Mkuu hadi sasa Sanders hajafanya 'endorsement' kwa Hillary Clinton jambo linaloendelea kuzua mjadala wa nini hasa anasubiri na kwa niniJun 22 2016, 3:36 pm ET
Sanders: 'It Doesn't Appear That I'm Gonna Be the Nominee'
WASHINGTON, DC— Bernie Sanders acknowledged Wednesday that he will likely not be the Democratic nominee for president, as aides privately conceded that his future in the race remains in flux.
When asked in an interview with C-SPAN's Steve Scully if he would be speaking at the Democratic National Convention in Philadelphia this July, Sanders paused before answering.
"Well, you know it's hard to say, it doesn't appear that I'm gonna be the nominee, so I'm not gonna be determining the scope of the convention," admitted the Vermont senator, two weeks after former Secretary of State Hillary Clinton was projected to be the Democratic Party's presumptive nominee.
It's the closest Sanders has come to conceding the prolonged Democratic primary race to his opponent.
Kwa habari zaidi soma hapa;
Kwa mara ya kwanza kabisa Bernie Sanders ameonesha dalili ya kuinua mikono na kukiri hana nafasi yoyote ya kuweza kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Democrats katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu. Kinachosubiriwa sasa ni kuona kama atachukua hatua gani katika kuwashawishi mashabiki wake kumuunga mkono mgombea mteule Hillary Clinton.
Hadi sasa ni asilimia 55% tu ya wafuasi wa Sanders wako tayari kumuunga mkono Clinton huku asilimia 22% wakisema hawatamuunga mkono na badala yake watampigia kura Donald Trump na asilinia 18 wakisema watamuunga mkono mgombea wa Libertarian. Swali ni je Sanders ataweza kubadilisha msimamo wa wapenzi wake? Jibu inaelekea litapatikana ndani ya wiki moja kutoka sasa.
Mkuu Nguruvi3, kwa mara ya kwanza Bernie Sanders ameonja joto la jiwe pale alipozomewa kwenye caucus ya Democrats alipotakiwa kusema ni lini atam-endorse Hillary Clinton lakini akasita kujibu mara moja. Hali hiyo imemshtua na sasa watu wanaamini kuwa sasa ni swala la muda tu atalazimika kufanya hivyo na siku ya Jumanne wiki ijayo Sanders ataungana na Clinton kwenye kampeni New Hampshire.SAKATA LA emails
MKURUGENZI AITWA KAMATI YA BUNGE
Mkurugenzi wa FBI bw Comey ameitwa kutoa ushuhuda wa email alilosema ilikuwa ni uzembe na hakuna ushahidi wa kumshtaki Bi Clinton
Siku moja baadaye mwendesha mashtaka akakubaliana na FBI kutofungua mashtaka dhidi ya Bi Clinton.
Comey akiwa Capito Hill alisisitiza Bi Clinton hakuongopa na hakuna ushahidi wa kumtia katika matata.
Hili la emails limezungumziwa na Trump katika mikutano yake.
Trump alisema ipo hongo kuwa Clinton atamteua Bi Lynch kuwa mwendesha mashtaka akichaguliwa-Rais. Madai yameonekana kuwa si ya kweli
Republican wakaharakisha kumwita Comey kumhoji kuhusu uchunguzi uliofunga jalada la Bi Clinton. Hili ni kosa la kisiasa kwasababu hawakujipa muda wa kutafiti namna ya kumbana bwana Comey aliyejiandaa vema
Hivyo kamati ya bunge ya GOP ilikurupuka katika kumwita Comey ambaye si kuwa anashadidia hoja yake ya juzi bali kwenda mbali na kusema Clinton hakuongopa. Hivyo, hoja za GOP zinazidi kufifia
Wakati huo huo Washabiki 'die hard fans' wa Sanders wamechukizwa na FBI. Hii ni karata ya mwisho kumrudisha Sanders katika convention Philadephia. Nao wanaungana na GOP katika vita dhidi ya Clinton
Pamoja na hayo, suala la emails linatumiwa Trump kumwelezea Clinto asiyeaminika, asiye mwadilifu na mwenye poor judgement.
Hoja hizi zilijengwa na Sanders aliyewafundisha GOP dhidi ya Clinton.
Democrat watambue anayewaumiza ni Sanders na atazdid kuwaumizi kwanini kampeni yake ilikuwa chafu dhidi ya Clinton.
Mpango wa Clinton kutokea katika mkutano na Sanders wiki ijayo hauwezi kubadili hali ya kisiasa hasa kwa wafuasi wa Sanders aliowajaza hasira
Inatarajiwa kura za maoni zitakazotoka wiki ijayo, Trump ataongoza na hili la emails ni tatizo kwa Clinton.
Hii kitampa Trump nguvu ya kuungwa mkono na GOP na wafadhili.
Je kuna ufanano wa kesi ya Gen. Patreus na Clinton katika uchunguzi na majibu?
Tutafafanua
Tusemezane
Naangalia tu democracy in action kwenye Republican Convention mjini Cleveland Ohio. Natamani Watanzania wangefuatilia jinsi chama cha siasa kinavyotakiwa kuendesha mkutano wake katika nchi zilizokomaa kidemokrasia. Sauti pinzani zinazimwa ama kwa maridhiano au kura na katu hazinyamazishwi kimizengwe. Kwa kweli tukubali tusikubali kuna mengi ya kujifunza ingawa si lazima tuyafuate.Mag3 Ha ha ha ha ha! si huko tu hapa nyumbani ilikuwa hivyo
Mkuu utakumbuka, Che Guivara, Bros Tito, Nkrumah, Gamal Abdel Nasar
Huari Boumedien, Mandela,Mondlane, Nandi Azikiwe, Tawafal Balewa, Mbiu Koinange, Dedan Kimathi, Nyerere, Hashim Mbita, Sir Churchill, FDR,Gandhi, Nehru, Olf Palme n.k. n.k.
Hawa ni wa karibuni tu, sasa linganisha na Sasa hivi, mhh dah!
Ahsante nafuatilia convention pia.Naangalia tu democracy in action kwenye Republican Convention mjini Cleveland Ohio. Natamani Watanzania wangefuatilia jinsi chama cha siasa kinavyotakiwa kuendesha mkutano wake katika nchi zilizokomaa kidemokrasia. Sauti pinzani zinazimwa ama kwa ama maridhiano au kura na katu hazinyamazishwi kimizengwe. Kwa kweli tukubali tusikubali kuna mengi ya kujifunza ingawa si lazima tuyafuate.