Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Siyo kuokoa jahazi ila anawajibika, kama kada wa CCM, kufanya lolote linalowezekana kuhakikisha magwanda hawapati madaraka.
 
Wasira si anaumwa na mafua? Wanamtesa Mzee wa watu. Wamwache asinzie nyumbani kwake salama.
 
<br />
<br />
wewe ndo umekurupuka. Unaendeshwa na tumbo kufikiri.

Kana huyo anatumia Masaburi, yawezekana hata hajasikia WAPO-MATUKIO walichosema. Ni kweli hawa CCM B wamefanya fujo, waliweka gari tenge eti ili cdm wasipite, hii mijitu ya CUF huwa ni mishali sana, na mingi haina busara kama ndugu yao Seif alivyowasaliti na akabakia kuchonga tu Timberland ikulu 'Mwingulu'
 
wasira si anaumwa ugonjwa wa kusinzia amepona,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!

Mkuu kwenye chama hakuna kusinzia utamuona active lakini naona wamechelewa !
 
Anapeleka utaalamu wa kuiba na kuhonga wapiga kura kwani yeye mwenyewe jimboni kwakwe alichakachua matokeo hali ilikuwa mbaya. Inambidi awe makini asije dondosha pua.
 
Kweli la kuvunda halina ubani... wanampeleka LA KUSINZI uwanjani???

Aiseeeee
 
Wasira alipojitoa CCM alisema hatorudi tena CCM labda atarudishwa akiwa maiti,sasa yuko tena CCM na ndiye muokoa jahazi swali langu Wasira amerudiswha CCM maiti?So maiti inawezaje kuokoa jahazi?
 
Siyo kuokoa jahazi ila anawajibika, kama kada wa CCM, kufanya lolote linalowezekana kuhakikisha magwanda hawapati madaraka.
Hapo kwenye red naamini hata kusinzia stejini pia ni lolote. Ila hizi sio enzi za TANU msidhani mnaweza kufanya lolote mkafanikiwa.
 
Mtatiro hebu kuwa mkweli. Picha za kwenye vyombo vya habari leo zimeonesha ukorofi wenu, gari yenu imeblock msafara wa CHADEMA kwa mbele, bado unatuaminisha kuwa eti 'iliingiliana' na 'kwa bahati mbaya'? Kweli mnayoyafanya ndio yanayothibitisha kuwa ninyi ni vipandikizi wa ccm na inawezekana mko kutimiliza mishen ya kukwamisha upinzani nchini.

Kuhusu kuwa kwenu wachache, si hoja ya msingi kujibu, kinachotusikitisha ni jinsi mnavyotumia nguvu dhidi ya CHADEMA. Usitupotezee imani tuliyokuwanayo vijana kwako, kwamba wewe ni kijana mwenye uchungu wa kweli wa nchi hii. Kataa kutumika bwana.
 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimesema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, na mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wassira ameitwa kwenda Igunga ili kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo.

Hayo yalielezwa jana wilayani Bunda na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka wilayani hapa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda.

Alisema Wassira atakwenda Igunga kuongeza nguvu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, utakaofanyika hivi karibuni.

Chama hicho tawala katika uchaguzi huo kimemsimamisha Dk Dalaly Kafumu, ambaye atapambana na wagombea wa vyama vya upinzani.

"Wassira atakwenda Igunga na tutahakikisha jimbo hilo linarejea CCM, kwani tayari chama chetu kimejipanga vizuri na ni chama chenye sera zinazotekelezeka," alisema.

Aidha, mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Mara, alisema kuwa chama hicho mkoani hapa, kimejipanga vizuri ili kuhakikisha katika uchaguzi mdogo utakaofanyika katika kata tatu za Jimbo la Rorya, ambazo madiwani wake walijiuzulu na kata moja ya wilayani Serengeti na moja ya wilayani Tarime kinapata ushindi wa kishindo.

Aliongeza kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Jimbo la Musoma mjini ambalo liko Chadema litarudi CCM.

Akichangia katika kikao hicho mjumbe mmoja Athumani Mambo, alisema kuwa CCM kumchagua Wassira kuwa mmoja wa wapiga kampeni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, ni jambo la msingi sana kwani Wassira anao uwezo mkubwa wa kushawishi wananchi.

Aliongeza kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita, Wassira alisababisha majimbo mengi ya mkoani Mara, kuchukuliwa na chama hicho, ikiwa ni pamoja na Jimbo la Tarime ambalo lilikuwa chini ya Chadema.

Kwa upande wake Wassira ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, alisema kuwa Jimbo la Igunga litakuwa la CCM, kwa sababu wamejipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kuhakikisha ushindi unapatikana.

swali langu je, kweli ccm wamekosekana watu wakuokoa jimbo la Igunga au maji yamezidi unga?

Yani CCM tegemeo lao ni Wassira....lol!! Kweli chama kinaelekea pabaya,ila tunashukuru maana wanatuongezea mtaji CDM...naomba na hawa waende jamani...
  1. Yusuf Makamba
  2. Chiligati
  3. Mkuchika
  4. Hawa Ghasia
  5. Celine Kombani
  6. Ngeleja
  7. Tambwe Hizza
  8. ......................
 
Siyo kuokoa jahazi ila anawajibika, kama kada wa CCM, kufanya lolote linalowezekana kuhakikisha magwanda hawapati madaraka.
Angalia hiyo ilikuwa post yako ya ngapi ili ujue mawazo yako yanahusianaje na hiyo namba ya post 666
 
<br />
<br />
Ukibeba mayai akatokea mkorofi akaonye dalili za kufanyia fujo, inabidi uwe mpole uyalinde mayai. ile form ndiyo mbunge mtarajiwa, cuf inawezekana walikuwa wanaiwinda. wameliwa!!!

Great thinker!
Yaani umefikiria kitu ambacho mi najishawishi kuwa ni sahihi kabisa.
 
Kusema kuwa vijana wa CDM walikuwa na bisibisi,visu na viwembe ni uongo wa mchana, chama chenye kawaida ya kutembea na silaha ni CUF, hata IGP mstaafu Ustaadh Omari Mahita aliwahi kuonyesha visu na majambia ya CUF wakati wa uchaguzi, hivyo wewe Mtatiro usituoongopee, hizo ni mbinu zenu na wenzenu CCM, au umeingia CUF bila kujua kuwa hao ni wauaji, kumbuka hata kule Pemba walichinja askari polisi kama kuku, hao ndiyo CUF.
 
Hiyo iconic photo imenifurahisha na kunisikitisha pia,
Ukweli ni kuwa CUF haina historia na haijawahi kukifanyie vurugu chama kingine cha upinzani, CUF ni chama makini na tutaendelea kuwa hivyo, jana Igunga tumekuwa na misafara miwili, wafuasi wetu wengi walijigawa katika msafara wa Maalim Seif na kuhudhuria kikao cha ndani na at the same time wafuasi wetu wengine wengi walijigawa kumsindikiza mgombea wetu LEOPOLD MAHONA. Katika mazingira hayo automatically CHADEMA wangekuwa wengi katika urudishaji fomu kwani hiyo tu ndio ilikuwa shughuli yao jana huku sie CUF tukiwa na shughuli mbili tofauti kwa wakati mmoja na zote zilihitaji wafuasi na viongozi.

Msafara wa mgombea wetu ulienda kwa amani na hapakuwa na matatizo yoyote, masuala ya kuingiliana hayakuwa mantiki kubwa kwani kupeleka fomu hakukuwa na ratiba rasmi na kila chama kilijipangia, CUF tulipofika barabara kuu tukakutana na CHADEMA na tulipishana kwa busara kwani tumekutana barabarani kila mtu akitokea ofisini kwake and then tulipoenda mbele zaidi tulikutana na CHADEMA kwa mara ya pili na kila upande ulitumia busara ndio maana hatukupigana.

Wakati tunarudi ofisini baada ya kurudisha fomu, baadhi ya vijana wa CHADEMA walikuwa wamejipanga na wakaanza kuingilia msafara wetu wakiwa na BISIBISI, VIWEMBE na VISU(Polisi wana ushahidi wa matukioa haya), Baada ya vijana wetu wa ulinzi BG's kuwagundua wafuasi wale wa CHADEMA na kugundua wana silaha walianza kuwakamata ndani ya msafara wetu na kuwakagua, tukakamata viwembe vitatu, bisibisi 3 na kisu kimoja(Polisi walishuhudia matukio haya).

Katika ukaguzi huo katikati ya msafara baadhi ya vijana hao walikutwa na kadi na bendera za chadema ambavyo tunavyo hadi hivi sasa.
Baada ya ukaguzi huo na baada ya Chadema kufika ofisini kwao wakati wanawaaga wafuasi wao waliruhusu mmoja wa wale vijana walionyang'anywa bisibisi ambaye ambaye alilalamika ati amepigwa na wale walioitwa "mabaunsa wa CUF", kwa ushahidi wa wazi kijana yule alisema bila woga kuwa ,mabaunsa wa CUF wamempiga na kumnyang'anya BISIBISI yake(ameyasema haya kupitia vipaza sauti vya CHADEMA katika mkutano wao wa kuagana na wanachama wao jana jioni).

Baada ya matukio hayo tulilalamika rasmi kwa Kamanda Oparesheni Maalum(SIRO) na Kamanda wa FFU(Anacletus) ambapo baada ya kuwapa taarifa walituita viongozi wa CUF na CHADEMA kujadili chanzo cha vurugu hizo na kila upande ulitoa malalamiko yake.

Nataka kusisitiza kuwa sie CUF tumekwenda Igunga kumnadi mgombea wetu na kulisaka jimbo kwa njia za kidemokrasia, kamwe hatutamia silaha wala mabavu wala vitisho kuiska amani na demokrasia.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu - Bara,
Chama Cha Wananchi CUF,
Igunga - Tabora,
07/09/2011.

Mtatiro hizi siasa zako za maji ya chooni zinakimaliza chama chako na wewe ushapoteza mvuto wa kisiasa kitambo sana.
 
Mtatiro naona unaongoza chama ambocho hukijui au naweza sema huna historia ya chama chako sasa umechokoza na umeipata historia kamili ya cuf sasa endelea na uongo wako kama hujaumbuka hapa
 
Asante kwa taarifa mliopo igunga tunawategemea nyinyi mtupe taarifa kamili na zaukweli bila upendeleo.chadema kuweni macho kwani hao cuf wametumwa kuvuruga chadema kwa sababu kama kushinda hawana jeuri hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom