Ndugu wana jamvi, huku Igunga hali ni tete kwa CDM, wamebaki kiutafuta watu vijiweni ili wajaze mkutano wao wa ufunguzi. Mgombea wao hana mvuto kwa wapiga kura, DR. Kafumu ushindani mdogo utatoka kwa mgombea wa CUF, lakini CDM mambo ni mazito, SERA zenu za kutamka POSHO hamtaki huku USIKU mkizichukua hazina tija kwa wapiga kura wa Igunga. Dr. Kafumu ni tunu kwa Igunga na kiashirio cha maendeleo ya IGUNGA.
Nipo hapa Igunga madukani muda huu, CDM kwisha kazi pamoja na matangazo ya magari juu ya ufunguzi wao leo, mwitikio ni mdogo sana! Poleni wana CDM Igunga na Arusha sehemu mbili tofauti, Huku Igunga hakuna vijana wa kuleta fujo ambao huwa wanajaza maandamano yenu na mikutano.