Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
MKAKATI WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA KATIKA KAMPENI ZA

UCHAGUZI MDOGO WA

JIMBO LA IGUNGA

UTANGULIZI
Septemba 7, 2011 mpaka Oktoba Mosi, 2011 Chama Cha Mapinduzi kitashiriki katika kampeni za kumnadi mgombea wake wa Ubunge katika jimbo la IgungaKatika kuhakikisha CCM inashiriki vema katika uchaguzi huo tumepitia mambo kadhaa na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati utakaolenga kuwezesha kupatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mdogo.
MKAKATI WA MEDIA.
a) Vyombo vya habari tutakavyoambatana navyo katika kampeni hizo ni pamoja na ITV-1, TBC-1, Channel Ten, Radio Uhuru, na waandishi wa magazeti ya Mwananchi, Mtanzania, Majira, Jambo Leo, Nipashe, Habari Leo na Uhuru na Mzalendo. Lengo ni kuwa na waandishi watakaokuwa wakiwajibika moja kwa moja kwetu.
b) Linahitajika gari moja ambalo litakuwa ni maalum kwa ajili ya waandishi wa habari litakalokuwa na mafuta ya kutosha kwenda kwenye maeneo ya mikutano na kurejea katika vituo vya kutumia habari bila usumbufu wala kuchelewa. (Inapendekezwa Gari hilo litoke moja kati ya magari ya Wilaya zilizo karibu na Igunga)
c) Kuwa na vifaa vitakavyotumiwa na waandishi kutuma habari kwa vyombo vyao vya habari bila usumbufu, kama Modem za mitandao yote pamoja na Laptop 4 na gharama ya vifurushi vya mawasiliano. Hii itasaidia kusimamia kazi watakayokuwa wakiifanya kwa ukaribu zaidi.
d) Kuwa na ufuatiliaji wa habari katika vyombo vya habari moja kwa moja ili kujiridhisha na aina ya taarifa zinazoripotiwa. (Wahariri wahusishwe) ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuratibu uandishi wa makala na Maoni ya wahariri yatakayolenga masuala ya msingi badala ya yale yanayohusu na kuzungumzia watu.

e) Kuhakikisha kuwa habari zote nzuri zinazokijenga chama chetu ziwe zinawafikia wanaigunga mapema bila kuchelewa.

f) Kuhakikisha kuwa online kampeni inafanyika kwa muda wote. Vijana maalumu watumike kwa muda wote kusambaza video na picha za matukio yote kwenye blogs na mitandao ya kijamii.
MKAKATI WA KUWASHIRIKISHA NA KUWAUNGANISHA VIONGOZI WA CHAMA NA WAPIGA KURA (Get people engaged during campaign and Get to voting Strategy)
Chama chetu kina muundo mzuri na madhubuti unaoshuka mpaka ngazi ya shina. Kwa bahati mbaya muundo huo hatuutumii katika kiwango kinachostahili. Katika uchaguzi huu mdogo daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo zima lipatikane na kila mpiga kura wa jimbo hilo afikiwe na ahamasishwe ajitokeze kupiga kura. Jumla ya waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Igunga ni 171,077. Jimbo lina kata 26, matawi 114 na mashina 3707. Ili kuwa na uhakika wa ushindi na kuweza kumfikia kila mpiga kura haina budi kila ngazi ifanye kazi ya kuwafikia na kuwashawishi wapiga kura katika viwango vifuatavyo. Kila shina lazima liwafikie wapiga kura 46. Na kila Tawi linatakiwa kuwafika wapiga kura 1500, na kila Kata lazima ihakikishe kuwa ninawafikia wapiga kura 6579. Kiwango hicho siyo kikomo cha mwisho, kuna kata zipo maeneo ya mjini na zinawapiga kura wengi kuliko nyingine hivyo basi kata hizo lazima zihakikishe kuwa zianwafikia wapigakura wengi iwezekanavyo. Wajumbe wote wa mashina, kamati za utekelezaji za jumuiya zote, kamati za siasa za matawi yote na mabaraza ya Jumuiya wapewe kila mmoja majina ya wapiga kura pamoja na mitaa wanayoishi, wawafuatilie na kuwashirikisha katika shughuli za chama kwa muda wote wa kampeni.
Kazi ya kuwashirikisha wananchi haiwezi kukamilika bila kuhakikisha wanatoka kwenda kupiga kura. Hivyo basi wajumbe wa mashina pamoja na viongozi ambao walishiriki kuwa andaa wananchi katika kipindi cha kampeni wahakikishe kuwa wanawafuatilia nakuwakumbusha watoke waende kupiga kura na kuichagua CCM. Uzoefu wa uchaguzi uliopita umetuonesha kuwa katika hatua hii hatukufanya vizuri na hivyo kuwa moja kati ya sababu zilizosababisha watu wachache wajitokeze kupiga kura.
HITIMISHOPamoja na kuhitajika kwa masuala mengi na ya muhimu kutekelezwa, haya ni muhimu zaidi katika kuwezesha hayo mengine kutekelezeka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa na msingi wa kitendaji ili masuala mengine yanayohitaji kutekelezwa kitaaluma, yafanywe hivyo.GHARAMA ZA KUFANIKISHA MIKAKATI HIYO
1. Posho (waandishi wa habari) 40,000/= @17 X siku 25 17,000,000/=
1. Nauli (Waandishi wa habari) 45,000/=@17 X 2 1,530,000/=
1. Modem 40,000/=@4modem 160,000/=
1. Mawasiliano 100,000/=@17 1,700,000/=
1. Back office (Gate keepers) 200,000/=@ 17 3,400,000/=
1. Online campaigning 10people@55,000/= X siku 25 13,750,000/=
JUMLA 37,540,000/=
NB: Kutokana na hali ngumu ya uchumi ya chama chetu, inashauriwa maafisa wote wa Idara na Chama ambao wanazo laptop zitumike kufanikisaha usambazaji wa taarifa za kampeni kwa muda wote. Jumla ya lap top tano zinatakiwa kwa ajili ya shughuli hiyo.NAWASILISH

Peleka Umbeya wako huko! mtu yoyete anaweza kuandika hii!

Nina hamu ya kuona hillo pingamizi jamani weeee acha tuu, na wasipopeleka pingamizi ina maana wote walikuwa wanajihami kama kuku mwoga

yani kuna watu hapa jf wanapenda kupotosha ukweli sana..tuwekeni wazi wakuu ni chama gani kimewekewa pingamizi???

Tunawaasa waandishi wa habari wafuate misingi ya taaluma ya uandishi wa habari, bila ku biase upande wowote. Kitendo cha mwandishi wa habari kuandika habari za uwongo kwa kumchafua fulani na kumpendelea fulani mwisho wa siku kunampunguzia au kumwondolea credibility mbele ya jamii.
Tangu lini makanjanja wakawa watu makini, hebu tuangalie pale TBC nani anaweza kutoa habari za ukweli ikiwa wote ni watu wa CCM kila mara nikuripoti habri mbofumbofu tu za upinzani huku kila baya la CCM WAKILITIA KAPUNI, Magazeti kama habari leo si ndio walitabiri kuwa DR JK atakuwa rahisi mmh. Tuwe waungwana waandishi tulionao hawana moyo wa kizalendo wako kimaslahi zaidi

Tatizo la chama cha Magamba ni kuona kuwa matatizo ya Wadanganyika ni ya muda tu wakati wa kampeni yaani wanafanya Wadanganyika ni watu wasiokuwa na uelewa mambo. Vyombo vilivyotajwa hapo ni vya makada wao wasiojali utu wa Watanganyika wanaozania kuwa watabaki milele wamesimama

Pingamizi limewekwa na vyama 3 kama ifuatavyo;

AFP -dhidi ya CCM kuwa Kafumu hana ruhusa ya mwajiri wake na hivyo ametoroka kazini anapaswa kuenguliwa na wakaweka precidence ya pingamizi la Prof.Mwandosya dhidi ya mgombea wa NCCR kule rungwe.CCM wameandikiwa juu ya pingamizi hilo na hawajajibu mpaka sasa .

AFP-dhidi ya mgombea wa CUF kuwa mgombea wa CUF hakuteuliwa na vyombo vya kikatiba vya chama kwani hakukuwahi kufanyika kikao chochote cha baraza kuu kwa ajili ya kumteua kama katiba yao inavyosema hivyo sio mgombea halali -kaandikiwa ajibu na mpaka sasa hajajibu.

CCM -dhidi ya CDM wao wamesema kuwa mgombea wa CDM sio mwanachama wa Chadema ila ni mtumishi wa serikali na hana kadi ya Chadema - Hili limetupiwa mbali kwani msimizi alipowataarifu CDM walipeleka kadi ya mgombea wao na barua ya likizo ambayo aliruhusiwa kugombea .Hivyo hakuna pingamizi dhidi ya mgombea wa CDM mpaka sasa .

More. info later ndio tuko kikaoni tunaendelea na mipango ya kuchukua jimbo.

kumekucha mpaka njuruku kwa waandishi na kuweka sawa wahahriri ...ngoja tuone nini kitafuata

Asante kwa taarifa mkuu!

Nyongeza ,ni kuwa AFP wamesema kuwa mgombea wa CCM kadanganya eneo la kuzaliwa kwani ameandika ni Igunga wakati amezaliwa Sengerema na kuhamia Igunga , wanasubiriwa kujibu ili tujue nini kitaendelea.

safi sana magamba mtakoma...CUF nao hawana jipya unafiki tu umewajaa..CHADEMA JIMBO LETU HILO

Naomba CCM wasienguliwe watapata cha kusema ngoma ipigwe dk 90 ila wa Kafu nilishawahi kusema toka siku ile arudishwe na msimamizi akalete barua ya chama na kwenda kuandikia baa bila kikao rasmi hana sifa.

baraza kuu la cuf linauzo wa kumpitisha mgombea kwa mujibu wa katiba ya CUF ndilo lenye maamuzi ya mwisho ya kuteua mgombea na walifanya hivyo. hakuna pingamizi msimamizi tupa kwenye dust bin.

Pingamizi limewekwa na vyama 3 kama ifuatavyo;

AFP -dhidi ya CCM kuwa Kafumu hana ruhusa ya mwajiri wake na hivyo ametoroka kazini anapaswa kuenguliwa na wakaweka precidence ya pingamizi la Prof.Mwandosya dhidi ya mgombea wa NCCR kule rungwe.CCM wameandikiwa juu ya pingamizi hilo na hawajajibu mpaka sasa .

AFP-dhidi ya mgombea wa CUF kuwa mgombea wa CUF hakuteuliwa na vyombo vya kikatiba vya chama kwani hakukuwahi kufanyika kikao chochote cha baraza kuu kwa ajili ya kumteua kama katiba yao inavyosema hivyo sio mgombea halali -kaandikiwa ajibu na mpaka sasa hajajibu.

CCM -dhidi ya CDM wao wamesema kuwa mgombea wa CDM sio mwanachama wa Chadema ila ni mtumishi wa serikali na hana kadi ya Chadema - Hili limetupiwa mbali kwani msimizi alipowataarifu CDM walipeleka kadi ya mgombea wao na barua ya likizo ambayo aliruhusiwa kugombea .Hivyo hakuna pingamizi dhidi ya mgombea wa CDM mpaka sasa .

More. info later ndio tuko kikaoni tunaendelea na mipango ya kuchukua jimbo.

any more updates Mkuu, it's now 19.04 jioni

Aksante kwa taarifa tunaomba muendelee kutujuza kama kuna lolote jipya

Mgombea wa CDM Igunga nasikia alishawahi kufungwa jela miaka mitatu kwa wizi

mpaka tunafika saa 10 jioni ni vyama viwili ndio vilivyowekewa pingamizi vyama hivyo ni CCM na Chadema ambazo pingamizi hizo wamewekewa na na chama cha wanainchi CUF, Tunaendelea kutafiti ni pingamizi zinahusiana na ni nini nitaendelea kuwajuza hapa jamvini.

mkuu kweli unaimudu kazi yako ya propaganda...lakini sio poa kutumia ID mbili tofauti kupost same taarifa inayofanana kila kitu!MZEE WA MAWE=CUF ngangari!

Mgombea wa CDM Igunga nasikia alishawahi kufungwa jela miaka mitatu kwa wizi

kumbe ni sera ya CCM kuajiri wezi? mbona alipokuwa afisa wa serikali hukusema . Keshawapiga bao...kuhusu pingamizi someni kwenye ile thread nyingine hapa hakuna kitu ni kukurupuka bila kujua nini kinaendelea kwenye karata tunasema hujui mzungu kalalia wapi na umelamba jokeri

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom