Hatuna haja ya kuuliza Cardinal Pengo au Askofu Kilaini kama Dr Slaa alifanya nini mpaka ikafikia aache au aachishwe upadre. Tunajua baada ya upadre alioa kama most of JF Members. Tunajua Slaa ni layman kama sisi, na kwamba ni mtu mwadilifu sana.
Pia tunajua Dk Slaa aliendelea kuwa mtumishi wa watu akiongoza Taasisi inayohudumia walemavu. Tunajua pia kwamba baada ya kuingia Bungeni, amekuwa shupavu na jasiri kufichua maovu ya mafisadi lukuki katika nchi yetu. Amejitolea, bila kujali usalama wake binafsi, kutaja wakubwa waliokwapua fedha za umma na kujitajirisha binafsi bila aibu.
Tunajua kwamba ktk Jimbo lake la Karatu ameleta maendeleo ya haraka, sio tu kwa kushirikiana na serikali kuboresha miundombinu kwa kutumia fedha zinazolipwa kama kodi na wananchi, bali pia kwa kuwasiliana na wafadhili wa nje moja kwa moja kuongezea juhudi za Tanzania. Dr Slaa ni mfano wa kuiga kwa Wabunge wote, wa Chadema na wa ccm. Karatu ni Wilaya iliyopiga hatua za mbele na za haraka tangu Slaa achaguliwe mbunge wao.
Hata hivyo, Chadema ina viongozi wengi wazalendo, jasiri, waadilifu na wenye uwezo. Juu ya yote, Chadema ni chama kinachoamini, kudhamini na kuheshimu demokrasia. Chadema kimeonyesha ktk historia yake tangia 1992 kwamba viongozi wake sio wang'ang'anizi wa madaraka au vyeo. Naamini kitaweza kutupatia mgombea mzuri atakayeweza kuongoza nchi. Kama ilivyodokezwa hapo nyuma, siyo lazima chama kiwe na uzoefu, na TANU haikuwa na uzoefu Waingereza walipowaachia Nyerere na wenzake.
Ningeshauri kwamba kwa sasa, wale viongozi wa kitaifa na wa kimkoa katika vyama vya siasa vya upinzani, wajifunze toka kwa Wifred Lwakatare na waungane na Chadema kuimarisha chama ambacho kimedhihirisha kwamba ndicho kitakachoweza kutoa changamoto kamilifu na ya kweli kwa ccm. Naamini ni kwa kutoa real challenge kwa ccm, ndipo nchi hii itaweza kupata demokrasia ya kweli na maendeleo ya kuridhisha wengi.
Nakubaliana kwamba kwa sasa juhudi lazima zifanywe ili Katiba ibadilishwe kuleta usawa ktk malumbano ya kisiasa. Tume ya Uchaguzi ni lazima ibadilike iwe ni Tume huru isiyopendelea Chama tawala.
Haya ni mambo yatakayofanyiwa kazi ktk kipindi hiki kabla ya Uchaguzi Mkuu, na yatafanikiwa zaidi endapo viongozi wa vyama vya upinzani watakiri sasa kwamba Chadema ndicho chama cha kuingia ili wafikie malengo. Nina hakika viongozi ndani ya Chadema sasa wataweza kuwa-accomodate wote watakaojiunga nao kuwaimarisha.