Uchaguzi 2020 Uchaguzi mkuu 2020 utakuwa mgumu sana kwa CCM na wapinzani wanaweza kutengenezewa mpenyo

Uchaguzi 2020 Uchaguzi mkuu 2020 utakuwa mgumu sana kwa CCM na wapinzani wanaweza kutengenezewa mpenyo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Uchaguzi mkuu wa 2020 utabebwa zaidi na kura za maoni kwa wagombea wa CCM ambao Kamati kuu ndio imeshika mpini.

Jaribu kuangalia tafrani zilizoanza kujitokeza za wabunge kugawa pipi kwa wagonjwa mahututi na wengine kwenda kuutimbatimba uwanja wa Sokoine na kuwahamishia maafande wa Magereza Samora Iringa.

Kuanzia January 2020 tutegemee vituko zaidi vya wabunge wa CCM huko majimboni hawa akina Mwita Waitara, Kibajaji, Jah people, Kigwangalla nk.

Pia tutegemee vijimambo vya kutosha kutoka kwa wabunge watarajiwa akina Jerry Murro, Le mutuz, Hajji Manara, Harmonize, Wema Sepetu, Kingwendu nk

Kiukweli kura za maoni zinaweza kuiletea tafrani CCM na kwa kuwa rushwa imedhibitiwa basi tutegemee masangoma wengi kutoka Senegal na Nigeria bila kuwasahau mitume na manabii kwa ajili ya kung'arisha nyota za wagombea.

Maendeleo hayana vyama

cc: Wakudadavuwa, tpaul
 
Hakutakuwa na kura za maoni. Watu watapita bila kupingwa. Iwapo kura za maoni zitapigwa basi wasiotakiwa watakamatwa na PCCB kwa kutoa rushwa.
 
Aje awakandamize zaidi watumishi wa umma.
 
Aisee kumbe Haji Manara, Wema Sepetu, na Harmonize ndio wabunge watarajiwa wa CCM!, na mtawaongezea kura za wizi kabisa kwa kutumia polisi wenu?!, halafu watanzania tunajiuliza kwanini hii nchi masikini, wakati tunatawaliwa na akili masikini miongo yote!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwa Haji Manara anaingia kwa gia ipi au ya viti maalum?
Kingwendu naye anaingia kama mgombea binafsi au?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mukubwa Mmawia nimeaka vibaya Sina hata thumuni,bado nipo kitandani nikiwa na mawazo Leo naishi vipi,lkn umenifanya Micheke mpaka vyumba vya jirani wanafikiri nimechanyiwa kuhusu manara na kungwendu.nimesaha njaa kwa muda.

Aksante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rushwa imedhibitiwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Na mimi nashangaa!
Nafasi walizopewa akina Waitara, Katambi, Kafulila, Machali, Mugwila, Kitila nk, pamoja na kumshawishi Diwani/ M'bunge ajiuzuru nafasi hiyo kutokea upinzani, na kumuhakikishia kuwa atakuwa mgombea na kuwa mshindi kwenye uchaguzi wa marudio, sio rushwa za wazi wazi hizo?
 
2020 kura zote kwa JPM ushindi 99.9%.

Hizi nyingine ni kelele tu mbele ya chama kubwa CCM.

Inawezekana na wewe ni mpiga dili umekatiwa mirija yako,..
 
Aisee kumbe Haji Manara, Wema Sepetu, na Harmonize ndio wabunge watarajiwa wa CCM!, na mtawaongezea kura za wizi kabisa kwa kutumia polisi wenu?!, halafu watanzania tunajiuliza kwanini hii nchi masikini, wakati tunatawaliwa na akili masikini miongo yote!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhe, hapo kwenye mstari wa mwisho umemaliza kila kitu.
 
2020 kura zote kwa JPM ushindi 99.9%.

Hizi nyingine ni kelele tu mbele ya chama kubwa CCM.

Inawezekana na wewe ni mpiga dili umekatiwa mirija yako,..
Jidanganyeni tuu, uchaguzi wa SM mlishindwa japo kwa miaka minne hamna washindani hadi mkaona mchakachue kwa kuwaondoa wagombea wa upinzani wote itakuwa huu ambao kampeni zitakuwepo?
Hadithi za ndege na reli unaenda kuwaambia wanakijiji wenye njaa ya elimu na ajira za watoto wao?
Ndio mtaiba kura na mizengwe mingi lakini kiukweli safari hii mtakufa wengi sana. Hakika nakuambia WEZI WA HAKI YA KURA ZA WANANCHI WENGI WATAUAWA.
Jiepusheni mkabidhi utawala kwa salama ili mponye roho zenu, hiki kizazi ni hatari sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sometimes kitu kinachoitwa demokrasia ni upuuzi tu!! sioni sababu ya kufanya uchaguzi wa 2020 (sana sana kwa nafasi ya uraisi) Magufuli anajitosheleza kwa kila jambo, kafanya makubwa sana na bado anaendelea kutekeleza miradi mikubwa ambayo ilikuwa ni historia. haiwezekani tusione thamani ya Raisi ambaye ndani ya awamu moja kafanya mambo ambayo yanameza karibia awamu zote halafu wapumbavu wachache bado wanabeza kweli? labda kama tunataka tuwachague wapiga madili ili turudi kule tulikotoka (serikali awamu nzima inajenga uwanja wa mpira mmoja tu eti ndo kumbukumbu yake.... mwingine awamu nzima anajenga daraja moja tu!..... mwingine awamu nzima anawaongoza watu kwa mtindo wa kuwawini kisaikologia kwa kuwambia kila kitu ni ruksa bila kudili na mzizi wa umaskini wa wananchi) ndo maana ilifikia hatua nafasi ya urais ilikuwa kama ya majaribio kila mtu alikuwa anaiwania ili akapige dili.. sasahivi magufuli karudisha hadhi ya urais kwa vitendo na kuonyesha kwamba nafasi ya uongozi ni dhamana, ni nafasi ngumu kama kweli una dhamira ya kuwatumikia wananchi na sio blaablaa...
 
Mkuu mbona kesha sema kuwa urais ni mzigo na kazi ngumu sana?

Sent using Jamii Forums mobile app

Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Hata Kagame alikuwa anasema hivyo hivyo. Lengo hasa la kusema hivyo ni kupima upepo anakubalikaje, ili ajue atatumia nguvu kiasi gani kuendelea kubaki madarakani.
 
Back
Top Bottom