MgungaMiba, kwanza karibu jf kirasmi zaidi kama unavyosema, pili umemwaga nondo za ukweli from ground zero, hivyo tunakuomba uendelee kutupasha kinachoendelea kwa kadri uwezavyo na kwa kadri siku zinavyosogea, ndivyo wana jf wa Igunga watazidi kuongezeka na uchaguzi ukikaribia, jf itatuma wawakilishi wake kuwa miongoni mwa waangalizi.
Taarifa hii uliyoileta sio ya kubezwa hata kidogo maana ni pre-emptive move itakayotumika kama caveat kuzuia hayo yaliyopangwa yasitekelezwe.
Wakati ukiendelea kutupatia ya huko, jitahidi sana kuwa objective kwa kutoegemea upande mmoja, ili kutupa picha halisi ya hali ilivyo ground zero, ukiegemea upande mmoja, taarifa zako zinaweza kuleta false hopes za great expectations, hivyo matokeo yakitokea the other way round, watu watakuwa wameshajihamanisha na ushindi, wakishindwa waishie kulia kuwa eti 'tumeibiwa'.
Kwa jinsi ulivyoanza na headline hii "Mgombea wa CDM Igunga kuenguliwa!", imekaa kishabiki kidogo, as if ni hakika mgombea huyo kuenguliwa, ila ukishasoma ndipo utagundua hii ni speculation tuu na sii hakika, headiline yako ilipaswa kuwa na alama ya kuuliza na sio alama ya mshangao ambapo kwa jinsi ulivyoiweka ni kuashiaria msisitizo. Innapaswa kuwa hivi "Jee, Mgombea wa CDM Igunga kuenguliwa?" Toa picha halisi ya huko bila kujali nani humu jf watakusifu au kukukashifu, simama kwenye ukweli, na ukweli utakusimamisha imara.
Pasco.