Mlengo wa Kati
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 2,730
- 492
UTANGULIZIMKAKATI WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA KATIKA KAMPENI ZA
UCHAGUZI MDOGO WA
JIMBO LA IGUNGA
Septemba 7, 2011 mpaka Oktoba Mosi, 2011 Chama Cha Mapinduzi kitashiriki katika kampeni za kumnadi mgombea wake wa Ubunge katika jimbo la IgungaKatika kuhakikisha CCM inashiriki vema katika uchaguzi huo tumepitia mambo kadhaa na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati utakaolenga kuwezesha kupatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mdogo.
MKAKATI WA MEDIA.
a) Vyombo vya habari tutakavyoambatana navyo katika kampeni hizo ni pamoja na ITV-1, TBC-1, Channel Ten, Radio Uhuru, na waandishi wa magazeti ya Mwananchi, Mtanzania, Majira, Jambo Leo, Nipashe, Habari Leo na Uhuru na Mzalendo. Lengo ni kuwa na waandishi watakaokuwa wakiwajibika moja kwa moja kwetu.
b) Linahitajika gari moja ambalo litakuwa ni maalum kwa ajili ya waandishi wa habari litakalokuwa na mafuta ya kutosha kwenda kwenye maeneo ya mikutano na kurejea katika vituo vya kutumia habari bila usumbufu wala kuchelewa. (Inapendekezwa Gari hilo litoke moja kati ya magari ya Wilaya zilizo karibu na Igunga)
c) Kuwa na vifaa vitakavyotumiwa na waandishi kutuma habari kwa vyombo vyao vya habari bila usumbufu, kama Modem za mitandao yote pamoja na Laptop 4 na gharama ya vifurushi vya mawasiliano. Hii itasaidia kusimamia kazi watakayokuwa wakiifanya kwa ukaribu zaidi.
d) Kuwa na ufuatiliaji wa habari katika vyombo vya habari moja kwa moja ili kujiridhisha na aina ya taarifa zinazoripotiwa. (Wahariri wahusishwe) ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuratibu uandishi wa makala na Maoni ya wahariri yatakayolenga masuala ya msingi badala ya yale yanayohusu na kuzungumzia watu.
e) Kuhakikisha kuwa habari zote nzuri zinazokijenga chama chetu ziwe zinawafikia wanaigunga mapema bila kuchelewa.
f) Kuhakikisha kuwa online kampeni inafanyika kwa muda wote. Vijana maalumu watumike kwa muda wote kusambaza video na picha za matukio yote kwenye blogs na mitandao ya kijamii.
MKAKATI WA KUWASHIRIKISHA NA KUWAUNGANISHA VIONGOZI WA CHAMA NA WAPIGA KURA (Get people engaged during campaign and Get to voting Strategy)
Chama chetu kina muundo mzuri na madhubuti unaoshuka mpaka ngazi ya shina. Kwa bahati mbaya muundo huo hatuutumii katika kiwango kinachostahili. Katika uchaguzi huu mdogo daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo zima lipatikane na kila mpiga kura wa jimbo hilo afikiwe na ahamasishwe ajitokeze kupiga kura. Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Igunga ni 171,077. Jimbo lina kata 26, matawi 114 na mashina 3707. Ili kuwa na uhakika wa ushindi na kuweza kumfikia kila mpiga kura haina budi kila ngazi ifanye kazi ya kuwafikia na kuwashawishi wapiga kura katika viwango vifuatavyo. Kila shina lazima liwafikie wapiga kura 46. Na kila Tawi linatakiwa kuwafika wapiga kura 1500, na kila Kata lazima ihakikishe kuwa ninawafikia wapiga kura 6579. Kiwango hicho siyo kikomo cha mwisho, kuna kata zipo maeneo ya mjini na zinawapiga kura wengi kuliko nyingine hivyo basi kata hizo lazima zihakikishe kuwa zianwafikia wapigakura wengi iwezekanavyo. Wajumbe wote wa mashina, kamati za utekelezaji za jumuiya zote, kamati za siasa za matawi yote na mabaraza ya Jumuiya wapewe kila mmoja majina ya wapiga kura pamoja na mitaa wanayoishi, wawafuatilie na kuwashirikisha katika shughuli za chama kwa muda wote wa kampeni.
Kazi ya kuwashirikisha wananchi haiwezi kukamilika bila kuhakikisha wanatoka kwenda kupiga kura. Hivyo basi wajumbe wa mashina pamoja na viongozi ambao walishiriki kuwa andaa wananchi katika kipindi cha kampeni wahakikishe kuwa wanawafuatilia nakuwakumbusha watoke waende kupiga kura na kuichagua CCM. Uzoefu wa uchaguzi uliopita umetuonesha kuwa katika hatua hii hatukufanya vizuri na hivyo kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha watu wachache wajitokeze kupiga kura.
HITIMISHOPamoja na kuhitajika kwa masuala mengi na ya muhimu kutekelezwa, haya ni muhimu zaidi katika kuwezesha hayo mengine kutekelezeka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa na msingi wa kitendaji ili masuala mengine yanayohitaji kutekelezwa kitaaluma, yafanywe hivyo.GHARAMA ZA KUFANIKISHA MIKAKATI HIYO
- Posho (waandishi wa habari) 40,000/= @17 X siku 25 17,000,000/=
- Nauli (Waandishi wa habari) 45,000/=@17 X 2 1,530,000/=
- Modem 40,000/=@4modem 160,000/=
- Mawasiliano 100,000/=@17 1,700,000/=
- Back office (Gate keepers) 200,000/=@ 17 3,400,000/=
JUMLA 37,540,000/=
- Online campaigning 10people@55,000/= X siku 25 13,750,000/=
NB: Kutokana na hali ngumu ya uchumi ya chama chetu, inashauriwa maafisa wote wa Idara na Chama ambao wanazo laptop zitumike kufanikisaha usambazaji wa taarifa za kampeni kwa muda wote. Jumla ya lap top tano zinatakiwa kwa ajili ya shughuli hiyo.NAWASILISH
Peleka Umbeya wako huko! mtu yoyete anaweza kuandika hii!