Uchaguzi 2020 Uchaguzi mkuu 2020 utakuwa mgumu sana kwa CCM na wapinzani wanaweza kutengenezewa mpenyo


Hebu weka deni la taifa la hao marais na huyu ili tujue wapi la kuanzia.
 
Kura za maoni CCM 2020 ni salaam tosha kwa wale wazee wa njaa kali aka waungaji mkono juhudi wanakwenda kushikwa sehemu nyeti...hiyo ndiyo CCM...una thamani wakati wanakuhitaji tu...otherwise wewe ni dampo tu aka toilet paper ile used.
 
Kama uchaguzi wa 2015 CCM iliweza kuu-handle vizuri basi itachukuwa muda kutokea tena uchaguzi mwingine mgumu kwa CCM. Labda 2025, ila jinsi Lowassa alivyoondolewa kwenye kinyang'anyiro na jinsi ''alivyotulizwa'' pamoja na ufuasi wake mkubwa wa wajumbe na wabunge aliokuwanao, ilitengeneza precedent kwa rais yoyote atakayekuwa kwenye hali kama ile, iwe kwa wabunge au kwake mwenyewe. Hata Mkapa angekumbuka kufanya kama Kikwete alivyofanya, Kikwete asingepata urais ukitilia maanani alivyokuwa hamtaki. Tatizo la Mkapa hakuwa ''active'' akajikuta dakika za mwisho amezungukwa na watu waliokuwa wanamwambia mzee hapa hakuna tena ujanja bila yeye kujua kuwa hao wote walikuwa kwenye mtandao wa kina Kikwete. Ubunge CCM mwaka 2020 utakuwa na mchuano sana lakini hata watakaoondolewa kwenye kinyang'anyiro hawatakuwa na nguvu ya kupambana wakiwa nje.
 
Huu ni upuuzi unaandika hapa. Kama waliotangulia kuongoza mfano Nyerere, Mwinyi , Mkapa na Kikwete wangetaka kubadili katiba ili waendelee kushikilia madaraka, huyu mnayemuabudu sasa hivi angekuwa rais!? Punguzeni ujinga kutoka vichwani mwenu.
 
Kwanza uchzguzi utakuwa kiini macho. Na Kampeni zote kutoka kwa wapinzani, itakuwa wanamsindikiza tu raisi wa tume ya uchaguzi ambaye wao wanamjua hata sasa. Kwa tume hii na sheria hii ya uchaguzi, atakayeshinda anajulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunazungumzia wabunge na madiwani bwashee!
 
Haya maneno yamekuwa yanasemwa tangu tuanze mfumo wa vyama vingi. Na haijulikani ni lini yataachwa kusemwa!
 
Utakuwa mwendelezo wa yale ya serekali za mitaa. Usitarajie utofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…