Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
KUMBE NI WEWE HOUSEBOY WA NEPI NAUYE![/COLOR] HAYA UWANJA WAKO SASA!
Kwake yeye hiyo ni heshima na si kebehi. Yuko tayari kumfanyia Nape na chama chake llolote hata kama litadhalilisha utu wake. Kuna wimbo unaimba " ...duniani kuna watu na viatu....."
 
Source: Mtanzania 9/9/11.

Kweli kama viongozi wetu ndio hawa, nchi hii sasa inaenda kubaya kabisa.

Wana JF: Nilidhani angeenda na kauli za kuwapoza wana Igunga kwa kipigo kikali cha maisha magumu na mlo mmoja, mfumuko wa bei na kilimo duni, yeye anasema kafurahi sana kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Dar hadi Igunga bila kuona vumbi.

Kimsingi, namuunga mkono na furaha yake kwa kuwa labda kwao lami ndio maendeleo. Ona haya ya Igunga;

  1. Kilimo cha pamba hoi.
  2. Huduma za afya mtihani
  3. Shule ni kusadikikaa
  4. Access to clean drinking water ni ndoto ya mwendawazimu
  5. Huduma za kibenki mashahidi nyie.
  6. Stendi safi ya mabasi imebaki kwenye ilani
  7. Vikundi vya kinamama na vijana vya maendeleo hoi
  8. Miundombinu kichekesho, shahidi yeye mwenyewe na Mwigulu,
  9. ....
Sasa kwa yeye kusema anaona raha lami imepita Igunga, basi hiyo lami ndio itatatua matatizo hayo na mengine mengi? Lami itashusha bei ya sukari? Lami itashusha bei ya mkate? Vipi hiyo lami itagawa dawa kutibu magonjwa? Lami itawapa wana Igunga maji safi ya kunywa?

Mi nadhani Mkapa angeenda kuwaomba wanaigunga msamaha kwa kusahaulika na zaidi sana kuwaangukia ili wamchague mgombea wao badala ya kusema lami safi sana.

Wazee wa kazi, Nawasilisha.
 
Jamani hata mimi najarabu kuangalia, naona CCM wapo sawa katika hili, wamejaribu kuangalia mtu mwenye mvuto kwasasa hayupo CCM, ndiyo maana wamemuomba huyu mzee, japo alikuwa akitajwa kwa wizi lakini alijitahidi kupiga kazi, kuliko watu wengine wanaiba na hawafanyi kazi. Kweli CCM maji yamewafika shingoni, (Kuna tetesi kwamba Rostam kakataa kuwasaidia katika hilo, wamecheki na magufuli amewashauri kwamba kiprotakali hatakiwi kwenda kufungua Kampeni kwasababu siyo mwenyekiti wala katibu mkuu wa chama, walitaka kumpeleka Kikwete lakini inahisiwa kwamba anaweza kupigwa mawe kama Mbeya kwasababu ya kile kinachosemekana fitina zake dhidi ya Rostam baadaye ikamuangukia Mkapa) nina uhakika Igunga hamtoki labda Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifuate maelekezo kama iliyopewa October 2010
 
Riz1 na uzaifu wake wote lakini hawezi kuwa Bogus kama huyu mtoa mada, by the way Riz1 atafute nini kwenye mitandao wakati mihela kedekede wanahongwa hadi suti.

mkuu .... njaa inawafanya watu wajidhalilishe ....! ignorance at its best
 
Kuna darasa la watu wazima pale Tandale Uzuri takulipia ukasome, unaona sasa unavyoandika unajiacha uchi. teh teh teh



eti kilaza anakosoa .... upuuzi mtupu
 
Cha ajabu ni nini???? watu wanakorofishana ndani ya ndoa itakuwa kwenye chama?????
 
eti kilaza anakosoa .... upuuzi mtupu
LATIFA,
Kila siku nakuambia jifunze matumizi ya herufu kubwa na ndogo, angalia sasa kumbe na wewe Kilaza, Teh teh teh teh
 
Kufika kwake jana ilikuwa kujaribu kudivert attention ya wana Igunga kwa mawazo finyu ya CCM,walijua akifika mida ambayo Chadema ndio wanaanza shughuli za ufunguzi wa Kampeni watu wangekuwa wengi kwake nadhani jibu kalipata mapema na kila atakoloporomosha litapata majibu mara mia moja atasikitika maisha yake yote
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 08 September 2011 21:35 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kupitia chama hicho, Joseph Kashindye (kushoto) kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika katika Viwanja vya Sokoine mjini Igunga, mkoani Tabora jana. Picha na Mpiga picha Maalum

Boniface Meena, Igunga
KAMPENI za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, mkoani Tabora zimeanza rasmi huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiwarushia makombora wagombea wa CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Wakati Chadema kilizindua kampeni hizo jana, CCM kinatarajiwa kuzindua kampeni zake huku Mkapa akitarajiwa kuongoza mashambulizi katika uzinduzi huo. Mkapa aliwasili Igunga jana kwa tambo za kuwasambaratisha wapinzani.

Tuhuma za Mkapa
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chadema, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibord Slaa alimtuhumu Mkapa kwamba alifanya biashara akiwa Ikulu kutokana na kuanzisha kampuni ya AnBen ambayo alidai kuwa imewaibia Watanzania chini ya mwamvuli wa Ikulu.

"Akija hapa mdaini pango kwa kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu wakati ile ni mali ya wananchi,” alisema Dk Slaa.
Alifafanua kwamba, Mkapa akiwaeleza kuwa serikali imeleta maendeleo wana Igunga wamuulize kuhusu fedha ambazo zilitoka Ikulu kwa ajili ya biashara zake binafsi.

Hata hivyo, madai hayo dhidi ya rais mstaafu Mkapa si mapya kwani tayari Dk Slaa alikwishayaibua na kuyatangaza katika maeneo mbalimbali nchini.

Amgeukia Kafumu
Kuhusu Dk Kafumu, Dk Slaa alisema mgombea huyo wa CCM alipaswa ajiuzulu kutokana na kashfa za rushwa zilizoikumba wizara ya Nishati na Madini ambako alikuwa akifanya kazi.

Kabla ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Igunga kupitia CCM, Dk Kafumu alikuwa Kamishana wa Madini.

“Kafumu akiongezwa kule kwenye halmashauri ni sawasawa na kuongeza panya kwa kuwa walioko huko ni mapanya na wanaotafuna fedha za wananchi,” alidai Dk Slaa.

Dk Slaa aliwataka wananchi waliokuwa wamefurika katika Uwanja wa Sokoine kumchagua mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili aweze kulinda rasilimali za wana-Igunga katika halmashauri.

Alisema Dk Kafumu hawezi kuleta mabadiliko yoyote jimboni Igunga na taifa kwa ujumla, kutokana na mfumo mbovu wa CCM usioweza kusimamia maslahi ya wananchi.

Dk Slaa alisema nchi inahitaji kutetewa na makamanda ili iweze kufanikiwa kwa kuwa CCM imeshindwa kazi ya kuwasaidia wananchi.

Aliwaambia polisi wanaoagizwa kuwapiga mabomu wananchi wasifanye hivyo, kwa kuwa kazi ya Chadema ni kuwatetea polisi wadogo ambao wanapewa posho ndogo isiyokidhi mahitaji yao.

Mbowe na suti za JK
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Serikali ya CCM imeshindwa kazi hivyo haifai kuwa madarakani wala kuongezewa wabunge kwa kuwa itazidi kuwadidimiza wananchi.

Alisema haiwezekani rais wa awamu ya nne apelekwe London kupimwa na kununuliwa suti halafu aweze kuwasimamia wananchi wenye matatizo mengi.

“Eti Msemaji wa Ikulu anakanusha ukweli..., hii ni aibu kwa taifa,” alidai Mbowe na kuongeza:

“Nchi inauzwa watu wanapewa suti hii ni mbaya, amekuwa akienda Marekani na akirudi anasema amekwenda huko kuwaona wakubwa watusaide neti..., wametuletea vyandarua hivyo tuvitumie kwa umakini…,” alibeza Mbowe.

Alisema hii ni aibu kubwa kwa nchi ya Tanzania kuomba mgawo wa neti, wakati rasilimali zilizopo nchini zinaweza kutatua tatizo hilo la malaria.

Kashindye ajifananisha na Nyerere
Mgombea Chadema, Kashindye, aliwaambia wananchi wa Igunga kuwa, wakiona mwalimu anaachia chaki na kwenda kwenye siasa, wajue hali ni mbaya na taifa linahitaji ukombozi.

“Hata mwalimu Nyerere aliachia chaki alipoona hali ni mbaya, akaamua kuingia kwenye siasa ili kuikomboa Tanzania tunayoishi leo,” alisema.

Alisema kuwa, CCM wanadhani watumishi wa Serikali ni mali yao kitu ambacho si kweli na kwamba, ameamua kuingia Chadema ili kuwatetea wananchi wa Igunga na taifa kwa ujumla.

“CCM ni chama kinachokufa, nisingeweza kuondoka na kuingia CCM kuwa mbunge wa kusinzia…,” alisema.

Alisema mfumo mbaya wa utawala wa CCM umesababisha fedha nyingi za ujenzi wa barabara wilayani humo kuliwa. Aliongeza kuwa hali hiyo imesababisha wananchi kuendelea kupata mateso.

“Nawaombeni mnitume niende huko bungeni nikawe spika ya Igunga ili nikaseme yote na tupate mafanikio,” alisema.

Mnyika, Heche wanguruma
Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutokumchagua Dk Kafumu kwa kuwa ameliingiza taifa katika hasara kubwa kutokana na mikataba mibovu ya madini aliyoingia akiwa Kamishna wa Madini.

Mnyika alidai kuwa, haiwezekani mtu kama Dk Kafumu ambaye amekuwa dalali wa madini ya nchi awe mbunge wa Igunga, kwani atauza mali na almasi ya wana-Igunga.

“Sheria mbovu za madini Kafumu ndiye aliyeziruhusu na ufisadi mkubwa umefanyika katika sekta ya madini chini ya usimamizi wake, alifanya udalali wa kuliibia taifa na amelitia hasara ya Sh2,000 bilioni kwa kuingia katika mikataba mibovu ya madini,” alidai Mnyika na kuongeza:

“Mkapa akija mwambieni hatudanganyiki kwa kuwa wakati wa Serikali yake, ufisadi mkubwa ulifanyika akiwa pamoja na Dk Kafumu.”.
alisema Mnyika.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche, alimshambulia Dk Kafumu kuhusiana na mikataba mibovu ya madini ambayo imeliingiza taifa katika migogoro mikubwa na umasikini.

Alisema kuwa, Dk Kafumu hafai kuchaguliwa kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa wakifanya ufisadi ambao umewaweka wananchi katika maisha magumu wakati wao wakifurahia maisha mazuri ya kuwanyonya watanzania.

Heche aliwataka polisi kutojiingiza kwenye shughuli za kisiasa kwa kuwa watasababisha vurugu. Naye Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Susan Kiwanga, alisema ni lazima Igunga wahakikishe chama hicho kinashinda kwa kumchagua Kashindye ili aweze kuwatetea bungeni.

Mkapa atua, aanza tambo
Wakati akirushiwa makombora hayo, Mkapa jana alitua Igunga na kueleza kwamba, amefika kupigana na kumnadi mgombea wa CCM.

Rais huyo wa Awamu ya Tatu, alisema amejisikia faraja kusafiri katika barabara ya lami kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza ambayo ni matunda ya CCM.Akiwahutubia wananchi katika Kitongoji cha Makomero alisema ni muhimu wana Igunga wakavipuuza vyama vingine kwa kuwa CCM ikitoa ahadi inatimiza.

"Nimewasili Igunga, wana-Igunga kazi ni moja, ni ushindi tu,” alisema Mkapa wakati akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea katika kijiji cha Makomero, kilichoko kilometa nane kutoka mjini Igunga.

"Nashukuru sana kuona kwamba, mara hii nimefika hapa Igunga kwa kupita barabara ya lami, mara ya mwisho nilipita ikiwa vumbi tu. Jamani, haya si maendeleo? alisema Mkapa huku akishangiliwa na wananchi.

Mkapa aliwataka wananchi wa Igunga kujitokeza kwa wingi Oktoba 2, mwaka huu kupiga kura na kuhakikisha wanampigia mgombea wa CCM Dk Dalaly Kafumu na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wamechagua maendeleo."La msingi ni hilo mengine nitawaambia tutakapokutana katika mikutano ya kampeni," alisema Mkapa.

Mkapa alipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM, waliongozwa na Mratibu wa Kampeni za CCM jimboni humo, ambaye ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, Katibu wa Oganaizesheni wa NEC, Asha Abdallah Juma na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassani Wakasuvi.

Baada ya kusalimia wananchi msafara wa Mkapa ulielekea Igunga mjini ukiwa na magari kadhaa, yaliyozungukwa na vijana waendesha pikipiki na baiskeli.Uchaguzi mdogo wa Igunga unatarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Rostam Aziz aliyeliongoza jimbo hilo kwa miaka 18.

Hata hivyo, jana hakuna kiongozi wa Chadema aliyemgusa tofauti na miaka ya nyuma walipomtuhumu kwa ufisadi.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Viongozi wa CDM Igunga jana baada ya mkutano waliombwa na baadhi ya magazeti kuzungumzia suala hilo, hakuna aleyekuwa tayari kuongea kuhusu suala hilo.
Kwa kuhofia kuchukuliwa hatua na viongozi wa juu wa CDM, hususani wawili waliotajwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake, Dr Slaa.
Hawa viongozi hawana huruma, wanaiongoza CDM kama kampuni binafsi na sio taasisi ya kisiasa na sehemu kubwa ya uongozi wao ni ubabe mfano mmeona Madiwani wa Arusha walichofanyiwa? Wamesema wale CDM Igunga kwa masikitiko makubwa
 
Kweli kauli mbiu imetulia, CDM wajipange kulinda kura zisichakachuliwe. Kamanda Mnyika, Mdee na Wenje watawaonyesha wana Igunga namna ya kulinda kura kwani maeneo kama Ubungo, Mwanza na Kawe bila nguvu ya vijana kulinda kwa nguvu hawa wote wasingekuwa bungeni.
 
Atapigwa ngwara ya mwaka
Wala msimwonee aibu. Fisadi namba wani. Nakumbuka wakati anahitimisha kampeni za fisadi mwenzake Kikwete aliwaita wapinzani makokoro.
Sitasahau au kumsamehe kwa hilo. Mpeni vidonge vyake, shenzi type!
 
Kwani lile Tingatinga la zamani ni Bovu?
 
Kwa kawaida miundombinu, afya, elimu, nishati na ulinzi ni mambo ya lazima katika nchi yoyote na wala si ilani ya chama cha siasa. Haya ni majukumu ya lazima ya serikali yoyote ile inapokuwa madarakani sababu ndiyo yanayoendesha taifa. Sasa Mkapa anapodai kuwa barabara ya lami imetokana na CCM, kama bado akili zake zinafanya kazi alidhani serikali ipi ilitakiwa kujenga hiyo barabara?
CCM walivyo wajinga tusishangae hilo ndilo likawa jambo la kupigia kampeni.
 
huko ndiko kumpigia kampeni kafumu? kweli huyu mukapa hajui kupiga kampeni ndiyo maana alikuwa akiuzwa kama ndizi na Mwalimu Nyerere mwaka 1995.
 
nyota ndogo umenifurahisha sana aliuzwa kama ndizi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…