Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,176
kutoka kwa Wa Jikoni:
Chai kidogo:
Mama Ngesi alishindwa udiwani na "jembe" la CDM mwaka 2010, na jembe hili lilipoonesha tu nia ya kupambana na huyu maza, kwa mujibu wa Wa Jikoni, jembe hili lilichomewa nyumba yake, Hakusema kama jembe hili linaishi pangoni ama kwenye hema, ILA amesema vijana wamejipanga kuitia kiberiti nyumba ya Mama Ngesi kama uchakachuaji wa magamba utafanikiwa leo hii.
Mwisho:
Wa Jikoni anasema hali ni shwari. Ushindi wa Chadema unasubiriwa kwa hamu kubwa.
- Aliyekuwa mgombea wa Udiwani kwa tikiti ya CCM katika uchaguzi wa mwaka 2010, kwa jina Mama Ngesi, nyumbani kwake kumekuwa kukifanyika mchezo wa kupiga kura za maruhani, na Wa Jikoni anasema jumla ya kura 4000 zimekamatwa.
- Idadi hiyo hiyo ya kura 4000 imekamatwa huko mitaa ya kijijini na vijana wako macho kuhakikisha kuwa uchakachuaji haufanikiwi. Hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari aliyerusha sms kwa mwandishi mwenzake aliyekuwa kituo cha Stoo ambako Wa Jikoni aka Nkwingwa amepigia kura.
- Kwa mujibu wa Wa Jikoni, uchakachuaji ni marufuku na vijana wapo tayari kuwashughulikia wale wote watakaothubutu kufanya hivyo kwa gharama yoyote ile.
- Propaganda kwamba wazee na wamama ndiyo wamepiga kura, kwa mujibu wa Wa Jikoni haina mashiko kwa kuwa, kwa macho yake, licha ya kukiri kuwa asubuhi kweli kina mama walikuwa wengi, ukweli ni kwamba kadiri kulivokuwa kunapambazuka, vijana wengi wamepiga kura, na hiyo propaganda haitasaidia kitu kwani hata Wana-Igunga wameisikia na wanaifanyia kazi.
- (nilitaka kusahau). Wa Jikoni anasema kuwa kuna watu wa magamba wamedakwa na laki 7 vituo vya vijijini wakigawa mpunga kama wanavogawa uroda.