Update;Nadhani kwa upande wa Republicans kama ilivyotabiriwa Trump kashinda Indiana na hivyo Ted Cruz kulazimika kubwaga manyanga. Na sasa macho yanaelekezwa kwa Democrats na msimamo wa wajumbe baada ya Sanders kushinda Indiana ni kama ifuatavyo;
Hillary Clinton...2201 (bado...182)
Bernie Sanders..1399 (bado...984)
Tayari Sanders kasema hatoki, anaendelea...
Kazi ipo badoUpdate;
- Hillary Clinton...2202 (bado...181)
- Bernie Sanders..1400 (bado...983)
Sanders ameulizwa na CNN kwanini bado anaendelea. Kilichonishtua kidogo ni message yake kila baada ya mudaNadhani kwa upande wa Republicans kama ilivyotabiriwa Trump kashinda Indiana na hivyo Ted Cruz kulazimika kubwaga manyanga. Na sasa macho yanaelekezwa kwa Democrats na msimamo wa wajumbe baada ya Sanders kushinda Indiana ni kama ifuatavyo;
Hillary Clinton...2201 (bado...182)
Bernie Sanders..1399 (bado...984)
Tayari Sanders kasema hatoki, anaendelea...
Sasa Clinton atakuwa na wapinzani wawili, Sanders na Trump, katika hoja zile zile. Kaazi kweli kweli!Sanders ameulizwa na CNN kwanini bado anaendelea. Kilichonishtua kidogo ni message yake kila baada ya muda
1. Anasema yupo ili watu wa majimbo yaliyobaki sauti zao zisikike.
Hapa kuna tatizo kidogo, Republican wameshamaliza licha ya wakati mgumu sana, sauti anazotaka Sanders zina mantiki gani?
2. Kabadili kauli na kusema analeta msisimko mkubwa na hilo ni jambo jema
3. Mwisho anasema uwezekano wa kushinda upo na super delegates waangalie majimbo yao yalivyopiga kura na wamuunge mkono
Tunaposoma kauli zake, kuna kitu ambacho Clinton kampeni haijakiona. Hatujui ni kipi, lakini lipo jambo. Na Clinton kampeni imefanya move ambayo haieleweki.
Clinton hakukampeni Indiana kwa bidii, mara alikuwa west Virginia.
Inaonekana wanajipanga kwa uchaguzi mkuu na kupambana na Trump.
Lakini je, kwa haya ya Sanders ambayo hayaeleweki katika lugha nyepesi, bado wana Imani ya kuwa presumptive nominee?
Sanders amekiri 'tough hill to climb, but not impossible to climb' Kwa maana hii ataendelea kuleta uharibifu mkubwa sana kwa Clinton hata kama hatafanikiwa kuwa mgombea
Tayari kama alivyozungumza leo,Trump anatumia hoja za Sanders kuanzia wakati huu
Ingawa Sanders anakana hilo kwa kusema 'Republican wanafanya research zao' kumhusu Clinton, hakuna shaka kwa upande wa Democrat, anaacha makovu makubwa
Makovu hayo ni pamoja na lile la wafuasi wake kuendelea kuimba hawatampigia kura Clinton.
Katika hali ya 'frustrations' Sanders amewashambulia the Establishments kwamba ndio wanaotegeneza super delegates itakayomsaidia Clinton. Kauli yake inaweza kumgharimu
Hili ndilo linalowapa Democrat hofu kwasasa. Kwamba, mashambulizi kutoka pande zote yatamdhoofisha ClintonSasa Clinton atakuwa na wapinzani wawili, Sanders na Trump, katika hoja zile zile. Kaazi kweli kweli!
John Kasich naye kabwaga manyanga na sasa Trump hana tena mpinzani ndani ya Republicans, sana sana wanapigana vikumbo kumpa sapoti isipokuwa bado watu kama Lindsey Graham. John Macain na wengineo. Gingrich tayari anaonekana kuchangamkia nafasi ya U-Vice President, duh!Hili ndilo linalowapa Democrat hofu kwasasa. Kwamba, mashambulizi kutoka pande zote yatamdhoofisha Clinton
Wapo wanaojiuliza Trump amewezaje kubadili mwelekeo kwa muda mfupi?
Zipo sababu nyingi
1. Kampeni ya Trump iliposhinda majimbo 5 wiki iliyopita ilikuwa pigo kwa Cruz na Kasich
2. Muungano wa Cruz-Kasich ulionekana ni kukata tamaa,wafuasi wao walivunjika moyo.
Washindani wawili wanapoungana dhidi ya mmoja, ni dalili za udhaifu na kukata tamaa
3. Cruz kumchagua Fiorina nalo liliongeza hali ya kukata tamaa.
Fiorina hana tatizo isipokuwa mazingira yake ya kuingia katika kinyang'anyiro yalikuwa na utata katika wakati wa majeruhi
4. Wafuasi wa Cruz na Kasich walikata tamaa na kumwacha Trump akipiga pigo la mwhisho kwa kishindo usiku wa jana
5. Reublican wengi hawakaupenda kwenda convention tofauti na the establishments. Wengi wanadhani convention ingeleta uharibifu Zaidi ya
Lakini pia kuna jambo zuri alilofanya Trump. Wakati kampeni yake ikisuasua wiki chache zilizopita wapinzani wake Cruz na Kasich waliomba wawe na mdahalo.
Trump aliona hatari ya midahalo kwani ilikuwa ina mu-expose katika mazingira magumu huku wapinzani wake wakiona bora. Kwa mfano, wengi walitambua kuwa Kasich ni mzuri sana dakika za mwisho wakati wamebaki 3. Hilo lilipelekea Trump kupoteza majimbo
Inaelekea washauri wake walimzuia, kwa maana mbili. Kwanza kutotoa nafasi kwa wapinzani wake ndani ya GOP kustawi, na pili, kutokuwa na rekodi inayoweza kumuumiza wakati wa uchaguzi mkuu.
Mfano wa hili ni kauli za kuondoa majeshi nchi za mashariki ya mbali ambalo kitaalamu na kwa siasa za Marekani halikukubalika kwa wataalam hawaafiki
Hata hivyol, pamoja na RNC kutoa tamko la Trump kuwa presumptive nominee, bado kuna mtifuano ndani ya Republican. Tutafafanua hili
Kwa Democrat, ipo sababu nyingine Sanders anaendelea kuwepo, akitegemea litatokea jambo nje ya uchaguzi dhidi ya Clinton na kuweza kujenga hoja. Tutaliangalia hili pia
Tusemezane
Poll za siku za karibuni zinaonyesha Clinton akimbwaga Trump kwa point 13John Kasich naye kabwaga manyanga na sasa Trump hana tena mpinzani ndani ya Republicans, sana sana wanapigana vikumbo kumpa sapoti isipokuwa bado watu kama Lindsey Graham. John Macain na wengineo. Gingrich tayari anaonekana kuchangamkia nafasi ya U-Vice President, duh!
Huko kwa Democrats mambo bado kabisa, Bernie Sanders ameamua liwalo na liwe, atapigana mpaka mwisho. Hali hii inamweka Clinton katika hali ya wasi wasi na sintofahamu ya kuamua aendeshe vipi kampeni bila ya kuwaudhi watu wa Sanders ambao wengine wameonesha kusita kumuunga mkono Clinton.
Update;
Kiujumla super delegates wako 712. Kati ya hawa 561 tayari wamechagua upande na 151 bado. Katika waliochagua upande 522 wako kwa Clinton na 39 wako kwa Sanders. Wakati huo delegates wa kuchaguliwa Clinton anao 1701 wakati Sanders anao 1411, hivyo kwa sasa hesabu kamili iko kama ifuatavyo;
Kimahesabu hakuna namna Sanders atamfikia Clinton; hata hivyo Sanders anadai anao ushawishi wa kutosha kuwabadilisha misimamo baadhi ya wajumbe kwenye Convention. Hii inatokana na baadhi ya polls kuonesha kuwa ni yeye anayeweza kumshinda mgombea wa Republican, Donald Trump, kwa mbali kuliko Clinton.
- Hillary Clinton...1701+522 = 2223 (bado...160 kufikia 2383)
- Bernie Sanders..1411 + 39 = 1450 (bado...933)
Clinton kwa upande wake ameamua kuelekeza mashambulizi yake zaidi dhidi ya Trump wa Republican badala ya mpinzani wake ndani ya chama, Sanders.
Mkuu Nizipitiea hojaSalama wakuu,
Naomba na mimi niweke senti zangu chache kwenye mada hii:
1. Baada ya Trump kushinda kwa upande wa Republican ni vigumu sana kuona ni jinsi gani mgombea yeyote kutoka Democrat ataweza kumshinda kwenye Uchaguzi Mkuu. Sasa hivi mtu wa kumvuruga Trump ni yeye mwenyewe
Mvuto wa Clinton unaathiriwa na mambo mengi.2. Clinton pamoja na kubebwa sana na chama chake pamoja na Obama mwenyewe bado mvuto wake umepotea sana kiasi kwamba ni vigumu mno kuweza kushinda. Kwamba, mtu kama Sanders ambaye miaka michache tu nyuma (kama siyo miezi) Wamarekani wengi walikuwa hawamjua anampa shida itakuwaje kwa mtu ambaye ni maarufu, anajua kuchezea vyombo vya habari kama Trump? !
Kuhusu Trump kuungwa mkono na conservative, hapa ndipo atakabiliwa na tatizo kubwa. Hadi tunavyoandika kuna kundi la conservatives linataka mgombea mwingine (independent) ambaye ni conservative wakisema Trump siyo.4. Kitu kimoja ambacho watu wengi hasa wanaomkosoa au wasiompenda Trump (na wasiokipenda chama cha Repablikani) wasichotaka kuamini ni kuwa Trump ana mvuto mkubwa kwa Wamarekani wengi hasa weupe. Nchi hii bado kwa kiasi kikubwa sana ni ya weupe na wengi wa hawa ni wahafidhina (conservatives).
Wengi wameona jinsi gani taifa hili chini ya Obama limedhoofishwa hasa katika masuala ya ulinzi, usalama na masuala ya kifamilia ambayo wengi Wamarekani wanayaona ni tunu kubwa. Wanahofia kwa kiasi kikubwa kwamba Clinton akishinda utakuwa ni mwendelezo wa siasa za kiliberali za Obama.
Lakini zaidi pia mambo ambayo jamii hii ya Wamarekani wengi wanayajali wanaona yanawakilishwa vyema na Trump kuliko mtu mwingine yeyote - kupunguza kodi za mtu na za makampuni (corporate tax na income tax); kulijenga upya jeshi la Marekani, kupigana na ughaidi kwa ukali zaidi na kujenga heshima ya Marekani duniani - nikiyataja machache.
Nadhani kwa upande wa GOP mchezo umeisha na vita inayomkabili presumptive nominee, Donald Trump, ni kukubalika kwake na mapokezi kwa baadhi ya viongozi wa Republicans. Leo Spika Paul Ryan amesita kumuunga mkono akisema anasubiri kuona jitihada zake katika kuleta umoja ndani ya chama. Viongozi walioapa kutomuunga mkono ni pamoja na Mitt Romney aliyeshindwa na Obama.Mag3 #152
Sanders anatishia sana hali ya Democrat. Juzi katoa kamkana Trump kutokana na pressure inayoanza kujijenga ndani ya Democrat
Sanders ana madai mengi kuhusu uchaguzi. Kwanza, alidai closed election zina disfranchise vijana ambao ni wapiga kura wake.
Alipoulizwa mbona hajalalamika kuhusu caucus? Hoja ikafika ukomo
Anadai utaratibu wa Democrat si mzuri na ubadilishwe. Akiulizwa, alipojiunga na harakati za uchaguzi kitabu chenye blue print kilikuwepo,mbona hakuhoji hilo?
Kuhusu tuhuma za wizi wa kura, Sanders anafanya siasa za dhaifu sana.
Ukiangalia 'demography' na takwimu unapata majibu yote.
Clinton anakiri wapiga kura kati ya 18-30 hawampigii.
Mwanzoni namba zilionyesha wanawake wanampigia Sanders, Clinton alikiri ukweli
Clinton anashinda maeneo ya urban, sanders anashinda alikoshinda Clinton 2008. Clinton ana advantage,huko rural anashindana,mijini ana support (colored people).
Kundi la Clinton ni 'base ya democrat' ndiyo maana anashinda closed elections
Kundi la Sanders ni independents ndiyo maana anashinda caucus na open primaries
Ni wazi kwa kuangalia matokeo tunaweza kufanya forecast ya maeneo yajayo.
Sanders atashinda Oregon kwasababu 'electoral block' yake ni weupe.
Clinton ana nafasi kubwa California kwasababu ya colored people
Ukitazama ramani kwa undani, Sanders ameshinda red states kama Utah, Idaho n.k. kwasababu ya kile wanachosema ni independents.
Hawa si independents, ni Republican waliokuwa organized na Sanders team
Ndio maana uchaguzi wowote usiowahusisha Clinton anashinda tena sana
Chukulia mfano wa Connecticut vs Michigan. Utaona hayo tunayoeleza
Au Maryland, Pennyslavania, Florida Vs Wisconsin, washington, Utah, Idaho
Hoja za Sanders zinawapa GOP nguvu sana.
Ndio maana Trump ana sympathize na Sanders,hatendewi haki na Democrat.
Kila siku anachomeka hoja za kuamsha hisia ndani ya Democrat
Trump anajua Dem wakivurugana, wale conservative wanaoitwa independent wasiomtaka watagawanyika.Dem watagawanyika na hapo atakuwa na njia laini
Tusemezane
Mkuu katika bandiko #150 (ii) tulisema Trump anakabiliwa na changamoto ya upinzani ndani ya chama.Nadhani kwa upande wa GOP mchezo umeisha na vita inayomkabili presumptive nominee, Donald Trump, ni kukubalika kwake na mapokezi kwa baadhi ya viongozi wa Republicans. Leo Spika Paul Ryan amesita kumuunga mkono akisema anasubiri kuona jitihada zake katika kuleta umoja ndani ya chama. Viongozi walioapa kutomuunga mkono ni pamoja na Mitt Romney aliyeshindwa na Obama.
Kwa upande wa DEMS mambo pia bado magumu. Sanders ameapa kuendeleza mapambano ndani ya chama ingawa hesabu hazikubali. Mpaka sasa idadi ya wajumbe ambao bado wanaogombewa ni 1114 kutoka majimbo 15 ikiwa ni pamoja na California yenye wajumbe 546. Sanders anatakiwa apate angalau asilimia 87% ili afikie idadi inayotakiwa, kitu ambacho katu hakiwezekani kabisa.
Mkuu nadhani matatizo ya Trump unayoyataja ndiyo yale yale yaliyokuwa yanatajwa tangu mwanzo. Alichosema mwanakijiji ndiyo hali halisi. Kwamba vyombo vya habari vilijaribu sana kuyasema hayo kwa nguvu ili kumkwamisha trump lkn vimeshindwa,labda km watakuja na mbinu mpya ukiacha hizi zilizoshindwa.Kuhusu Trump kuungwa mkono na conservative, hapa ndipo atakabiliwa na tatizo kubwa. Hadi tunavyoandika kuna kundi la conservatives linataka mgombea mwingine (independent) ambaye ni conservative wakisema Trump siyo.
Ikifika wakati wa kuyaeleza kwa kina, na wakati umefika kwasabau watakuwa wawili, Trump atababaika zaidi na kuwagawa conservative.
Mfano, mwanzo aliunga mkono suala la 'abortion' akisema wanawake waamue hatma yao kama wanavyosema Waliberali.
Ilikuwa kutaka kuungwa mkono na akina mama. Kwa bahati mbaya lipo katika rekodi, na ndilo hasa akina Cruz walilitumia kuonyesha si conservative
Majuzi kaongelea Trans gender ya toilet akiwa na msimamo wa conservative.
Kuhusu Israel, Trump ana msimamo wa Democrat tofauti na ule wa GOP.
Ukimsikiliza Rubio na Cruz, misimamo yao ililenga kuwavuta conservatives.
Kuna flip flop za hapa na pale katika identity yake.
Kuhusu ulinzi na usalama, nani anaelewa agenda ya Trump?
Kuzuia Waislam wasiingie Marekani ita solve tatizo la Ugaidi?
Kuwatenga allies wa Uropa na middle east kutasaidia katika mapambano ya Ugaidi?
Kikubwa zaidi, Trump anapambana na gaidi yupi? Ukimsikiliza ana maanisha kwenda kuwatandika mabomu, swali wapo eneo gani?
Msimamo huo alikuwa nao Cruz kwa kusema atafanya 'blanket' kumaliza ugaidi.
Alipoulizwa eneo gani, hakuwa na jibu na si dhani Trump analo
Trump anaeleza mambo mengi yanayowagusa Wamerekani kama uhamiaji haramu, ugaidi, udhaifu wa uchumi n.k. katika 'sensational way''
Tatizo hakuna anayejua ana plan gani katika kukabiliana nayo
Mfano, anasema uchumi wa Marekani ni dhaifu ukishindwa na mataifa kama China.
Haraka haraka inaonekana kweli, kitakwimu si kweli.
Ni Taifa gani katika yale ya G20 lenye uchumi mzito zaidi ya Marekani kwa sasa?
Na je uchumi wa China ni mzuri kama Trump anavyosema?
Kwa miezi takribani 8 mfululizo namba za uchumi wa China zinaporomoka
Trump anawatisha watu kuhusu hali ilivyo mbaya, bila kuwaeleza ukweli.
''Atamaliza ISIS'' bila kueleza kwa mbinu gani ikijulikani siyo jeshi lenye eneo maalumu.
Wasi wasi wa baadhi ya Wamerekani ni jinsi ambavyo sera zake hazielezeki.
Utakumbuka katika primaries zote muda mwingi ametumia matusi, lugha chafu bila kueleza 'red meat' na hata aliojaribu alijikanganya sana
Kuhusu udhaifu wa jeshi la Marekani, hapa napo pana tatizo.
Ni kigezo gani kimetumika kubaini jeshi ni dhaifu?
Je, yale ya Bush kwenda kutandika nchi nyingine ndiyo uimara wa jeshi?
Na nani anajua jeshi la Marekani lina nini?
Walipobaki wawili, sera zitachambuliwa kwa undani kuliko wakati wa matusi
Democrat watafanya kosa wakienda mrengo wa matusi,Trump ni fundi hawatamweza.
Wakienda kwa sera, weledi wa Trump utaonekana na hapo pana tatizo kubwa
Exactly na hiki tumekiongelea sana kuanzia primairies na caucus zinaanza katika bandiko hiliNguruvi, utaona kuwa Trump hawagawi conservatives sana anawagawa Republicans; wale ambao wanaamini chama ni chao na kuwa huyu mgeni kaja na kakichukua. Republicans hawa (kina Paul Ryan, Mitt Romney, McCain na wengine) kwa kiwango kikubwa wanaona kuwa watu wao wote ambao wangewakilisha maslahi ya chama - kina Gov. Perry, Gov. Bush n.k hawakufanikiwa. Swali ni kwanini. Hawajajua bado mood ya Wamarekani wengi.
Conservatives wengi utawaona wanasimama nyuma ya Trump kwa sababu moja - wako tayari kumchukua 40% conservative kuliko 100% republican!