Uchaguzi 2020 Uchaguzi Mkuu; Kuna haja ya kuchagua wanaojitengenezea kinga wasishtakiwe?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Moja ya sababu kubwa ya kuangusha utawala huu wa CCM ni hili la kuleta kwa hati ya dharula muswaada was marekebisho ya sheria ili kuongeza wigo wa viongozi wavunja sheria na Katiba kutoshtakiwa.

Hivi mtenda haki na mlinzi wa Katiba aliye APA kuilinda anawezaje kujiwekea kinga ya kuvunja sheria? Anaogopa nini hasa kama anaheshimu kiapo chake?

Hayo ni maandalizi ya kuandaa mpango wa kuvunja Katiba na sheria na VIONGOZI WA NAMNA HIYO HAWATUFAI.

Ni makosa makubwa sana kumkaribisha nyumbani mwizi anayekuambia kabisa kuwa anajiandaa kukuibia na anaandaa namna ambayo huta mshitaki.
 
"Katika uchaguzi huu Kuna haja ya kuchagua watu wanao support ushoga?"

"Katika uchaguzi huu Kuna haja ya kuchagua watu wanaotangaza Nia ya kugombea urais wa Tanzania huku wakiishi ulaya(kwa mabeberu)?"
 
Mbona ndani ya ccm kuna mashoga kibao na wengine ni ma RC ??? uliwahi kuhoji kuhusu teuzi za hao watu ??? kwn kuwa shoga unalazimishwa??
 
Mkuu Endelea kujibu na sentesi ya pili usiishie hiyo tu ya ushoga japo nayo huna udhibitisho wa majina Wala Nini Ila Mimi ninaongea na evidence e.g TL speach yake ya kutetea mashoga.
 
Kati mambo ya hovyo kuwahi kufanywa au kutendwa na watawala ni hili suala la kujiwekea uwingo wa kinga hata wanapotukosea au kuvunja sheria.
Tanzania imedhalilika sana kimataifa kwa uongozi duni wa awamu ya 5
 
Mkuu Endelea kujibu na sentesi ya pili usiishie hiyo tu ya ushoga japo nayo huna udhibitisho wa majina Wala Nini Ila Mimi ninaongea na evidence e.g TL speach yake ya kutetea mashoga.
Miaka ya 99 kurudi nyuma wabunge wa jinsia ya kiume walikuwa wanapanga guest chumba kimoja hapa dodoma.
Ndipo ilipozaliwa hakuna watu wa jinsia moja kulala chumba kimoja.
 
Moja ya sababu kubwa ya kuangusha utawala huu wa CCM ni hili la kuleta kwa hati ya dharula muswaada was marekebisho ya sheria ili kuongeza wigo wa viongozi wavunja sheria na Katiba kutoshtakiwa.

Hivi mtenda haki na mlinzi wa Katiba aliye APA kuilinda anawezaje kujiwekea kinga ya kuvunja sheria? Anaogopa nini hasa kama anaheshimu kiapo chake?

Hayo ni maandalizi ya kuandaa mpango wa kuvunja Katiba na sheria na VIONGOZI WA NAMNA HIYO HAWATUFAI.

Ni makosa makubwa sana kumkaribisha nyumbani mwizi anayekuambia kabisa kuwa anajiandaa kukuibia na anaandaa namna ambayo huta mshitaki.
Kujiwekea kinga maana yake wanajiandaa kusababisha maafa makubwa sana ndani ya nchi hii
 
Hatuna cha kuwafanya ndomana wanajiamini. Ingekuwa sanduku la kura ndo linaamua hakuna ambaye angethubutu kufanya hivi wakati imebakia miezi mitatu tu uchaguzi ufanyike. Ingekuwa nchi zinazojielewa hata hapo kwa majirani zetu tu Kenya haiwezekani kufanyika ujinga huu. Yaani ingekuwa ni tiketi ya kuwatupa nje ya uringo. Yaani mtu unajiuliza wanaogopa nini? Au wanataka kutufanya nii mpaka wajiwekee ma-firewalls kama yote?

Yaani wanataka kuweka firewalls kwa kila muhimili, anayesimamia kutunga sheria wanamlinda, anayesimamia kutafsiri sheria analindwa, na anayesimamia utekelezaji analindwa. Kwahiyo hapo cycle imekamilika kinaweza kutengenezwa kitu cha makusudi kinyume na katiba na kikapita stage zote bila kukwama na hakuna wa kubanwa, hakuna tena check and balance. Hakutakuwa na mwenye hofu ya kuvunja sheria tena watajifanyia lolote lile. Sijui hii kitu CCM wameitoa wapi itakuja kuwala wenyewe siku moja.

Mar. Mwl. Nyerere alishatuonyaga kuwa Katiba imempa madaraka makubwa sana akija mtu mbaya ataitumia vibaya. Sasa sisi badala ya kupunguza ili tuweze kuwajibishana ndo tunazidi kuongeza wigo na kuwalinda juu, hivi kweli sisi tuna akili kweli?????? Au vichwa vyetu vimebeba mate tu na makamasi tu[emoji51][emoji51].
 
"Katika uchaguzi huu Kuna haja ya kuchagua watu wanao support ushoga?"

"Katika uchaguzi huu Kuna haja ya kuchagua watu wanaotangaza Nia ya kugombea urais wa Tanzania huku wakiishi ulaya(kwa mabeberu)?"
Ukiwa bado hai lakini unafikra maiti ni jambo la kuhuzunisha sana. Hakuna tiba hapo Ila kusubiri tuu nawe uzime
 
Wanajiandaa kukwepa rungu la Tundu mara aingiapo Ikulu asiwashughulikie
 
Back
Top Bottom