Mwandishi Jacob Daffi wa mwanahalisi amedai kunasa waraka wa ccm unaelezea kwamba ccm imepanga kutumia sh milioni 35 kuhonga waandishi wa magazeti na television ili kupika habari nzuri kuhusu chama hicho.
Lengo ni kuhakikisha habari nzuri tu ndizo zinaandikwa kuhusu kampeni za Igunga.
Kwa mujibu wa waraka huo magazeti yatakayotumika kwa mkakati huo ni mwananchi,majira,nipashe,jambo leo,habari leo na mtanzania.
Television zitakazohusika ni itv,tbc one na chanel ten.Pia baadhi ya mitandao ya kijamii itahusishwa katika mpango huu mchafu.
Imedaiwa mpango huu wote umeandaliwa na idara ya nape nnauye.Habari kamili imeandikwa uk wa 6 wa mwanahalisi.