Heshima yenu wakubwa,
Asubuhi hii nimesoma habari ya Nape Nnauye kupigwa biti na katibu mkuu wake Wilson Mkama ktk gazeti la Mwanahalisi kwa sababu ya kwenda Igunga kuhani msiba wa Kijana aliyegongwa gari ktk msafara wa CCM na kufa papo hapo huko Igunga.
Taarifa zinasema kitendo chake hicho kimeuwaudhi sana Rais JK na W. Mkama kwa madai kwamba kitendo hicho kinaweza kumuudhi Rostam na kusababisha uchaguzi Igunga kuharibika.
Taarifa zinaendelea kusema kuwa, sokomoko hili lilitua mpaka kwa katibu mkuu Wilson Mkama aliyemwuliza Nnape, Nanukuu gazeti,
Nnape kwanini ulienda Igunga? Ulikatazwa na kamati kuu usiende, sasa, kwanini umeenda Igunga? \
Nnape alijibu, Nilikwenda kuhani msiba.
Mkama; Nani amekutuma? Mkama alifoka? Nape hakuwa na jibu.
Gazeti lilimtafuta Nnape kwa simu na kumuuliza kuhusu sokomoko hilo naye akajibu,
Alfred (mwandishi), mimi sina la kujibu kuhusu hilo. Akauliza, Jamani mimi ni kijana mwenzenu, nimewakosea nini?
Mkama alipopigiwa simu kuhusu habari hiyo, kwanza alicheka ha ha ha ha. Kisha akasema, fahamu sisi hatufanyi kazi za kiutendaji kupitia magazetini. Isitoshe, si vema kuzungumzia mambo mazito kama haya magazetini. Nakwenda Zanzibar, nitarudi kesho kutwa( Jumatano) njoo ofisini tuzungumze. Alipoambiwa kuwa gazeti liko mbioni kuchapishwa, alijibu sawa, lakini kwanini usije ofisini?
In my view, Mkama hakukanusha kumpiga biti Nnaye, ina maanisha alifanya hivyo( This is my opinion).
Gazeti pia lilikumbusha kuwa Nnape amewahi kujigamba ktk mtandao wa kijamii ( Jamii forums) kuwa mliosema sitaenda Igunga, mbona nimetinga
Igunga?
My take,
Nnape anajua alitendalo ndani ya CCM? Anaujua kweli msimamo wa JK?
Je, huku siko kushindwa kwa wazi kwa JK kwa hoja yake ya kuvuana magamba?