Wajameni: Alisikika Mkapa akisema 'Na nyie Takukuru tunaomba mtuache tugawe mahindi kwa kuwa ccm ni chama sikivu, na hii sio rushwa mmesikia'? Hii ilitokea kwenye ufunguzi wa malumbano yao Igunga, na utafiti tumefanya na kugundua mahindi yanagawiwa mchana kweupe. Hayo ndio maendeleo anayosema Ben yanampa faraja kabisa. Lami toka Dar hadi Mwanza, chakula kaputii... Nchi hii bwana.
Sasa hapo napenda kusema Takukuru walijibu 'Sawa mkuu, na sasa mtagawa viroba vingapi?. Yaani hii ni sawa na Mkweree alipoambiwa na Marekani, 'Hey hebu ruka juu' Yeye alijibu 'Sawa mkuu, sasa niruke hadi wapi - nipimie wewe'.
Wisdom: Tulipitisha sheria ya uchaguzi ambayo sina hakika kama huyu Ben aliipitia kwa ukamilifu. Tunamuomba Tendwa atoe tamko vinginevyo ccm inagawa rushwa njenje. Yaani hii inakera sana. Wana JF, nawasilisha.