Kweli unavyosema mzee yalikuwa maoni tuu,najua wengi watajitokezaWakati ukifika tutasema nani ni Bora zaidi kuliko wote kati yao maana kila mtu ataweza kusema kuwa anafaa kuliko mwingine kati yao
Wanabodi,
Maoni yangu kwa chama Chadema yataendelea kuwa yaleyale kuwataka waungane na vyama vingine nikiwa na maana vichwa vya watu toka pande zote wajipange pamoja kugombea uchaguzi mwaka 2010. Kama ilivyokwisha tokea, ikiwa vyama vingine havitaki kujiunga wbasi wale viongozi na wananchama wanaotaka Muungano wajiunge na Chadema kwa sababu nafasi yetu kujiunga ipo wazi kabisa..
Nifupi ktk mbinu za kujiandaa hata ikibidi kuwafuata na kuwaomba wajumuike na Chadema ktk kugombea mwaka 2010 basi jambo hilo lifanyike..
Pili, wazo la kiti cha Urais ni gumu sana kwa sababu wananchi huchagua jina la mtu na umaarufu wake. Ni lazima Chadema au Upinzani kama wataungana kusimamisha jina litakalo weza kuuzika kwa wananchi..Kama ingekuwa amri yangu Dr. Slaa pekee ndiye anasimama mbele ya Mbowe kwa umaarufu sasa hivi.
Na sidhani kama kuna ubaya kama akifuatwa mtu kama Salim.A Salim na kurubuniwa nafasi hiyo maadam tu Chadema ipate kupita mtihani huu wa kwanza. Nasema salim kwa sababu sii dhambi kabisa kuhama chama kwa sababu ya maslahi ya Taifa..
Kikwete ambaye ni rais wetu alitishia kukihama chama CCM ikiwa asingechaguliwa kusimama uongozi wa CCM..Hivyo basi kama kuna dhambi au makosa nadhani Kikwete alifanya kwa herufi kubwa..
Nionavyo mimi Salim A. salim anaweza kusimama na Kikwete na akashinda bila kutegemea ni sera zipi anakuja nazo kwani NDIVYO TULIVYO..
Na mwisho ni lazima Chadema wafahamu, waelewe na kuzingatia kwamba Wadanganyika wote - NDIVYO TULIVYO. Mbinu ,ahadi na maandalizi yote yafanyike kwa kufikira WATU na MAZINGIRA tunayoishi na siii Siasa nyingi za sera na mrengo wakati wananchi wenye njaa wanataka kuona ugali mezani..
Haya ni maoni yangu tu kutokana na jinsi nilivyowasoma wadanganyika..
Kuunganisha vyama kwa kweli mimi napinga sana napenda sana ninavyoona kuwa chadema inainuka kama chama chenya nguvu na kinachokua kwa nguvu ya ajabu,ningelipenda sana tuwe na chama kimoja kikubwa cha upinzani kitakachochuana na CCM
uzoefu umeonyesha wakiungna wanatumia muda mwingi kulumbana na kukashifiana kwa hiyo kwangu mimi ruksa kuwa na chama kimoja chenye nguvu
Wanaweza kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kwenye maslahi ya nchi kama kubadili katiba,kupambana na mafsadi,usalama wa taifa n.k.
kama wana JF tunaweza kuorodhesha majina hapa kutoka miongoni mwa wanajamii ambao tunaona wanaweza kusimamishwa kwa ngazi ya uraisi itakuwa changamoto yetu pia kuwajadili kwa kina tukitoa sababu kwa vipi atakuwa changamoto kwa JK ambaye anatakiwa aachie ngazi 2010 kabla hajaipeleka nchi pabaya zaidi amba[po itakuwa shida kurudi
Chadema waelekeze nguvu zao zote sehemu zote mijini na vijijini na walenge makundi yote kwa nguvu zote
Ukweli kabisa ila ni kupewa muda CHADEMA, wanaweza na kuna uwezekano kuwa kura za mwaka 2010 Jk atapata zaidi ya asilimia 60 hivi na ndio maana huwa nasema kuwa kuna ulazima wa kuunganisha nguvu ya chamaMkuu ni uzoefu gani huo?.. mimi nachofahamu vyama hivi havikukusudia kabisa kuungana toka mwanzo pamoja na kwamba Chadema walikuwa tayari na nadhani TLP ndiye mwanzilishi wa hoja hiyo. Tatizo limekuja baada ya vyama vingine kukataa kuunda chama kimoja na sababu kubwa ni Uongozi wa juu na hizi ruzuku..Kwa sababu kila mmoja wao anafikiria anayo shot to being elected akiwaweza kusimama kama mgombea..
Chadema kinaweza kuwa chama mbadala kwa kipimo gani?.. kumbuka hata asilimia 20 kwa Wabongo ni chama mbadala maadam chama tawala kina popularity ya zaidi ya asilimia 70. Hivyo kipimo halisi cha Mbadala, uwezo wa kupambana na CCM ni pale chama kinapoweza kufikia asilimia 40 ya umaarufu na hasa kwa viongozi wake kwani Tanzania hadi leo umaarufu wa chama unatokana na kiongozi. Sidhani kama Chadema wamefika huko hata kidogo lakini kama wataunganisha nguvu zao wanaweza kufikia asilimia 40.. mchezo ukabakia ktk kura za wale wasiokuwa na mrengo...
Kikwete kashuka Umaarufu na yawezekana imefikia asilimia 60 au hata 50 lakini tatizo ni replacement. Watu wengine wote walibakia hawana umaarufu kabisa na sioni ndani ya CCM kama kuna mtu mwenye Popularity sasa hivi..Mwandosya jina kubwa lakini halina mvuto kwa wakulima hivyo wanaochukua nafasi wengi wapo Upinzani lakini pia hawana nguvu kubwa kuweza kufikia asilimia 40, labda huyo Dr. Slaa na Salim kutokana na sifa walokwisha jenga.. Tukumbuke tu kwamba wapiga kura wengi nchi zote duniani ni wazee, vijana wengi huwa ktk mihangaiko ya kutafuta riziki hata siku ya upigaji kura..
Mwisho kuungana nakozungumzia mimi ni kwa watu, vichwa vya watu viungane badala ya vyama kwani jambo hilo limeshindikana. Wale wote wenye nia nzuri kwa taifa, warubuniwe wafuatwe na kupewa nafasi ktk uchaguzi mkuu kwani kinachotakiwa sasa hivi ni kuitoa CCM ktk Uongozi kisha baada ya hapo itajulikana mbele ya safari.. kama Kenya walipoweza kumsimamisha Mwai Kibaki (popular) against Moi na Mtoto wa Kenyatta. Wakachukua ushindi kuiondoa KANU ktk kiti cha IKulu, halafu wakaja tengana baada ya kutofikia muafaka wa kisera..Leo hii Kibaki na Raila (upinzani) ndio wanaongoza vyama vinavyopingana Kenya.. Kanu haina nafasi tena.
tundu lissu ni mtupu mbele ya kitila mkumbo.apewe nafasi hiyo kitila mkumbo kama kweli ni chama makini.kama wachangiaji wengine walivyo kwisha sema, mimi pia nadhani chadema waanze sasa kueleza ni nini watafanya tofauti na ccm pindi wakiingia madarakani. Mfano,
1. Wanaweza kuweka issues kwamba hawatakuwa na wakuu wa wilaya wa kuteuliwa isipokuwa watachaguliwa na wananchi na cheo cha mkuu wa mkoa kitafutwa.
2. Elimu ya msingi bure,
3. Elimu ya sekondari ni lazima kwa kila mtoto hadi form 4 na serikali itagharamia nusu ya ada ya watoto wote ktk sekondari za serikali.
4. Mishahara ya wafanyakazi itapanda kila mwaka kwa flat rate
5. N.k.
Kuhusu presidential candidate, mi nadhani mwanasheria tundu lissu anafaa kama atapendekezwa na chama.
Bila kuchukua hatua muhimu za kuonesha kujiandaa kuongoza, Chadema itaweza kuongoza? Uongozi ni maandalizi, asiyejiandaa kuongoza ataongoza bila kujiandaa! Matokeo yake ni kuburuzana.
Logically CHADEMA haiwezi kitu, haihitaji mwarobaini kulibaini hilo CHADEMA kuipa uongozi ni sawa na kununua mkate dukani harafu na kwenda nao sehemu wanakookea mikate.
simile hii haingii akilini. Labda uifafanue.
U can't boil an empty pot and expext soup. Can U ?