Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
ILEJE NA SONGWE TUMESHASHINDA KWA TECHNICALITIES, SASA TUNAENDA MOMBA........
Na Elius Ndabila
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, macho na masikio ya watanzania wote ni kuelekea OCTOBER 28 ni nani atashinda?
Lakini wakati Watanzania wanajiandaa kujua ni nani wataibuka kidedea kwenye uchaguzi huu mwezi Oktoba, katikati ya mwezi wa saba niliandika kuwa uchaguzi una mbinu nyingi za kushinda. Nilisema mbinu kubwa ni KURA NA TECHNICALITIES (Mbinu). Nilisistiza uchaguzi tuanza kushinda tangu siku ya kwanza unapochukua fomu. Niliandika hivyo nikijua wazi watu wengi wanakuwa busy na mbinu moja tu ya uchaguzi na kusahau Technicalities.
Kwa mkoa wa Songwe hususan Wilaya za Ileje na Songwe wamethibitisha kuwa Uchaguzi unaanzia kwenye Mbinu. Hadi sasa Wilaya za Ileje na Songwe Wagombea wake kwa ngazi za Ubunge wameshapita bila kupingwa baada ya wapinzani wao kushindwa kuruka viunzi/ Technicalities. Wagombea wa vyama vya upinzani walinaswa kwenye mtego hata kabla ya kuanza kampeni.
Wapo wanaolalamika kana kwamba wameonewa. Ninaomba kuwakumbusha tu kuwa kujaza fomu vizuri ni hitaji na takwa la kisheria. Unapokosea kujaza fomu unajiondolea uhalali wa kushiriki kwenye mchakato kwani unakuwa hujakidhi vigezo. Sheria haina huruma, uwe umefanya kosa kwa kujua au kuto kujua sheria inakuadhibu.
Wapo wanaosema kwa nini CCM wao hawakumbwi na haya matatizo. Ninaomba niwakumbushe kuwa linapokuja suala la uchaguzi CCM hakuna mzaha. Hili linakuwa ni suala la chama na si la mtu. Fomu za Wagombea wa CCM hujazwa kistadi kwa kushirikiana viongozi wa Wilaya, Mkoa na Wanasheria. CCM hawajazii fomu nyumbani, Madiwani linapokuja suala la kujaza fomu wote huitwa kwenye ofisi za CCM Wilaya kupata maelezo na kujaza fomu.
Halikadhalika linapokuja suala la Mbunge hujazia fomu ofisi za wilaya kwa kusimamiwa jopo la watumishi hushiriki ili kuondoa makosa yanayoweza kumuondolea sifa ya kukosa uhalali wa kugombea. Wakati CCM wakifanya haya, wenzetu upinzani sidhani kama wana hata eneo maalum la kukutana kujaza fomu, ninadhani Upinzani wengi kila mtu hujaza fomu kivyake ndiyo maana wanafanya Technicalities mistake.
Ileje na SONGWE kazi imeisha. Wagombea wanapita kujitambulisha na kutafuta kura za Rais na Madiwani. Wakati Songwe na Ileje haya yakifanyika sasa nguvu tunaelekeza Momba, Tunduma, Mbozi na Vwawa. Huku tunategemea kushinda kwa KURA baada ya TECHNICALITIES kugonga mwamba.