4. Kitu kimoja ambacho watu wengi hasa wanaomkosoa au wasiompenda Trump (na wasiokipenda chama cha Repablikani) wasichotaka kuamini ni kuwa Trump ana mvuto mkubwa kwa Wamarekani wengi hasa weupe. Nchi hii bado kwa kiasi kikubwa sana ni ya weupe na wengi wa hawa ni wahafidhina (conservatives).
Wengi wameona jinsi gani taifa hili chini ya Obama limedhoofishwa hasa katika masuala ya ulinzi, usalama na masuala ya kifamilia ambayo wengi Wamarekani wanayaona ni tunu kubwa. Wanahofia kwa kiasi kikubwa kwamba Clinton akishinda utakuwa ni mwendelezo wa siasa za kiliberali za Obama.
Lakini zaidi pia mambo ambayo jamii hii ya Wamarekani wengi wanayajali wanaona yanawakilishwa vyema na Trump kuliko mtu mwingine yeyote - kupunguza kodi za mtu na za makampuni (corporate tax na income tax); kulijenga upya jeshi la Marekani, kupigana na ughaidi kwa ukali zaidi na kujenga heshima ya Marekani duniani - nikiyataja machache.
Kuhusu Trump kuungwa mkono na conservative, hapa ndipo atakabiliwa na tatizo kubwa. Hadi tunavyoandika kuna kundi la conservatives linataka mgombea mwingine (independent) ambaye ni conservative wakisema Trump siyo.
Ikifika wakati wa kuyaeleza kwa kina, na wakati umefika kwasabau watakuwa wawili, Trump atababaika zaidi na kuwagawa conservative.
Mfano, mwanzo aliunga mkono suala la 'abortion' akisema wanawake waamue hatma yao kama wanavyosema Waliberali.
Ilikuwa kutaka kuungwa mkono na akina mama. Kwa bahati mbaya lipo katika rekodi, na ndilo hasa akina Cruz walilitumia kuonyesha si conservative
Majuzi kaongelea Trans gender ya toilet akiwa na msimamo wa conservative.
Kuhusu Israel, Trump ana msimamo wa Democrat tofauti na ule wa GOP.
Ukimsikiliza Rubio na Cruz, misimamo yao ililenga kuwavuta conservatives.
Kuna flip flop za hapa na pale katika identity yake.
Kuhusu ulinzi na usalama, nani anaelewa agenda ya Trump?
Kuzuia Waislam wasiingie Marekani ita solve tatizo la Ugaidi?
Kuwatenga allies wa Uropa na middle east kutasaidia katika mapambano ya Ugaidi?
Kikubwa zaidi, Trump anapambana na gaidi yupi? Ukimsikiliza ana maanisha kwenda kuwatandika mabomu, swali wapo eneo gani?
Msimamo huo alikuwa nao Cruz kwa kusema atafanya 'blanket' kumaliza ugaidi.
Alipoulizwa eneo gani, hakuwa na jibu na si dhani Trump analo
Trump anaeleza mambo mengi yanayowagusa Wamerekani kama uhamiaji haramu, ugaidi, udhaifu wa uchumi n.k. katika 'sensational way''
Tatizo hakuna anayejua ana plan gani katika kukabiliana nayo
Mfano, anasema uchumi wa Marekani ni dhaifu ukishindwa na mataifa kama China.
Haraka haraka inaonekana kweli, kitakwimu si kweli.
Ni Taifa gani katika yale ya G20 lenye uchumi mzito zaidi ya Marekani kwa sasa?
Na je uchumi wa China ni mzuri kama Trump anavyosema?
Kwa miezi takribani 8 mfululizo namba za uchumi wa China zinaporomoka
Trump anawatisha watu kuhusu hali ilivyo mbaya, bila kuwaeleza ukweli.
''Atamaliza ISIS'' bila kueleza kwa mbinu gani ikijulikani siyo jeshi lenye eneo maalumu.
Wasi wasi wa baadhi ya Wamerekani ni jinsi ambavyo sera zake hazielezeki.
Utakumbuka katika primaries zote muda mwingi ametumia matusi, lugha chafu bila kueleza 'red meat' na hata aliojaribu alijikanganya sana
Kuhusu udhaifu wa jeshi la Marekani, hapa napo pana tatizo.
Ni kigezo gani kimetumika kubaini jeshi ni dhaifu?
Je, yale ya Bush kwenda kutandika nchi nyingine ndiyo uimara wa jeshi?
Na nani anajua jeshi la Marekani lina nini?
Walipobaki wawili, sera zitachambuliwa kwa undani kuliko wakati wa matusi
Democrat watafanya kosa wakienda mrengo wa matusi,Trump ni fundi hawatamweza.
Wakienda kwa sera, weledi wa Trump utaonekana na hapo pana tatizo kubwa