Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Zipigwe tu,tujue mbabe ni nani.mambo ya ushndi wa mezani sio mtamu.pingamizi zote zipigwe chni na match ianze mara moja.
 
Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,

Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA.

Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.

Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.

Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).

Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.

Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu - Bara,
Chama Cha Wananchi CUF,
Igunga - Tabora,
07/09/2011.

Kama CUF wangekuwa makini kule Shimoni Mombasa walienda kuchukua nini? wadanganye wajinga siyo humu jf. nakujua wewe msomi lakini inaonyesha unatumia akili za mkopo pole sana. endelea kujipotezea credibility yako in politics. you will soon treated accordingly believe me. Achana na hao CUF mkuu wangu watakupoteza. sasa hivi wanakutumia kwa ajili ya ukristo wako, but for sure, you will no longer exist in that position
 
hahaha..........natamani dk kafumu aenguliwe!!!!!!!
 
kwa mujibu wa tbc 1 pingamizi zote zimetupiliwa mbali na wagombea wote 8 wametangazwa kuwa ni wagombea halali


ana bahati huyo kafumu......ila hashindi...cdm wako juu na lazima wachukue jimbo
 
kwa mujibu wa tbc 1 pingamizi zote zimetupiliwa mbali na wagombea wote 8 wametangazwa kuwa ni wagombea halali

Hata kama kulikuwa na mapingamizi ya ukweli, sikutegemea kama mgombea wa ccm angeenguliwa.

Nadhani kazi imebaki moja tu, kufanya kampeni za uhakika lakini kubwa kuliko yote ni kulinda kura, hapo ndo magamba wanafanyia mambo.
 
Mgombea wa CDM Igunga nasikia alishawahi kufungwa jela miaka mitatu kwa wizi
ndugu ritz nashauri tafuta kaz za kufanya haiwezekani kila siku usiku na mchana uko tu kwenye hii forum au umeajiriwa na nape?
 
Mbona Masha alikuwa mwizi naye akapewa uwaziri?
 
Mpaka ilipofika saa 10. Leo jioni ni wagombea wa vyama viwili tu ndio walio wekewa pingamizi walizowekewa na chama cha wanainchi CUF, taarifa tulizozipata kutoka katika vyanzo vya huko Igunga. kuhusu ni pingamizi zinahusu nini nitaendelea kuwajuza
<br />
<br />
pingamizi zote zimetupiliwa mbali na msimamizi wa uchaguzi. CUF(CCM-B) wana akili kama ya mnyama fulani aliyesababisha mods kumfungia mpambanaji wetu Daudi Mchambuzi.
 
P&#305;ngam&#305;z&#305; z&#305;metupwa mbali
 
Mwandishi Jacob Daffi wa mwanahalisi amedai kunasa waraka wa ccm unaelezea kwamba ccm imepanga kutumia sh milioni 35 kuhonga waandishi wa magazeti na television ili kupika habari nzuri kuhusu chama hicho.

Lengo ni kuhakikisha habari nzuri tu ndizo zinaandikwa kuhusu kampeni za Igunga.
r
Kwa mujibu wa waraka huo magazeti yatakayotumika kwa mkakati huo ni mwananchi,majira,nipashe,jambo leo,habari leo na mtanzania.

Television zitakazohusika ni itv,tbc one na chanel ten.Pia baadhi ya mitandao ya kijamii itahusishwa katika mpango huu mchafu.

Imedaiwa mpango huu wote umeandaliwa na idara ya nape nnauye.Habari kamili imeandikwa uk wa 6 wa mwanahalisi.

Hee!!
Jamaa linawashutumu mafisadi kwa rushwa kubwa kubwa, huku nae akizitoa?
Nape acha hizo.
.
 
@Mijadala ya namna hii humu ndani JF haitakwisha, ukweli unaweza kuwa wazi lakini ukapindishwa kwa makusudi. Ombi langu wote mlioko Igunga, mnapotupa habari, jaribuni kutupa na video pictures kwenye Utube. Kisha sisi mwenyewe tutapima upi ukweli na upi uongo...kuepusha propaganda, kwani baadhi ya vyama vimejiandaa vya kutosha kufanya propaganda humu JF (Hasa chama cha mapinduzi). @Kuhusu CUF kuingilia msafara wa Chadema, according to Mwananchi newspaper la leo, mgombea wa CUF amekiri wafuasi wake kufanya hilo na kusema hizo zilikuwa ni mbwembwe tu za kawaida za uchaguzi!! Now Mtatiro is speaking something different. mmh Hapo kutakuwa kuna tatizo tu...
 
Ukitaka kumjua mtu tenga muda usome post zake za zamani.
 
Mgungamiba, bila shaka machungu unayo kuhusiana na dhuluma ya aina yoyote wezi wanavyopanga kufanya. Hata hivyo, nakushauri utayari wako juu ya kinachotokea Igunga katika jamvi hili uwepo pia kwa viongozi waandamizi chama yaani CDM. Kwamba, uwe na ushirikiano katika kujaribu kutegua mitego ya sisimu uliyoisema kwenye "post" yako kuhusiana na zoezi lililoanza leo kule Igunga (uchaguzi mdogo). Tusiishie kusoma tu ya Wikileaks pekee wakati hata sisi wananchi tunazo taarifa za kinyama ambapo, tukiziweka wazi hatimaye tutapunguza manyanyaso yaendeshwayo na mabepari/wakoloni wa leo. Angalizo: ukiishia kusema uliyoyasema hapa na usiwe tayari kuwasaidia wananchi wenzako wa Igunga kumpata mbunge wao mahiri, basi yote uliyoyasema yatabaki kuwa uzushi tu.
 
MKAKATI WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA KATIKA KAMPENI ZA

UCHAGUZI MDOGO WA

JIMBO LA IGUNGA





UTANGULIZI
Septemba 7, 2011 mpaka Oktoba Mosi, 2011 Chama Cha Mapinduzi kitashiriki katika kampeni za kumnadi mgombea wake wa Ubunge katika jimbo la IgungaKatika kuhakikisha CCM inashiriki vema katika uchaguzi huo tumepitia mambo kadhaa na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati utakaolenga kuwezesha kupatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mdogo.
MKAKATI WA MEDIA.
a) Vyombo vya habari tutakavyoambatana navyo katika kampeni hizo ni pamoja na ITV-1, TBC-1, Channel Ten, Radio Uhuru, na waandishi wa magazeti ya Mwananchi, Mtanzania, Majira, Jambo Leo, Nipashe, Habari Leo na Uhuru na Mzalendo. Lengo ni kuwa na waandishi watakaokuwa wakiwajibika moja kwa moja kwetu.
b) Linahitajika gari moja ambalo litakuwa ni maalum kwa ajili ya waandishi wa habari litakalokuwa na mafuta ya kutosha kwenda kwenye maeneo ya mikutano na kurejea katika vituo vya kutumia habari bila usumbufu wala kuchelewa. (Inapendekezwa Gari hilo litoke moja kati ya magari ya Wilaya zilizo karibu na Igunga)
c) Kuwa na vifaa vitakavyotumiwa na waandishi kutuma habari kwa vyombo vyao vya habari bila usumbufu, kama Modem za mitandao yote pamoja na Laptop 4 na gharama ya vifurushi vya mawasiliano. Hii itasaidia kusimamia kazi watakayokuwa wakiifanya kwa ukaribu zaidi.
d) Kuwa na ufuatiliaji wa habari katika vyombo vya habari moja kwa moja ili kujiridhisha na aina ya taarifa zinazoripotiwa. (Wahariri wahusishwe) ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuratibu uandishi wa makala na Maoni ya wahariri yatakayolenga masuala ya msingi badala ya yale yanayohusu na kuzungumzia watu.

e) Kuhakikisha kuwa habari zote nzuri zinazokijenga chama chetu ziwe zinawafikia wanaigunga mapema bila kuchelewa.

f) Kuhakikisha kuwa online kampeni inafanyika kwa muda wote. Vijana maalumu watumike kwa muda wote kusambaza video na picha za matukio yote kwenye blogs na mitandao ya kijamii.
MKAKATI WA KUWASHIRIKISHA NA KUWAUNGANISHA VIONGOZI WA CHAMA NA WAPIGA KURA (Get people engaged during campaign and Get to voting Strategy)
Chama chetu kina muundo mzuri na madhubuti unaoshuka mpaka ngazi ya shina. Kwa bahati mbaya muundo huo hatuutumii katika kiwango kinachostahili. Katika uchaguzi huu mdogo daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo zima lipatikane na kila mpiga kura wa jimbo hilo afikiwe na ahamasishwe ajitokeze kupiga kura. Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Igunga ni 171,077. Jimbo lina kata 26, matawi 114 na mashina 3707. Ili kuwa na uhakika wa ushindi na kuweza kumfikia kila mpiga kura haina budi kila ngazi ifanye kazi ya kuwafikia na kuwashawishi wapiga kura katika viwango vifuatavyo. Kila shina lazima liwafikie wapiga kura 46. Na kila Tawi linatakiwa kuwafika wapiga kura 1500, na kila Kata lazima ihakikishe kuwa ninawafikia wapiga kura 6579. Kiwango hicho siyo kikomo cha mwisho, kuna kata zipo maeneo ya mjini na zinawapiga kura wengi kuliko nyingine hivyo basi kata hizo lazima zihakikishe kuwa zianwafikia wapigakura wengi iwezekanavyo. Wajumbe wote wa mashina, kamati za utekelezaji za jumuiya zote, kamati za siasa za matawi yote na mabaraza ya Jumuiya wapewe kila mmoja majina ya wapiga kura pamoja na mitaa wanayoishi, wawafuatilie na kuwashirikisha katika shughuli za chama kwa muda wote wa kampeni.
Kazi ya kuwashirikisha wananchi haiwezi kukamilika bila kuhakikisha wanatoka kwenda kupiga kura. Hivyo basi wajumbe wa mashina pamoja na viongozi ambao walishiriki kuwa andaa wananchi katika kipindi cha kampeni wahakikishe kuwa wanawafuatilia nakuwakumbusha watoke waende kupiga kura na kuichagua CCM. Uzoefu wa uchaguzi uliopita umetuonesha kuwa katika hatua hii hatukufanya vizuri na hivyo kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha watu wachache wajitokeze kupiga kura.
HITIMISHOPamoja na kuhitajika kwa masuala mengi na ya muhimu kutekelezwa, haya ni muhimu zaidi katika kuwezesha hayo mengine kutekelezeka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa na msingi wa kitendaji ili masuala mengine yanayohitaji kutekelezwa kitaaluma, yafanywe hivyo.GHARAMA ZA KUFANIKISHA MIKAKATI HIYO

  1. Posho (waandishi wa habari) 40,000/= @17 X siku 25 17,000,000/=

  1. Nauli (Waandishi wa habari) 45,000/=@17 X 2 1,530,000/=

  1. Modem 40,000/=@4modem 160,000/=

  1. Mawasiliano 100,000/=@17 1,700,000/=

  1. Back office (Gate keepers) 200,000/=@ 17 3,400,000/=

  1. Online campaigning 10people@55,000/= X siku 25 13,750,000/=
JUMLA 37,540,000/=
NB: Kutokana na hali ngumu ya uchumi ya chama chetu, inashauriwa maafisa wote wa Idara na Chama ambao wanazo laptop zitumike kufanikisaha usambazaji wa taarifa za kampeni kwa muda wote. Jumla ya lap top tano zinatakiwa kwa ajili ya shughuli hiyo.NAWASILISHA.







Hapo kwenye red watakuwa:
1. Mwita25
2. Ritz
3. Ngongo
4. Mzee wa Mawe
5. Faiza Fox
6. Mlengo wa kati
7. Ibwe
8. John Marwa
9. Malaria Sugu
10. Mgungamwiba
 
Ningekuwa sina akili ningepata GPA ya 4.0?

Nasikia hiyo ni ya kuungaunga kama nini....mara leo kwa prof x kesho kwa Mr Y unadhani hatujui? Sasa ulikuwa unaenda kufanya nini wewe mnafiki? Maana kila siku ulikuwa unafanya kazi ya kuonga walimu wakutoe...lile somo ulilokamatwa na prof.....unadhani hatujui ulichomoaje?
 
Wakuu,,Mwita na wengineo wa mlengo wake wanachofanya ktk kila thread ni kutupia vitu kuwatoa great thinkers kudadavua na kuchangia thread mama badala yake wanaanza kumshambulia yeye jambo ambalo anafanikiwa sana. Nadhani wanajamvi tuwe tuna m ignore na kuendelea kujikita katika mada/thread husika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom