Nafikiri haya yanaweza kweli kuwa matokea ya Igunga kwasababu zifuatazo;
Kati ya majimbo magumu kwa Chadema basi hili ni mojawapo, kwanini:
1. Chadema, Mbowe, Slaa na wengine wameshindwa kufunguka na kumuattack Rostam moja kwa moja wakijua wazi kuwa huyu jamaa alikuwa anakubalika sana huko, kumuattack kungepoteza mvuto.
2. CDM wameshindwa kuongelea ufisadi kwa upana wa Nchi ambao ndio sera kuu, hii inatokana na hofu hiyohiyo kwani RA ameokena ndo kubwa la majambazi kwahiyo wamejikita kuiattach halmashauri ya Igunga na kukiri kuwa serikali imepeleka pesa nyingi Igunga lakini hakuna kilichofanyika, another weakness.
3. Vita ya ndani ya CCM imepotezewa, wamechukua watu neutral ili kuwapumbaza wana Igunga, wote waliokuwa wanampiga madongo RA wamewekwa kando.
4. Wananchi wa Igunga kubali usikubali watapiga kura in favour of RA,
5. RA yuko mtegoni, akiwapiga chini magamba wenzake wanaweza kumgeuzia kibao kwenye dili zake, akiwafagilia CDM watamuumbua baadae kwahiyo anatakiwa kusuka au kunyoa lkn kwa politics za TZ ni bora aende sawa na magamba yasije kumdhuru baadae kwasababu bado wameshikilia dola.
6. CDM wangeungana na vyama vingine labda wangekuwa kwenye sehemu nzuri ya kuichallenge CCM lkn kwa hali ya sasa ni ngumu.
7. Najua CDM kinawezaz kuwa chama makini na kuyatambua haya hivyo uwezekano wa kubadilisha matokeo ukawepo kama tu karata zao watazichanga vizuri.
Ingekuwa jimbo jingine huu ungekuwa ushindi wa wazi kwa CDM lkn kwakuwa huyu mstaafu alikuwa kisiki, jimboni ndani ya CCM na hata serikalini japo hakuwa kiongozi tusubiri tuone matokeo.