2 1,530,000/=

  1. Modem 40,000/=@4modem 160,000/=

  1. Mawasiliano 100,000/=@17 1,700,000/=

  1. Back office (Gate keepers) 200,000/=@ 17 3,400,000/=

  1. Online campaigning 10people@55,000/= X siku 25 13,750,000/=
JUMLA 37,540,000/=
NB: Kutokana na hali ngumu ya uchumi ya chama chetu, inashauriwa maafisa wote wa Idara na Chama ambao wanazo laptop zitumike kufanikisaha usambazaji wa taarifa za kampeni kwa muda wote. Jumla ya lap top tano zinatakiwa kwa ajili ya shughuli hiyo.NAWASILISHA.

hii ni kali sana kuliko kawaida hapa sasa ndio unaanza kutofautisha kati ya wapinzani na chama tawala wao wanawaza wafanye vipi ili waibe na wapinzani wao wafanye vipi ili waeleweke kwenye hiki kizazi kisichokuwa na uthubutu..
 
Agalieni jamaa asije akasinzia kwenye mkutano, maana huyo hanaga aibu!
 
Ningekuwa sina akili ningepata GPA ya 4.0?
Unachoniboa ni utumbo wako huo, wiki iliyo pita ulisema una TV ya inch 40, mbona una dream vitu vidogo sana katika maisha? mimi nilidhani utaniambia una hisa kiasi gani katika kampuni flani, nakufananisha sana na mlinzi wangu pale home, story zake hazitofautiani na za kwako juzi nimemsikia akisema yeye zamani alikuwa anakuwaga wa kwanza darasani na alikuwaga ana washindaga wenzake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom