Ivory Coast ilifanya uchaguzi wa urais Oktoba 25,2025, uchaguzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu lakini pia kwa hofu kutokana na misukosuko ya kisiasa iliyoikumba nchi hiyo wiki kadhaa kabla ya kupiga kura. Uchaguzi huu ulikuwa wa kumchagua rais wa Jamhuri ya Ivory Coast, nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa taifa hilo lenye wakazi takriban milioni 32 katika Afrika ya Magharibi
Hata hivyo, kampeni kuelekea uchaguzi huo ziligubikwa na hali ya sintofahamu, kujiri kwa maandamano, kukamatwa kwa mamia ya wananchi, na lawama nzito dhidi ya serikali ya Rais Alassane Ouattara, ambaye licha ya umri wake wa miaka 83, aliamua kuwania muhula wa nne baada ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2016 kuondoa ukomo wa mihula ya urais
Soma Ivory Coast: Wananchi maelfu waingia mtaani kumkataa Mgombea Urais wa chama tawala kugombea muhula wa nne
MATUKIO YALIYOJIRI
Viongozi wakuu wa Upinzani kuzuiliwa kuwania nafasi ya Urais
Mapema mwaka 2025 Tume ya uchaguzi (IEC) iliwazuia viongozi kadhaa mashuhuri wa upinzani kugombea urais. Miongoni mwa waliokataliwa ni Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa nchi hiyo, na Tidjane Thiam, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Credit Suisse
Sababu zilizotolewa ni uraia wa kigeni na masuala ya kisheria: Thiam alionekana kutostahili kugombea kwa kuwa alikuwa na uraia wa Ufaransa, huku Gbagbo akikosa sifa kutokana na hukumu za makosa ya jinai
Soma Tidjane Thiam aukana Uraia wa Ufaransa ili kugombea Urais wa Ivory Coast
Uamuzi huo ulilaaniwa na wapinzani wengi, walioutaja kama njama ya serikali kuhakikisha hakuna mgombea mwenye nguvu atakayemzuia Rais Ouattara kuendelea madarakani
Kukamatwa kwa Waandamanaji 237
Takribani watu 237 walikamatwa Oktoba 11, wakati wa maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan. Maandamano hayo yaliandaliwa na wanaharakati waliopinga kile walichokiita mwelekeo wa kimabavu wa serikali
Polisi walitumia mabomu ya machozi na kuweka vizuizi barabarani kuzuia maandamano kuanza, huku mamlaka zikisisitiza kuwa mikusanyiko yote ni haramu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi kwa sababu za kiusalama

Mahakama Ivory Coast iliwahukumu Waandamanaji 32 Miaka Mitatu Gerezani
Siku nne tu kabla ya uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25, 2025 mahakama nchini Ivory Coast iliwahukumu watu 32 kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kushiriki maandamano yaliyopigwa marufuku mapema Oktoba 2025
Hukumu hiyo ilikuja wakati vyama viwili vikuu vya upinzani nchini humo vikiwataka wafuasi wao kuandamana kupinga kuondolewa kwa viongozi wao, Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam, waliokatazwa kugombea urais. Waandamanaji hao walitiwa hatiani kwa makosa ya “kuvuruga utulivu wa umma” na “kukusanyika barabarani bila kibali.” huku awali watu wapatao 30 walipokea adhabu kama hiyo na zaidi ya waandamanaji 700 walikamatwa
Matokeo ya awali Rais Alassane Ouattara kuongoza kwa kura nyingi
Wakati siku ya kupiga kura ilipowadia Oktoba 25, 2025, takribani wapiga kura milioni 9 walijitokeza kumchagua rais mpya — au kumthibitisha yule aliyepo
Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya Tume Huru ya Uchaguzi (IEC), Rais Alassane Ouattara aliibuka mshindi kwa tofauti kubwa, akipata zaidi ya asilimia 90% ya kura katika ngome zake kuu.
Iwapo matokeo hayo yatathibitishwa rasmi, Ouattara ataendelea kwa muhula wa nne, hatua inayozua maswali kuhusu mustakabali wa demokrasia nchini humo
Wagombea wengine wa upinzani, akiwemo Simone Ehivet Gbagbo, mke wa Rais wa zamani Laurent Gbagbo, hawakuwa na rasilimali wala nguvu ya kisiasa ya kutosha kumpa changamoto Ouattara
Soma Mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast ateuliwa kuwania urais Oktoba 25, 2025
Matokeo rasmi ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa leo Oktoba 27, 2025 na kama ilivyotarajiwa, huenda yakamhakikishia Rais Alassane Ouattara ushindi mwingine — akiendelea kuiongoza Ivory Coast kwa zaidi ya miaka 15, huku wananchi wengi wakibaki kugawanyika kisiasa na kijamii
Source: African news, Associated Press (AP), ABC News & ICTJ

Wasiwasi wa Demokrasia na Mustakabali wa Taifa
Mwaka wa uchaguzi 2025 inaacha alama nzito katika historia ya kisiasa ya Ivory Coast. Wengi wanahofia kuwa nchi inaelekea kwenye utawala wa muda mrefu unaozidi kuondoa misingi ya demokrasiaMatokeo rasmi ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa leo Oktoba 27, 2025 na kama ilivyotarajiwa, huenda yakamhakikishia Rais Alassane Ouattara ushindi mwingine — akiendelea kuiongoza Ivory Coast kwa zaidi ya miaka 15, huku wananchi wengi wakibaki kugawanyika kisiasa na kijamii