Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.
Tumemkamata mgambo akiwa kwenye foleni ya kupiga kura huku akitoa rushwa ya shs 5,000/= kata ya Swingizi, baada ya kumweka chini ya ulinzi, tukamkuta na shs laki saba, kwa sasa anashikiliwa na polisi, anasema alitumwa na viongozi wa CCM.

Nchemba anapita kila kituo anamwita msimamizi na kumpa hela, kwa sasa amedhibitiwa na vijana wetu

Mhe PCCB wao wameamua kula mishahara ya walipa Kodi bure?
 
Kwanini hamkuchukuwa hizo fedha?
hebu fafanua mkuu azichukue halafu....yaani mfano polisi akikamata mwizi kaiba radio unashauli polisi aichukue hiyo redio au unaimanisha nini....
 
Nimeota CHADEMA imeshinda kwa ushindi mdogo huko Igunga, na kata 10 za udiwani katika chaguzi ndogo zimeenda chadema
 
alfred masako na fatma nyangasa wanajaribu kuchambua mchakato wa jinsi upigaji kura unaoendelea huko igunga. huyu mpigapicha anavyomuonyesha fatma kwa nyuma tu, anaharibu concetration
Wanataka wamchanganye Nchemba ili concentration yake ya kutoa hongo ipungue.
 
Kwa nini watu wa ccm wajivunie uwingi wa akina mama na wazee, na wapinzani wajivunie uwingi wa vijana. Vyama vyote vina jumuia za makundi yote. Na wapinzani hufanya kosa kwa kutokuwafikia akina mama. Watu wote ni wa vyama vyote. Endeleeni kutuupdate.
hilo liko wazi akina mama wangapi wanapata mda wa kutembelea mitandano kama JF...hivyo hivyo kwa wazee kuwaelimisha vijana hitaji nguvu nyingi sana tofauti na mtu ambae hata kusoma ni shida anaenda kwa kukalili tu...
 
All in all bado magamba mawili kwa mujibu wa nApe
Alisema kujifurahisha tu: Katuni 8.jpg
 
14.16pm - ITV/Radio One wameripoti kuwa kuna watu wamekamatwa kwenye kituo wakiwa na shahada halisi za watu wengine pamoja na photocopies. Inasuburiwa neno la polisi katika mkutano na waandishi baada ya muda.
 
Mimi naamini katika ukweli. Kama kweli watu walijitokeza wengi kupiga kura mpaka hivi sasa ni akina mama na wazee basi ccm itashinda uchaguzi. Akina mama na wazee bado ni kundi la watu linaloridhika sana na hali walionayo.

Hata wakiwa na matatizo, watalalamika lakini hawatachukuwa uamuzi wa kufanya mabadiliko. Na CCM inalijua sana hilo.
 
hebu fafanua mkuu azichukue halafu....yaani mfano polisi akikamata mwizi kaiba radio unashauli polisi aichukue hiyo redio au unaimanisha nini....
Kwani wao ni Polisi!

Hizo fedha zitarudi tena kwenye mzunguko wa hongo, kama wanazikamata na kuwaacha nazo.
 
alfred masako na fatma nyangasa wanajaribu kuchambua mchakato wa jinsi upigaji kura unaoendelea huko igunga. huyu mpigapicha anavyomuonyesha fatma kwa nyuma tu, anaharibu concetration

Ha ha ha haaaaaaaa...........!! Mbufyaaaa, umesomeka.
 
Tumemkamata mgambo akiwa kwenye foleni ya kupiga kura huku akitoa rushwa ya shs 5,000/= kata ya Swingizi, baada ya kumweka chini ya ulinzi, tukamkuta na shs laki saba, kwa sasa anashikiliwa na polisi, anasema alitumwa na viongozi wa CCM.

Nchemba anapita kila kituo anamwita msimamizi na kumpa hela, kwa sasa amedhibitiwa na vijana wetu
Are these people serious? How on earth can such stupid thing kutokea tena kwa kajimbo kamoja tu

Sisiemu you are more than tired, hakika mmetuchoka sana watanzania...halafu utalisikia lile jinga la NEC linakuja kusema CDM wanaleta vurugu, uko wapi sasa kuzuia chanzo cha vurugu kama ujinga huu....

Sipendi vurugu ila nikisikia mtu kama huyu kapigwa na hata kavunjwa na kung'olewa meno nitakuwa na furaha japo huzuni pia upande robo wa nafsi yangu
 
Inaonekana hali si nzuri kwa CCM, maana hata wale makuwadi wa Mafisadi humu JF wamekimbia gafla!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom