Pre GE2025 Uchaguzi mkuu ujao upinzani Tanzania uunganishe nguvu au wagombee hivi hivi kiholela kama kawaida?

Pre GE2025 Uchaguzi mkuu ujao upinzani Tanzania uunganishe nguvu au wagombee hivi hivi kiholela kama kawaida?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo mleta mada unadhani kwa mfano CHADEMA ikaungana na TLP, NCCR, CUF, CHAUSTA, UMD, UDP itakuwa na nguvu ya kushinda kuliko ikisimama yenyewe?
Yaani vyama rafiki na CCM ndio unataka viunganishwe na chama kikuu cha upinzani ili kuitoa CCM madarakani?

Embu tafari upya.
 
Kama kusingekuwa na Wizi wa kura unaofanywa na NEC kwa usimamizi wa vyombo vya ulinzi na Usalama,ikiwa kila chama kikasimamisha mgombea wake Chama pendwa hakiwezi kushinda uchaguzi.
wahenga walisema,
nanukuu.....

"aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea"

ukiwaza kushindwa ni lazima ushindwe tu 🐒
 
Kwa hiyo mleta mada unadhani kwa mfano CHADEMA ikaungana na TLP, NCCR, CUF, CHAUSTA, UMD, UDP itakuwa na nguvu ya kushinda kuliko ikisimama yenyewe?
Yaani vyama rafiki na CCM ndio unataka viunganishwe na chama kikuu cha upinzani ili kuitoa CCM madarakani?

Embu tafari upya.
kuungana ni kawaida tu na inawezekana. Mbona NLD waliungana na Chadema pamoja na ACT....

lolote linaweza kutokea na hiyo itasaidia kuficha kidogo hata ule ukibaraka wa kiongozi wa chama Fulani 🐒
 
Hakuna uchaguzi Tanzania bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Mtu mjinga tu, au anayefaidika binafsi ndio atajitokeza kushiriki hizo chaguzi za kishenzi kwa mazingira yanayopigiwa kelele kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Uchaguzi wa 2020 chini ya dhalimu Magufuli ulikuja kuweka mpaka wa kutoendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi. Bila mabadiliko ya kweli ni upuuzi kama upuuzi mwingine kuendelea kushiriki hizo chaguzi za kihayawani.
ukizira, ukisusa, ukigoma au vinginevyo haitakusaidia chochote wewe pamoja na wenye upeo kama wako 🐒

hata hivyo,
wakati wengine wakishiriki uchaguzi huru,wa haki na wa wazi, ni vizuri wewe na wengine mtakao kua mmefura, mkakaa nyumbani kwa utulivu bila kuwabughudhi watakao kua wanatumia haki zao za msingi kuchagua viongozi wanao wataka 🐒
 
Chama Cha Mapinduzi kipo imara zaidi kwa sasa kuliko nyakati nyinngine zozote zilizopita

Kaka chama chako kipo imara Sasa huwa unawashwawashwa na Nini kuhusu upinzani?
Hii inaonesha ndani ya ccm mambo hayapo sawa.
JF ni zaidi ya shule au darasa la siasa ukiwa serious kujifunza 🐒
 
Loooh huo mchezo waoishajaribu zilepesa wakashindwa kugaiana huyu anasema wana wabunge wengi apate hela zaidi loh
Utashi wa kisiasa ni kiduchu sio miongoni mwa wanasiasa 🐒
 
kibaraka anataka kumshtaki Rais eti kwasababu amepiga picha nzuri sana na Mbowe na viongozi wa baraza la wanawake yeye akiwa hayupo 🤣

hii unaizungumziaje kamanda 🐒
Ulijibu, ni nje ya mada uliyoleta🙏
 
Ulijibu, ni nje ya mada uliyoleta🙏
ukiuwa na maswali na majibu yako ya kufurahisha mfukoni matokeo yake ndio haya....

ukijieleza ndani ya mada kisiasa utajibiwa kisiasa tu 🐒
 
Wape ushauri CCM namna ya kuiba kura zaidi, ya wapinzani hayakuhusu.

Uliwahi kusikia shetani anatoa ushauri kwa muumini, halafu ukapokelewa?

Ushauri huu ungeupeleka kwa vile vyama 11, vitangaze wazi kuwa wagombea wake ni wale wa CCM.
 
Wape ushauri CCM namna ya kuiba kura zaidi, ya wapinzani hayakuhusu.

Uliwahi kusikia shetani anatoa ushauri kwa muumini, halafu ukapokelewa?
msije kunilaumu sikushauri 🐒

nimetoa maoni, mtazamo na ushauri wangu wa kitaalamu kwenu wapinzani. Ni hiari yenu bila shuruti yoyote, lakini pia ni wajibu wenu kidemokrasia kabisa, muuzingatie ushauri huu makini sana au muupuuze kwa manufaa au hasara yenu wenyewe baadae 🐒
 
Back
Top Bottom