Uchaguzi Marekani

Uchaguzi Marekani

Lakini kabla sijaendelea, ngoja niulize ili nijue kwa uhakika unazungumzia kauli ipi.

Ni kauli ipi hiyo ya Trump kuhusu watu weusi unayoizungumzia hapo?

Unaweza kuniwekea hapa hiyo kauli na chanzo labda cha ulipoitoa, tafadhali?
Mkuu nimezungumzia kauli yake kuhusu weusi. Hapa naomba uelewe, hatukuongelea usahihi au upotofu wa kauli yake. Tumesema, kauli zake zimewakirishisha weusi

Mfano mmoja ni kauli ya Trump alipokuwa anaongea Indiana(?) dhidi ya Wakenya na Waafrika. Ipo katika maandishi kutoka source mbali mbali.

Kwa ufupi, hakuna kundi ambalo halijaguswa na kauli za Trump katika jamii

Suala la usahihi au mapungufu ya kauli si sehemu ya mjadala, tunachokiangalia ni athari za kauli hizo mbele ya safari ya kampeni ikihusisha Republican

Ningefurahi kama ungeniuliza pia, wapi amezungumzia akina mama katika hali wasiyoipenda, waislam, immigrant n.k. kama nilivyoanisha katika bandiko

Mfano mwingine, Trump anamwita seneta 'little guy' na alipojibu hoja kuhusu ufupi wa vidole vyake, nadhani unajua alienda mbali kuzungumzia nini kuhusu..., anyways!



Ahsante
 
Mkuu nimezungumzia kauli yake kuhusu weusi. Hapa naomba uelewe, hatukuongelea usahihi au upotofu wa kauli yake. Tumesema, kauli zake zimewakirishisha weusi.

Mfano mmoja ni kauli ya Trump alipokuwa anaongea Indiana(?) dhidi ya Wakenya na Waafrika. Ipo katika maandishi kutoka source mbali mbali.

Okay, nimekuelewa.

Sasa basi, kwa taarifa yako, hiyo kauli inayodaiwa kuwa Trump aliwaongelea Wakenya na Waafrika kwa ujumla, ni ya uongo. Ni uzushi.

Unasema ipo katika maandishi kutoka source mbalimbali. Ni kweli. Lakini hizo sources si credible.

Nakuhakikishia kabisa kuwa, ukinipatia credible source yoyote ile kuhusu hiyo habari nitatoa dola 100 kwenda sehemu yoyote ile utakayoamua.

Hiyo habari uliyoirejea ilitungwa kwenye tovuti za tashtiti za Kenya na ikaenea kwenye mitandao hususan ya Afrika.

Marekani kwenyewe hakuna, narudia tena, hakuna chombo chochote kile cha habari kilichoripoti hiyo habari.

Kwa hiyo, kuhusu hiyo, umepotoka. Si habari ya kweli hiyo [na hapa sisemi Trump hajawahi kutoa kauli tata].

Bofya hapa usome zaidi:

Several African web sites claimed Donald Trump described black people as lazy and prone to crime, but we were unable to find any evidence supporting the rumor.

Kwa ufupi, hakuna kundi ambalo halijaguswa na kauli za Trump katika jamii

Suala la usahihi au mapungufu ya kauli si sehemu ya mjadala, tunachokiangalia ni athari za kauli hizo mbele ya safari ya kampeni ikihusisha Republican

Hapana, hapa sikubaliani nawe. Habari ya kwamba Trump aliwasema vibaya Waafrika na Wakenya akiwa huko Indiana ni ya uongo, uzushi.

Huwezi kabisa kusema kuwa hiyo habari ni ya kweli wakati si ya kweli.

Hivi unadhani ingekuwa ni kweli kasema hivyo isingeripotiwa na BBC, CNN, AFP, AP, Reuters, Al Jazeera, NBC, CBS, ABC?

Iweje hiyo habari iwe kwenye vi websites uchwara vya Kenya na nchi zingine tu za Kiafrika?

Mbona kauli zake tata zote zipo na zimesharipotiwa na vyombo vya kuaminika vya habari isipokuwa hiyo tu?

Ningefurahi kama ungeniuliza pia, wapi amezungumzia akina mama katika hali wasiyoipenda, waislam, immigrant n.k. kama nilivyoanisha katika bandiko

Sikuuliza hivyo kwa makusudi kabisa. Makusudi yenyewe ni kwa sababu hayo mengine hayana ubishi na karibu kila chombo cha habari cha kuaminika kiliripoti hivyo na video zake zipo.

Kwa hiyo siwezi kubisha kitu ambacho ni cha ukweli.

Nitabisha na kukikataa kile ambacho si cha ukweli, kama hiyo kuhusu Waafrika na Wakenya huko Indiana.

Mfano mwingine, Trump anamwita seneta 'little guy' na alipojibu hoja kuhusu ufupi wa vidole vyake, nadhani unajua alienda mbali kuzungumzia nini kuhusu..., anyways!

Naam, hiyo nayo ni kweli kabisa ingawa kuhusu mambo ya viganja vyake vya mikono hakuyaanza yeye. Na ni kweli kwa sababu hata kwenye mdahalo alilizungumzia na ushahidi huu hapa:



Kwa hiyo, mimi sikatai kwamba Donald Trump keshatoa kauli nyingi sana za utata.

Ninachokataa ni eti Donald Trump aliwasema vibaya Waafrika na Wakenya huko Indiana.

Huo ni uongo na uzushi unaolenga katika ku capitalize kwenye tabia yake ya kutoa kauli tata.
 
NN, ni vyombo vingapi vya habari vimeripoti kuhusu KKK?

Ukimsikiliza Trump hana kosa kuwa endorsed na KKK!

Ni vyombo vingapi vya habari vimeandika kuhusu kauli yake ya kutolijua kundi la KKK?

Anyways, hoja iliyopo ni kuwa hakuna kundi la jamii ambalo halijaguswa na kauli tata za Trump

Kwa mfano, katika hoja nimeongelea weusi wa Marekani wameguswa na kauli zake!
 
NN, ni vyombo vingapi vya habari vimeripoti kuhusu KKK?

Ukimsikiliza Trump hana kosa kuwa endorsed na KKK!

Ni vyombo vingapi vya habari vimeandika kuhusu kauli yake ya kutolijua kundi la KKK?

Anyways, hoja iliyopo ni kuwa hakuna kundi la jamii ambalo halijaguswa na kauli tata za Trump

Kwa mfano, katika hoja nimeongelea weusi wa Marekani wameguswa na kauli zake!

Mkuu, mainstream media yote ya Marekani iliripoti kuhusu hilo suala la Trump kushindwa kumlaani David Duke pamoja na KKK.

Kaka, mimi ni bonge la political junkie hususan siasa za Marekani.

Licha ya print media ya Marekani kuandika kuhusu hilo suala, hata kwenye broadcast media lilizungumziwa sana na ushahidi huu hapa chini.

Tuanze na CNN wakati Trump akihojiwa na Jake Tapper.



Tuendelee na CNN hao hao wakiliongelea hilo suala la David Duke na KKK kwenye kipindi cha Don Lemon.



Haya...twende kwenye right leaning media....FOX News....nao waliliongelea sana tu hilo suala. Hapa Megyn Kelly anamhoji Mike Huckabee, gavana wa zamani wa Arkansas.



Haya, twende kwenye left-leaning media...MSNBC.....nao walilijadili sana hilo suala. Ona hapa.



Hata Republican leadership kwenye Congress pamoja na Dems nao walilaani kushindwa kwa Trump kuwalaani KKK na huyo kiongozi wao wa zamani, David Duke! Angalia mwenyewe hapa chini hii clip ya AP [Associated Press].



Unaona jinsi ambavyo hii habari haina utata wowote ule? Au unataka hadi niweke makala za majarida ya Marekani yaliyoandika kuhusu hiyo habari?

Lakini, kwa wakati huo huo, hata nikikuomba chanzo cha magazeti ya kuaminika ya Kenya yaliyochapisha hiyo habari ya Trump kuwasema Wakenya, hutopata!

Utaishia kupata kimtandao cha Kenya kinachoandikaga habari za kizushi kuhusu wanasiasa wa Kenya kiitwacho politics.ke au kitu kama hicho.

Hiyo habari haikuwepo hata kwenye Daily Nation!

Kuhusu watu weusi kuguswa na baadhi ya kauli zake, hilo ni kweli na moja ya ushahidi ni huko kushindwa kwake kumlaani David Duke.

Ila, ile habari ya huko Indiana ni ya uongo, uzushi. Ni political satire tu.
 
NN, ni vyombo vingapi vya habari vimeripoti kuhusu KKK?

Ukimsikiliza Trump hana kosa kuwa endorsed na KKK!

Ni vyombo vingapi vya habari vimeandika kuhusu kauli yake ya kutolijua kundi la KKK?

Anyways, hoja iliyopo ni kuwa hakuna kundi la jamii ambalo halijaguswa na kauli tata za Trump

Kwa mfano, katika hoja nimeongelea weusi wa Marekani wameguswa na kauli zake!

Mkuu, nakuwekea viunganishi vya vyombo vya habari vilivyoandika kuhusu kauli ya Trump kujifanya halijui genge la KKK!

Tuanze na The Washington Post:

Why no one should be surprised that Donald Trump didn’t disavow the KKK

Time Magazine nao waliandika.
http://time.com/4240268/donald-trump-kkk-david-duke/
Donald Trump Refuses to Condemn KKK, Disavow David Duke Endorsement

USA Today nao waliandika mengi tu!

Trump blames bad television ear piece for KKK comments

Sasa mzee, hizo zote ni credible news sources!

Kuna credible news source gani iliyoandika kuhusu Trump kuwasema vibaya Waafrika na Wakenya?

 
JITIHADA ZA KUMZUIA TRUMP ZAENDELEA
TRUMP ANAKIDHI VIGEZO VILIVYOWEKWA!


Jitihada zinaendelea kwa 'the establishment' kuzuia ugombea wa Trump

Jitihada zinafanyika kukiwa na uchelewaji sana kama wangetaka

Baada ya kushindwa Iowa, GOP waliridhika njia ya Trump itakuwa na milima mirefu
Waliamini kama angeendelea huenda angebadilika katika kauli zake 'tone'

Trump ameshinda majimbo mengi kuliko wagombea wengine.
Ameshinda majimbo 12. Wagombea wanaofuata wakiwa na majimbo 7 na Kasich 1

Tulieleza sheria za GOP na Dem zinatofauti na zilivyo na ugumu katika kuzielewa
Kwa mfano super delegates wa Dem wanapatikana kwa mtindo tofauti na ule wa GOP

GOP waliweka utaratibu,pamoja na kushinda wajumbe mgombea ashinde majimbo 5.

Utaratibu una utata kwa tafsiri ya RNC ya mkutano mkuu uliopita unaotaka majimbo 8. Bado kuna mjadala kuhusu utaratibu huo unaoitwa Rule 40

Kwa vyovyote vile Trump kashinda kigezo hicho, na ana wajumbe wengi kuelekea ushindi

'GOP elite' watafanya nini kumzuia Trump katika hatua hii?

Wanajaribu kushauri kuunganisha tiketi ya Cruz na Kasich, jambo gumu kidogo

Uwezekano mwingine ni kuelekea mkutano mkuu.
Kwamba wahakikishe mkutano'unabadili' mwelekeo kama ilivyokuwa kwa Dem 1980

Ted Kennedy wa Dem akiwa na wajumbe wanaokaribiana na Carter alipeleka hoja DNC
Mzunguko wa kwanza wa kura Ted alishindwa na kuachana na suala hilo

Republican wana hofu kubwa kulipeleka suala hilo RNC.

Swali ni kuwa Trump kashinda uchaguzi kwa kura za wananchi, watafanya nini na nini matokeo yake kwa wapiga kura?

GOP elites wanaweza kujenga hoja,Trump atapata upinzani kutoka makundi ya jamii na kushindwa na Bi Clinton(assumption kuwa ndiye mgombea).

Hoja itajibiwa kirahisi, kuwa uchaguzi wa Marekani kura za watu 'popular vote' hazimchagui Rais, bali anachaguliwa na viti (electoral college).

Hapa ieleweke Rais hachaguliwi moja kwa moja, ingawa kura za wananchi kupitia wajumbe ndizo humchagua

Ndivyo ilivyokuwa kwa Al Gore wa Dem aliyepata kura nyingi(popular vote) kisha kushindwa kwa viti na Bush

Kinachohitajika ni viti 270 kati ya 538(electoral college).

Endapo Trump anashinda katika primaries na Caucus uwezekano wa kushinda viti upo hata kama hana popular vote. Republican elites wana wakati mguu kwa Trump

Tutajadili hili la electoral college na kwanini inawezekana kuwa na popular vote kubwa na kushindwa kupata viti 270 vya Urais

Tutaendelea
 
RAMANI YA UCHAGUZI KWA SIKU ZA KARIBUNI
Nilipitia jarida maarufu la 'wall street journal'' au WSJ na kukutana na ramani ifuatayo

All 2016 primary and caucus results so far

Ramani hii inaweza kuwa si timilifu kwa asilimia zote, lakini inatoa picha ya mjadala kuhusu majimbo yaliyopiga kura na kura za wagombea.

Inaweza kutusuaidia katika mjadala,kwa kutoa mwanga tu

Ukiweka cursor katika madirisha ya juu unaweza kuchagua kama unaTaka dem au GOP
Cursor katika jimbo itakuonyesha uchaguzi ulivyokuwa katika majimbo.

Unaweza kuchagua 'county' yaani vitongoji kupata picha ilivyo

Majimbo yasiyo na rangi bado hayajafanya uchaguzi

Tunasisitiza ni kwa ajili ya kutupa mwanga wakati tunaendelea na mjadala

Sehemu inayofuata tutaangalia kwanini Bi Clinton na Bw Sanders wanabadili mikakati

Na kisha tutazungumzia maandamano yanayoendelea dhidi ya Trump wa Republican

Maandamano yanatueleza nini siku za usoni?

Tuendelee
 
BI CLINTON NA BW SANDERS NA MIKAKATI

Katika bandiko #27 tuligusia kidogo kuhusu electoral college, jinsi Rais anavyochagulia.

Ni mapema kujadili suala hili linalochanganya sana kutokana na sheria au taratibu zake

Ni suala litakalohitaji mabandiko tarkibani 4 au 5 mfululizo.
Tumeonelea ni vema tuliweke kiporo hadi karibu na uchaguzi mkuu. litaeleweka vema.

DEM NA MIKAKATI TOFAUTI

Ushindi wa Sanders Michigan ulisemwa ni kwa kumwandama Clinton kwa hoja ya biashara 'free trade' .

Michigan iliathirika kufuatana na maoni ya wachambuzi. Eneo jingine lilikuwa Ohio

Sanders aliendelea na hoja hiyo Ohio akitumani ingemweka Bi Clinton pagumu
Aliwekeza sana katika matangazo akinasabisha free trade na Bi Clinton

Mkakati haukufaulu, 'Super Tuesday 3' Bi Clinton alimnyanyasa Sander kwa majimbo 5

Ushindi uliodhihirisha,hoja ya free trade si sababu ya Bi Clinton kushindwa Michigan

Ukitazama majadiliano na midahalo, Bi Clinton amejinasibisha sana na sera za Obama.
Mfano, anapigia chapuo Obamacare , sera zake zimelenga kuondoa mapungufu

Bw Sanders hakubaliani, na hawezi kueleza nini atafanya tofauti na Obamacare.
Kinachoonekana Bw Sanders anataka kuifuta, jambo la' risk'
Atanasabishwa na Republican wanaosema wataifuta Obamacare

Bi Clinton anasimama na Obama kuhusu climate change na kuwa alikuwa sehemu ya mafanikio ya makubaliano ya Paris.

Anaunga mkono kunusuru viwanda'bail out', na anajinasibisha na suala la nyuklia la Iran

Clinton naonekana amebeba kitabu cha Obama, anakazia maeneo yenye watu wengi.
Mwaka 2008 alishinda 'vijijini' na Obama kwenye miji ,sasa anafuata nyayo za Obama

Tatizo analokumbana nal0 ni vijana umri wa 19 hadi 30 wanaelekea kwa Bw Sanders. Wanawake waliotegemewa kumuunga mkono wanaelekea kwa Sanders!

Kwa hali hiyo, Sanders alimbana maeneo ya mijini akitumia vijana wa rika tulilosema na kugawana kura na Bi. Clinton huku Sanders akishinda vijijini.

Ndicho kilichotokea Michigan ingawa Sanders wanaamini ni hoja ya free trade

Jumanne Bi Clinton alibadili mwelekeo,kurudi vijijini, mijini akitumia kitaba cha Obama.

Hilo limembana Sanders na kupteza majimbo 5 kwa usiku mmoja. Ilikuwa ni pigo zito

Inaendelea....
 
SANDERS ABADILI MKAKATI
Ramani ya uchaguzi hadi sasa haimpi nafasi kubwa kama ilivyokuwa awali

Hoja ya kushinda maeneo kama Michigan, imezikwa na majimbo ya Illinoi, Ohi na Florida

Idadi ya wajumbe wanaohaidi kumuunga mkono haingozeki 'super delegates'
Na hoja ya free trade haionekani kuwa na mashiko mbele ya safari

Sanders anatambua ,siasa za kimataifa na za nje hawezi kusimama vema na Bi Clinton

Hoja kuwa anashinda maeneo mengi yakiwemo ya vijijini inaoenekana kukosa mashiko

Mkakati wa Sanders ni kuonyesha yeye ndiye anaweza kukabiliana na Trump

Sanders anasema kura za maoni zinampa ushindi dhidi ya Trump kuliko Bi. Clinton

Bw Sanders anataka kuitumia hoja hii mbele ya safari. Na tayari ameanza kurushiana kejeli na Trump akimwita 'pathological liar' yaani muongo katika hali ya afya.

Anachojaribu, ni kushawishi super delegates waone yeye ndiye atakabiliana na Trump

Hoja yake inajibiwa na Bi. Clinton anayesema, katika wagombea wote iwe republican au Dem yeye ndiye mwenye kura nyingi 'popular vote'

Hii maana yake ni nini? Kwamba majimbo yaliyobaki ni mengi, na ramani haimpi nafasi kubwa bwana Sanders, hivyo anajenga mazingira ya kushinda kwa wajumbe 'super delegates' kumuuunga mkono, au kushawishi hoja iende mkutano mkuu wa DNC

Kwa mantiki, uchaguzi wa Dem ni mbichi.Sanders anahitaji nguvu kidogo ajenge hoja

Bi Clinton akizembea kidogo tu anaweza kulipa gharama kubwa

Ted Kennedy alifanya jaribio hilo wakati wa Jimmy Carter ingawa lilishindwa katika mzunguko wa kwanza wa kura katika mkutano mkuu

Wote wawili wanaonekana kubadili mikakati kulingana na wakati

'Vurugu' zinazomkabili Trump kwa maandamano kwa njia nyingine zinamsaidia Sanders

Tuangalie maandamano yana picha gani!

Ni kwamba Trump hapendwi? Ni mkakati wa 'Republican the establishment''?

Nini kinaendelea hasa!

Tutajadili
 
MAANDAMANO DHIDI YA TRUMP
NI WAPINZANI WA DEM AU NI ' GOP THEESTABLISHMENT'' ?

Yamekuwepo maandamano dhidi ya Trump yaliyopelekea vurugu kwa baadhi ya maeneo

Hoja ya waandamanaji ni kumpinga Trump, haijulikani ni hasira zipi inayounganisha makundi yote.

Tuliwahi kusema , Trump ametoa kauli tata kwa makundi yote ya jamii
Waandamaji wanaonekana kumpinga Trump, kwa hofu ya kuwa mgombea wa GOP

Maandamano ya Chicago, Trump aliyahusisha na wafuasi wa Bernie Sanders
Ni ngumu kujua waandamanaji wanakereka na nini na ngumu kujua ni wafuasi wa nani

Kuhusishwa Bw Sander ni kutoa 'promo' Hakuna ushahidi wa wazi kuwa ni wafuasi wake.
Alichokifanya Trump ni kumpa Sanders publicity dhidi ya Hillary.

Trump anafahamu akisimama na Hillary ipo hatari kubwa kuudhi mbali ya hoja
Anaujua mtandao wa Clinton na kama ni kuchagua, Sanders ni bora kwake

Trump anafahamu Bw Sanders ana hasira ni rahisi kumvuta katika kejeli na si hoja

Lakini pia Sanders ana kashfa ya usoshalisti na video iliyotoka Miami katika mdahalo wa Dem, inamweka mahali pagumu si kwa Dem pekee bali uchaguzi mkuu kama atafanikiwa

Sanders anatumia fursa ya kutangazwa na Trump na ku 'engage' katika mijadala.

Lengo ni kuwashawishi ana wafuasi, anaweza kukabliana na Trump
Kwamba wajumbe (super delegates) waangalie uwezekano wa kumuunga mkono

Kitu kinachojitokeza , waandamanaji si wafuasi au watu wa makundi yaliyo katika mgogoro na Trump bali wamo Republican wakichagizwa na ' GOP the establishment'

Hoja ni kumonyesha Trump, mtu mwenye utata na jamii na GOP wana wakati mgumu katika uchaguzi mkuu dhidi ya Dem. Jitihada zinaanza kuzaa matunda.

Kiongozi wa Republican Bw Priebus amesikika na kukaririwa na media akisema anakiandaa chama kwa uchaguzi ndani ya mkutano mkuu (RNC)-contested convention, ikibidi

Hata hivyo amesisitiza, mgombea mwenye wajumbe wengi atakuwa mshindi!

Kauli ya kwenda RNC inaungwa mkono na Gavana Kasich kwa 'siri'

Mwezi mmoja uliopita Bw Priebus alikataa kuwepo uwezekano, sasa anabadili mwelekeo

Nini hatma ya haya, itaendelea

Trump Doctrine: Tough Talk, Blunt Policies, Stern Denials


Tusemezane
 
JE, TRUMP ANA MAKOSA KUTOKANA NA 'VURUGU'?

Baada ya vurugu za Chicago upo mjadala unaoendelea ukimhusisha Trump na vurugu

Wachambuzi wanaeleza hata kama si wafuasi wa Trump, bado ana dhamana ya kuhakikisha mikutano yake haileti sintofahamu

Trump anasema wanaofanya vurugu si wafuasi wake bali wanaowafuata mikutano
Akaelekeza nguvu kujibu hoja kuwa ni wafuasi wa mrengo wa kulia 'leftist' wa Dem

Akamtuhumu Sanders wa Dem akitarajia ugomvi utahamia Dem au atasukuma zigo Dem

Trump ana haki ya kutoa maoni yake na si vema kusema ni sahihi au la
Wapo wanaounga mkono, wapo wanaopinga. Hiyo ndiyo demokrasia ya Taifa kubwa

Kumzuia au kufanya vurugu katika mikutano yake hajatendewa haki na waandamanaji

Pamoja na uhuru wa maoni, Trump anadhamana na kauli, zingine zinavuka mipaka

Kwa mfano, anaposema Walatino ni wabakaji, alitakiwa awe na takwimu kuthibitisha.

Tunasisitiza hata kama ukweli upo lazima awe na ushahidi unaojitosheleza

Kauli dhidi ya Mwandishi M. Kelly wa Fox News ilienda mbali na kuwagusa wanawake.
Na mwendelezo wa kauli zenye hisia imekuwa kawaida

2008 McCain aliwakanya wafuasi wake kama Obama alivyofanya tatizo likitokea.
Wakiwa viongozi walichukua dhamana ya watu wao

Ilimpasa Trump kukemea mabaya na kuwausia wafuasi wake hata kama wamechokozwa
Dharau dhidi ya maoni ya wanahabari kuwa anapaswa kuchukua dhamana yanamgharim

Majuzi Trump amesema ingawa wafuasi wake wana kimuhe muhe (fervent) anawataka kuepuka vurugu hata wanapochokozwa! Too little too late!

Hiyo kauli alitakiwa aitoe mapema kabisa, sasa hamkani si shwari tena

Kauli imekuja baada ya kubaini the establishment wanaburuza uchaguzi kwenda RNC.

Imeandikwa, Priebus anaandaa chama kwa uchaguzi ndani ya RNC- contested convention
Hicho kimemuibua Trump licha ya kudharau kauli za wadau wakimtaka akemee uhuni

Maandamano yanayoendelea yana mikono mingi ''Anti-Trump Republican'' wakiwemo

Hili nalo linaeleza uchanga wa Trump katika siasa au ubabe unaoelekea kumgharimu

Ni jambo lilooenkana mapema akashindwa kubaini, sasa ni tembo sebuleni

Trump atakwepa kiunzi?

Tusemezane
 
Kwamba Donald Trump alitoa lugha chafu kwa Waafrika na kuwahusisha viongozi wa Kenya na Zimbabwe ni habari zisizo na ukweli wowote. Habari hizi zingekuwa ni za kweli basi zingekuwa ni leading news kwenye vyombo kama CNN, Al Jazeera, BBC not mentioning vile ambavyo vipo dominant US. Hata hivyo, huwezi kukuta hiyo habari zaidi ya kuonekana kwenye blog za Afrika, more possibly zikiwa zimezishwa na Kenyan Bloger!

Tukija kwenye mada yenyewe, hivi sasa sio siri tena kwamba wenye chama chao wana hofu na Trump... lakini mbaya zaidi ni hofu with conflicting forces!! Kumpa nafasi wanaogopa na kumkata wanaogopa... ni kama Lowassa kwa CCM hata kama baadae Lowassa alikatwa!!
 
JUMANNE YA MAGHARIBI (WEST)

Mtinange unahamia Uta, Idaho, Arizona na Samoa. Kwa Dem itakuwa Utah, Arizona na Idaho
Kwa GOP itakuwa Utah, Arizona na Samoa

Uchaguzi wa kesho umetanguliwa na matukio mawili.
Kwanza mkutano wa AIPAC, pili, majadiliano ua wagombea watano mmoja mmoja CNN-US

TUGUSIE AIPAC KIDOGO

Ni American Israel Public Affairs Committee.
Kundi la Waisrael wa Marekani wenye ushawishi (lobbying) katika mabunge au serikali ya Marekani kuhusu mambo ya Israel

Ni kundi kubwa lenye wafuasi wengi, lina nguvu za kiuchumi na ushawishi katika siasa za Marekani. Mwelekeo wa kundi hili unaendana sambamba na Reublica kwa kuangalia masilahi mapana ya Israel

Lipo kundi jingine linaloitwa J street , nalo kama AIPAC linasimamia masilahi ya Israel

Tofauti ni kuwa J.stree linamwelekeo wa kidiplomasia, AIPAC inasimama katika 'nguvu'
Kwa mtazamo wa haraka AIPAC inasimama na GOP, J.Street inasimama na Dem

Mkutano wa AIPAC umeleta viongozi wanaoshiriki kinyang'anyiro cha Urais wa Marekani
Aliyekosekana ni Bernie Sanders wa Dem ambaye amehutubia kupitia waandishi akiwa Utah

Wagombea wote wanaeleza sera za Marekani kusimama na Israel.

Hata hivyo, misimamo yao inatofautiana . Republican wanasema hakuna chaguo kusimama na Israel, Dem wanasema ni muhimu kuwa na suluhu kwa njia za kidiplomasia

Kilichojitokeza wagombea kutafuta kuungwa mkono na AIPAC yenye nguvu na ushawishi

Itakuwa si sahihi kusema AIPAC ndiyo pekee Marekani.

Hili ni moja ya makundi yanayojulikana kuwa na masilahi.

Ndivyo ilivyo kwa makundi kama ya Weusi(NAACP) au Walatino n.k.

AIPAC si pekee, upekee wake ni nguvu kubwa ya ushawishi na kicuhumi kuliko makundi mengine

Kwa siasa za Marekani, makundi masilahi yanajitokeza wazi kueleza misimamo yao bila woga

Wakati huu wagombea wakitafuta pesa za kampeni, AIPAC ni kundi muhimu kwao

AIPAC ni tofauti na kundi jingine linalojulikana kama Super PAC ingawa majukumu ni sawa

Tuangalie kwa ufupi nini Super Pack kabla hatujajadili hali ya kesho na misimamo ya wagombea

Itaendelea
 
SUPER PACs

inasemwa ni 'kamati ya wanaharakati' wanaokusanya pesa kwa shughuli za kisiasa iwe kumuunga mkono mgombea au chama.

Hawajihusishi na siasa moja kwa moja bali kutafuta fedha za kulipia ada mbali mbal

Super Pacs hawana ufungamano na asili ya watu au kitu kingine.

Ni wanaharakati wenye mahusiano na mashirika yanayotoa michango Dem na GOP

AIPAC ni kundi kwa ajili ya Waisrael wakati Supe PACs ni wanaharakati kama Kiswahili hicho ni sahihi. Lakini wote ni makundi masilahi katika siasa za Marekani.

Jinsi gani Super PACs inavyofanya kazi ni habari ndefu na inayochanganya
Ni ngumu kuweka mstari wa 'rushwa' na shughuli za Super PACs, hata hivyo ipo kisheria

Jarida la Wall Street linasema, Super PACs walikusanya takribani milioni 25 kumuunga mkono Marco Rubio aliyejitoa. Hii ni dalili ya Super PACs kuingiwa na kiwewe cha Trump

Super PACs inaonekana kundi linalonunua wanasiasa , hoja ya Sanders dhidi ya Clinton.

AIPAC
Mkutano haukuwa na jipya Zaidi ya siasa za kawaida za kuunga mkono Israel
Hata hivyo, Trump atatokea katika habari kwa maono yake ya siasa za nje za Marekani

Mjadala wa CNN-inaendelea
 
MJADALA WA CCN
Ulifuatia mkutano wa AIPAC kwa wagombea watano kuhojiwa na CNN mmoja mmoja

Donald Trump
Katika maswali aliyoulizwa , moja linalohusu kauli yake ya kuchochea vurugu(riot)

Trump aliyeonekana kuwa mtulivu na mwenye kuchagua maneno alieleza kuwa alichokisema ni kuuliza wafuasi wake endapo 'atakatwa' kama hawataleta vurugu(riot)

Ni kinyume na alichokisema siku za nyuma ikionyesha amebadili kauli 'tone' kuhusu 'riot'
Trump ameelewa vurugu zinamgharimu kwa sifa na ametoa wito wa kukataa vurugu

Mabandiko yaliyopita tulisema vurugu hazimsaidii Trump iwe zimefanywa na wafuasi wake au makundi mengine. Uwepo wa jina ni silaha inayotumika 'kmchinjilia mbali'.

Amegundua hilo ingawa kwa kuchelewa

Bernie Sanders wa Democrat

Ameeleza msimamo wake kuhusu Israel kwavile hakuhudhuria AIPAC.

Katika hali ya kushangaza msimamo wake umekuwa wa kati na kati na hata kuwanyooshea kidole Israel kwa madhara ya middle East

Inaweza kuwa ni msimamo huo ndio uliompelekea kutohutubia AIPAC kwani kufanya hivyo huenda angezomewa wakati kesho ana uchaguzi mzito.

Msimamo wake ulikuwa mzito dhidi ya Israel ingawa anaunga mkono Israel kujilinda.

Sanders ni Myahudi(Jews) na haieleweki alichosema alimaanisha au ilikuwa chenga

Alitumia fursa kumwandama Bi. Clinton kwa masuala ya Super PACs akisema yeye si establishment . Akiwa ni seneta hilo linabaki kuwa swali kama kweli si the establishment

Alipulizwa kwanini anaendelea kugombea akijua hali ya hesabu si nzuri kwa upande wake, Sanders alisema, ni undemocratic kumzuia mtu kuendelea na kampeni.

Pili , si kutenda haki kwa majimbo yatakayokosa primaries kama New York, California, na tatu,kampeni za muda mrefu zinajenga chama

Nne,katika jimbo la Utah ana Point 11 dhidi ya Trump na point 19 dhidi ya Trump Kitaifa

Hoja za Sanders zinaunga mkono tulizojadili hapo awali.

Kwamba lengo si kushinda bali kushinda majimbo ili awashawishi wajumbe (super delegates) ana uwezo wa kumshinda Trump. Na mwisho , kwama amevuta independent

Hafanyi ulinaganifu na Clinton, na akifanya anaonyesha udhaifu Clinton dhidi ya Trump

Anachokusdia ni kusogeza uchaguzi uende California na New York kwenye wajumbe wengi, na ushindi si kupata wajumbe bali kuonyesha ukubwa wa ramani anayoshinda

Kwa mantiki hii uchaguzi wa kesho bado ni muhimu sana kwa Bi. Clinton.
Kinyume chake Sanders atapata kujenga hoja ya kuelekea mkutano mkuu (DNC)

Sehemu inayofuata ttawajadili Clinton, Kasich na Cruz

Inaendelea...
 
Bernie Sanders

Kabla ya kujadili washiriki wengine, tuongezee kidogo kuhusu Mr Sanders
Hoja kubwa anayoongelea ni kubadili mwelekeo wa super delagates wamuunge mkono

Sanders ameunga mkono hatua za Obama kuhusu Israel na kumshambulia Netanyahu kwa kitendo cha kuhutubia Congress bila kumjulisha Obama.

Ame mshambulia Bi. Clinton kuhusu ushiriki wa Trump katika harusi ya mwanawe Chelsea. Hili lilikuwa kumfungamanisha Bi Clinton na Trump kama maswahiba

Sanders amemhusisha Bi. Clinton na Super PACs, kwamba amenunuliwa na wazee wa wall street wenye masilahi yao.

Tatizo la hoja hizi ni kuwaondoa Dem katika hoja na kuanza kurushiana vijembe.

Bi Clinton
Alikuwa na mtazamo zaidi wa uchaguzi mkuu zaidi hasa suala ;a immigration
Hakuwa na kauli nzito kwa mshindani wake, japo alionekana kumzungumzia Trump

Bi Clinton alisema amekuwa katika utumishi wa umma kuliko Sanders
Hivyo ni rahisi GOP kumshambulia kuliko Sanders

Gavana Kasich
Alitambua hesabu hazipo upande wake, anachokifanya ni kutengeneza mazingira yatakayopelekea kura katika Mkutano mkuu (RNC). Anaonekana kuwa mtulivu

Hoja yake kubwaM,anaweza kumzuia Trump kama alivyomzuia Ohio

Alipoulizwa kwanini asijitoe ikiwa asilimia 70 ya Republican wanamtaka kufanya hivyo
Kasich alisema yeye siyo 'quitter' na bado na anategemea ushindi

Anajivunia kura za maoni zinazoonyesha akisimama na Bi. Clinton atamshinda kwa asilimia 51 kwa 45 na kwamba ndiye pekee aliyeonyesha uwezo wa kukabiliana na Dem

Hii ndiyo hoja anayoitumia kubadili mwelekeo
Ujumbe wake ni kuwa Rep watakwenda kwenye mkutano mkuu(RNC)

Uchaguzi wa Leo
Kuna wajumbe takribani 360 wamaowamiwa na vyama vyote

Kwa upande wa Dem, ushindi wa Sanders lazima uwe katika kiwango cha asilimia nyingi
Lakini pia ushindi wa Bi. Clinton utaendelea kuipigilia msumari katika 'jeneza la Sanders'

Republican wana mtihani mkubwa kule Arizona ambako kuna wajumbe 59 na mshindi atachukua wajumbe wote. Kwamba, atakayeshinda popular vote atashinda wajumbe wote

Hapa, kama Trump akishinda atawaweka Cruz na Kasich katika wakati mgumu sana
Republican watalazimika kukubaliana na hoja kwamba Trump ndiye mshindi

Uwezekano wa kumshinda ni mdogo. Cruz na Kasich watagawana kura Trump akisimama na kundi lake.

Republican wangependa Kasich achie ngazi ili mpambano ubaki kati ya Cruz na Trump

Tatizo , Kasich kaonyesha uwezo wa kumzuia Trump, na Cruz haonekani kuwa mshindi

Kumuondoa Kasich kutafungua mafuriko kwa Trump.
Kumwacha Kasich ni kuendelea kugawa kura kati ya Cruz na Kusich

Hapo ndipo utata unapowakumba Republican

Tusemezane
 
DEM NA WESTERN TUESDAY
HESABU ZA LEO

Arizona ina wajumbe 75 katika siku ya leo. Uchaguzi ni primaries

Bi.Clinton anaoongoza kura za maoni ingawa uwezekano wa Sanders kushinda upo sana

Swali ni kuwa ushindi utabadilisha ramani ya wajumbe?

Kwa nadharia ikiwa Bi Clinton au Sanders mmojawapo atashinda, ni kati ya 45-50%
Hizi si habari njema kwa Sanders anayehitaji wajumbe wengi.

Ushindi katika kiwango cha 45 au 50 asilimia kunaaminisha kugawana wajumbe

Hii maana yake, kati ya wajumbe 75 tofauti inaweza kuwa wajumbe 5-8.

Kwa Bi Clinton ni ongezeko,kwa Sanders anatakiwa ashinde 60-70% kufidia upungufu

Uta na Idaho zina wajumbe 33 na 23, uchaguzi utakuwa ni Caucus.
Mtiririko unaonyesha Sanders kufanya vema katika Caucus na hivyo kutegemewa kushinda

Kwa namba zozote 50% au 60% bado idadi ya wajumbe ni wachache.
Majimbo yote mawili yana wajumbe 56 ukilinganisha na Arizona lenye wajumbe 75 pekee

Ushindi wa Sanders Idaho au Utah hauna wajumbe wa kumfikia Bi Clinton kwa ukaribu

Kama Sanders atashinda majimbo yote matatu , hoja kubwa itakuwa ni kuacha mchakato uendelee,atafanya vizuri California na New York yenye wajumbe wengi

Hata hivyo, leo Bw Sanders ana mtihani mgumu kwa maana moja.

Yamekuwepo mashinikizo kutoka kwa Dem yakimtaka aache kampeni ili Clinton aweze kujijenga tayari kwa uchaguzi mkuu.

Endapo kwa namna yoyote atapoteza majimbo yote au mawili, shinikizo litamwelemea

Kwa upande wa GOP hali ikoje hadi sasa hivi? Itaendelea...

Tusemezane
 
Asante Nguruvi3 kwa uchambuzi maridhawa kuhusu uchaguzi wa Marekani. Toka mwezi wa Januari nilikiuwa nahangaika na mods wa JF kwa nini wameninyima fursa ya kuchangia jukwaa hili na ni leo tu niliporuhusiwa kufanya hivyo ingawa sababu ya kuzuiwa sijapewa. Hata hivyo tuko pamoja na mathalan sina tena kizuizi na mimi nitatoa zangu "two cents" kwa wakati muafaka kulingana na hali halisi. Siasa ya Marekani ni ngumu ndugu zangu na hizi za sasa ni kama manyunyu tu, safari hii mvua za vuli zitakapoanza, asiye na mwana aanze kutafuta jiwe la kueleka...tuendelee.

Sina hakika wangapi wenu wameisikiliza hii;


 
Mkuu NasDaz hali inazidi kuwaelemea 'the establishment' kutokana na matokeo tuliyoyapata sasa hivi. Tutaeleza hali

Mkuu Mag3 Video hiyo inashadidia maneno ya Hillary Clinton katika moja ya midahalo
Hillary alisema, Bernie Sanders alimsema Obama kama weak president bila kujali 'antipathy' anayoipata kutoka kwa republican.....
 
Back
Top Bottom