Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.
chama kutegeme wazee kama mtaji wa kisiasa ni dalili ya kifo kibaya sana zaid hata cha mende
 
Ok wakuu mliopo eneo la tukio endeleeni kuangalia kwa makini na kudhibiti vitendo viovu vinavyoweza kuharibu amani yetu angalieni hao wagambo pamoja na jeshi la polisi msiwaamini sana jiridhisheni kwa kila jambo ili mradi hamvunji sheria iliwanainchi wa igunga wapate haki yao ya msingi yakumchagua kiongozi wanae mpenda sio kwa kurubuniwa na baadae wape shida toeni elimu stahili na mungu atawabariki.

Pia angalieni watu wanaokamatwa na polisi jiridhisheni kama kweli wana makosa isije ikawa janja ya nyani
 
Upigaji kura unaendelea huko Igunga. Watu wengi wamejitokeza na kura zinaendelea katika hali ya amani na utulivu.

Waliojitokeza kwa wingi ni wazee na kina mama.

Kwani wazee na kina mama (ina maana hakuna kina mama wazee?) wana shida gani au wanafikiri wazee ndo wa ccm?
 
Itv wanaripoti kuwa kunamtu kakamatwa ana shahada ambazo si zake, pia wao watu wamekamatwa wakiwa nakadi feki, zingine si zao na wengine wana kopi za shahada. Pia kuna vituo feki (hewa) vimeripotiwa.

Kazi hiyo waandishi wanafuatilia.
 
Vijana wa cdm wanajitahidi kudumisha ulinzi wa kura.kazi nzuri.
 
mimi naamini katika ukweli. Kama kweli watu walijitokeza wengi kupiga kura mpaka hivi sasa ni akina mama na wazee basi ccm itashinda uchaguzi. Akina mama na wazee bado ni kundi la watu linaloridhika sana na hali walionayo.

Hata wakiwa na matatizo, watalalamika lakini hawatachukuwa uamuzi wa kufanya mabadiliko. Na ccm inalijua sana hilo.

kwa maoni yangu, naona unatengenezwa uhasama baina ya jamii ya watanzania, wazee na akina mama hadhi yao itashuka sana kwani wanaonekana kujihusisha moja kwa moja kufanikisha tz kutawaliwa kwa hasara na li-ccm.
 
Jana niliandika mahali fulani kwamba tatizo kubwa linaloikabili chadema ni kwamba inapendwa na wapenda mageuzi ambao ni wapo busy na uzalishaji mali kiasi cha kwamba hawakumbuki hata kujiandikisha kupiga kura.

Kama kundi la wazee na wamama ndo lililojitokeza kwa wingi huko Igunga, basi CHADEMA waandike maumivu. Maana hili ni kundi lenye fikra za kizamani sana na linalodanganyika kirahisi na Kanga na kepu.
 
Itv wanaripoti kuwa kunamtu kakamatwa ana shahada ambazo si zake, pia wao watu wamekamatwa wakiwa nakadi feki, zingine si zao na wengine wana kopi za shahada. Pia kuna vituo feki (hewa) vimeripotiwa.

Kazi hiyo waandishi wanafuatilia.

Hilo la vituo feki vya kupiga kura linajulikana ndio mchezo wa ccm, tunachotarajia kusikia toka huko igunga ni namna gani vyama vya upinzani vimejizatiti kukabiliana na hizo kura za vituo feki.
 
polisi wamewaachia nakudai kuwa sio issue mtu kuwa na kadi zaidi ya moja au ya mtu mwingine....wameachiliwa mkuu

14.16pm - ITV/Radio One wameripoti kuwa kuna watu wamekamatwa kwenye kituo wakiwa na shahada halisi za watu wengine pamoja na photocopies. Inasuburiwa neno la polisi katika mkutano na waandishi baada ya muda.
 
Msimamizi anakana kuwepo na kituo hewa cha kupigia kura japo kimetajwa na wanadai viko vingi pembeni ya mji.haya twende.
 
chama kutegeme wazee kama mtaji wa kisiasa ni dalili ya kifo kibaya sana zaid hata cha mende

hii concept ya kina mama na wazee nimeisikia sana leo, tena wakati mwingine kutoka kwa mbunge fulani(jina kapuni). hivi hii dhana maana au lengo lake ni nini hasa wadau?
 
mi nashangaa yaani wanawakamata watu na pesa ya hongo halafu wanawaacha nazo matokeo yake wakina mchemba wanazichukua tena ha po polisi na kuziingiza tena kwenye mzunguko wa rushwa kupitia mtu mwingine
 
Inaonekana hali si nzuri kwa CCM, maana hata wale makuwadi wa Mafisadi humu JF wamekimbia gafla!

Kuna jamaa yangu Igunga ananihabarisha kuwa tayari watu wachache wameshaanza kusherehekea ushindi wa CDM pale kwenye vioski vilivyojipanga barabara ya lami kwenda Singida, mliopo vijijini huko hebu na nyie mzidi kutupa sherehe hii ikoje huko vijijini?
 
Vituo feki? Kwani hakuna list ya vituo vya kupigia kura katika huo uchaguzi?
 
Msimamizi anakana kuwepo na kituo hewa cha kupigia kura japo kimetajwa na wanadai viko vingi pembeni ya mji.haya twende.

Mkuu hizi ni fikra potovu, orodha ya vituo vyote ilitolewa kwa vyama vyote toka juzi, na walipewa hadi ramani na msaada wa kwenda kuvikagua, na vilevile msimamizi wa uchaguzi atajumlisha vituo vyote vilivyokuwa na mawakala wa vyama.
 
Kwa nini watu wa ccm wajivunie uwingi wa akina mama na wazee, na wapinzani wajivunie uwingi wa vijana. Vyama vyote vina jumuia za makundi yote. Na wapinzani hufanya kosa kwa kutokuwafikia akina mama. Watu wote ni wa vyama vyote. Endeleeni kutuupdate.

Usihofu.
Zama zileee ilikuwa inaonekana kama wazee na wamama ni nguvu ya ccm.....leo hii hali sivyo. Kila kada, umri, jinsia, rangi au kabila wanataka maisha bora ki-ukweli. Yaani wame-amshwa na wakaamka ...ccm wasijidanganye hapo.
 
Hata mimi sipendi hali hiyo ya mtu kutoa rushwa na polisi pamoja na usalama wa taifa wanaangalia tu ndio maana leo asubuhi nilisema tusiwaamini sana vyombo vya usalama tujiridhishe kwa kila jambo mtu kama huyo afadhali akatwe masikio maana hapendi amani na pesa zisipelekwe polisi afadhali wapewe watoto yatima na hao wazee wanao danganyika kwa ajili ya hali ngumu yawezekana hali duni ya wa tanzania ni mtaji wa ccm kwakuwa wataweza kuwarubuni kiurahisi watu masikini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom