Waridi
JF-Expert Member
- Mar 30, 2008
- 1,025
- 172
WanaJF,
Hii ni kutaka kukuhabarisheni kwamba ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi kinachondelea kwa sasa ni hatua za mwisho mwisho za kuhitimisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa kitaifa wa chama.
Kama ilivyo ada, kila baada ya miaka mitano unafanyika uchaguzi wa namna hii.
Itakumbukwa kwamba hadi sasa NCCR imekwisha kuwa chini ya uongozi wa wenyeviti wanne tofauti kwa nyakati tofauti
Katika uchaguzi huu, habari za ndani zinatonya kwamba wanaowania Uenyekiti ni wawili (sijajua kama wote watapitishwa)
Vile vile yaelekea nafasi nyinginezo kv. makamu mwenyekiti,katibu mkuu,naibu katibu mkuu,mweka hazina zitakamatwa na sura mpya kabisa kwa sababu wengi wa waliogomea nafasi hizo na wenye mwelekeo wa kushinda si wale waliokuwa wakizishikiria.
Wachunguzi wa mambo wanasema, mwelekeo huo ni ishara kwamba chama hiki kimepania kujijenga upya kabisa, ya kale yatapita...
Tega sikio, soon nitakuhabarisheni nani kang'olewa, nani kashinda, nani kawaje.
Duru zinasema mtanange huu ni Jumapili ya juma hili.

- alianza Mhe.Mabere Marando
- akafuatia Mhe.Agustine Mrema
- akaja Mhe.Aidari Maguto(marehemu)
- na wa sasa Mhe.James Mbatia