Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
we acha uongo,sie hapa ndo tuko igunga,ukweli ni kwamba CUF walipangia kuanza maandamano yao ya kurudisha form saa saba na CDM saa nane mchana.

ILa cha kushangaza CUF kwanza hawakupeleka form yao katika muda uliopangwa na pia walienda kupaki gari lao la matangazo karibu na office ya CDM kama hiyo haitoshi wakasubiri mpaka walivyoona msafara wa CDM umeanza safari saa nane nao wakachua gari lao na kuingilia msafara wa CDM na kulipaka katikati ya balabala.

Ikabidi member wa CDM waanze kulipisha ilo gari, kama hiyo haitoshi tena kwa mara ya pili CUF wakakatisha tena katikati ya msafara wa CDM karibu na stand ya haisi bila sababu yeyote! Huo ndio ukweli msiwandanye wanaJF.

Hapa ndo tunaanzia rasmi kuwafunga midomo vichwa vya ng'ombe na wachumba wao kafu. Tupe habari kamili mkuu.

Acha unafiki kaka upo igunga ya wap? Msafara nimeuona mm mwenyewe magari hata 10 hayakufika. Usiwadanganye watz

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimesema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, na mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wassira ameitwa kwenda Igunga ili kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo.

Hayo yalielezwa jana wilayani Bunda na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka wilayani hapa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda.

Alisema Wassira atakwenda Igunga kuongeza nguvu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, utakaofanyika hivi karibuni.

Chama hicho tawala katika uchaguzi huo kimemsimamisha Dk Dalaly Kafumu, ambaye atapambana na wagombea wa vyama vya upinzani.

"Wassira atakwenda Igunga na tutahakikisha jimbo hilo linarejea CCM, kwani tayari chama chetu kimejipanga vizuri na ni chama chenye sera zinazotekelezeka," alisema.

Aidha, mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Mara, alisema kuwa chama hicho mkoani hapa, kimejipanga vizuri ili kuhakikisha katika uchaguzi mdogo utakaofanyika katika kata tatu za Jimbo la Rorya, ambazo madiwani wake walijiuzulu na kata moja ya wilayani Serengeti na moja ya wilayani Tarime kinapata ushindi wa kishindo.

Aliongeza kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Jimbo la Musoma mjini ambalo liko Chadema litarudi CCM.

Akichangia katika kikao hicho mjumbe mmoja Athumani Mambo, alisema kuwa CCM kumchagua Wassira kuwa mmoja wa wapiga kampeni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ni jambo la msingi sana kwani Wassira anao uwezo mkubwa wa kushawishi wananchi.

Aliongeza kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita, Wassira alisababisha majimbo mengi ya mkoani Mara, kuchukuliwa na chama hicho, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Tarime ambalo lilikuwa chini ya Chadema.

Kwa upande wake Wassira ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, alisema kuwa Jimbo la Igunga litakuwa la CCM, kwa sababu wamejipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kuhakikisha ushindi unapatikana.

swali langu je, kweli ccm wamekosekana watu wakuokoa jimbo la Igunga au maji yamezidi unga?

Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,

Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA.

Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.

Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.

Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).

Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.

Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu - Bara,
Chama Cha Wananchi CUF,
Igunga - Tabora,
07/09/2011.

Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,

Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA. Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.

Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.

Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.

Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).

Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.

Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.

Julius Mtatiro,

Naibu Katibu Mkuu - Bara,

Chama Cha Wananchi CUF,

Igunga - Tabora,

07/09/2011.

Julius nitasema ukweli daima hata kama utasema nakuandama,vitendo vyenu vya kuiandama chadema vitawaondoa katika historia ya kisiasa hapa bara.

Vyombo vote vya habari hasa magazeti asubuhi hii vimeandika jinsi Cuf walivyojipanga jana kuifanyia fujo chadema.Nikuulize swali dogo kwanini katibu wa CUF wilaya ya igunga bw. Maganga alipeleka vijana wa cuf ukumbi wa silver C kukutana na nape wa ccm?

Mna agenda gani? Laiti chadema wangekuwa ni watu wa fujo ule umati mkubwa wa wafuasi jana wangewafanya nini cuf?

Julius fahamu kwamba mbinu zote za siri mnazofanya kati ya cuf na ccm dhidi ya chadema zinajulikana vema.

Hizi bangi bana, sera ya CDM ni kufanya fujo, nitatizo la kuwa na vijana wavuta bangi.

Wamejipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kuhakikisha ushindi unapatikana kwa njia za wizi wa kura, aka uchakachuaji.

_DSC0924.JPG

Ivi hii picha ina maana gani?

Umesema anakwenda kuokoaa au kuuzamisha kabisa pindi atakapoanza kusinzia jukwaani??

Kwanza aende haraka sana akawaeleze walazwahoi wa Igunga kwamba amewanyanyulia mibomba mingapi ya maji safi alipokua waziri pale kabla hajahamia wizara ya BORA UTAWALA nchini.

Naona kila chama kimepeleka nondo zake Igunga, ni suala la muda tu kitaeleweka

we acha uongo,sie hapa ndo tuko igunga,ukweli ni kwamba CUF walipangia kuanza maandamano yao ya kurudisha form saa saba na CDM saa nane mchana,ila cha kushangaza CUF kwanza hawakupeleka form yao katika muda uliopangwa na pia walienda kupaki gari lao la matangazo karibu na office ya CDM kama hiyo haitoshi wakasubiri mpaka walivyoona msafara wa CDM umeanza safari saa nane nao wakachua gari lao na kuingilia msafara wa CDM na kulipaka katikati ya balabala,ikabidi member wa CDM waanze kulipisha ilo gari,kama hiyo haitoshi tena kwa mara ya pili CUF wakakatisha tena katikati ya msafara wa CDM karibu na stand ya haisi bila sababu yeyote! Huo ndio ukweli msiwandanye wanaJF.
ok tunashukru kwa taarifa mkuu endelea kutujuza

Mtatiro, mimi naamini katika ukweli, umetoa maelezo yanayoonyesha mna jeshi, umenishawishi niamini cuf ni washari! wewe mtatiro umeenda igunga kitambo kidogo, umeratibu vipi ratiba ya chama chako hadi kujikuta kina matukio mawili ndani eneo la sq km 3, kurudisha form ilipaswa kuwa ndiyo tukio kuu, iweje viongozi wa kitaifa wafike igunga lakini wasishiriki tukio muhimu la kurejesha form ili kuongeza hamasa kwa lengo la kuvutia yet undecided voters. naanza kuunganisha dots maneno yako kwenye kinyanganyiro cha ubungo ulivyogaragazwa na Mnyika hayana tofauti na mnavyojichanganya sasa. tafadhali Mtatiro fafanua njia mliyopita, iweje mkienda mmekutana mara mbili kwenye safari ya uelekeo mmoja. jenga hoja tuuone uadilifu wa cuf kwenye maandishi pia ufanane viwanjani. eleza mkakati mlioupanga kwenye kikao chenu cuf na Nape (ccm).

Nimesema mara kadhaa humu. CUF na CHADEMA mtawapa ushindi CCM wa "kishindo" endapo mtaendelea kutafunana hivi.

CCM watakuwa wanapongezana sana tu kwa kuangalia mnavyosigana hapo Igunga. Ushauri wangu kwenu CUF:

Kwa kuwa Maalim Seif ameonekana akianza ziara ya kiserikali mkoani Tabora kabla hajafika hapo Igunga, kuna haja gani ya ninyi kuweka mgombea?

Kama wassira ndio wa kuokoa Jahazi la CCM igunga baasi Magamba hakuna kitu tena!!

wasira si anaumwa ugonjwa wa kusinzia amepona,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom