Uchaguzi ni upotevu tu wa muda na pesa usio na msingi

Kwa kuwa mnaona Mbowe na genge lake hawana chao mnaponda. Kama mnalijua hilo mbona mnashiriki miaka nenda rudi .SIZITAKI MBICHI HIZI.
 
Yani bora gharama za kuendesha kampeni + uchaguzi tungetumiwa kila mtu ktk cm then watuambie mfumo ya vyama vingi umeshindikana kwa nchi yetu basi maisha yaendelee
 
Naunga mkono hoja ifike kipindi tuambiwe kuwa hii nchi ni ya chama kimoja na hakuna uchaguzi maana t7napoteza muda na rasimiali pia
 
Mkuu usiseme kwenu ,sema kwetu labda kama sio Mtanzania mpenda mabadiliko
 
Oooh makamanda mshatepeta yale mapovu mliyokua mnabwabwaja tuliwaambia tarehe 28 mwisho wenu
 
Huo huo uchaguzi wao feki unawasaidia hao majambazi wa ccm kutambua ni kwa kiasi gani wananchi tumewachoka.
Kuna wakati mtu anajidanganya Hadi, anaamini ule uongo anao jidanganya Ni kweli

Mtoa Maada ana joja
 
Ushauri wangu kwa vyama mbadala najua hakuna Mbunge wala diwani hata mmoja mtakayempata, sasa wekezeni nguvu zenu kuhangaika kuitafuta katiba mpya
Kuitafuta haki na katiba mpya siyo kazi ya vyama vya siasa. Ukiseama hivyo tafsiri yake ni kwamba wewe unaridhika na kufurahishwa na mfumo uliyopo.

Kama wananchi hatutaweza kuwashinikiza watawala, katiba mpya itaendelea kuwa hadithi isiyo na mwisho.
 
Ni aibu kweli. Tumetumia mabilioni ya shilingi kuandaa uchaguzi alafu baada ya hapo tunaanza kuibiana, kukatana mapanga, kutekana, kupigana risasi.
Yani Waafrika tunashida sana
 
Umesema ukweli, tatzo sisi Watanganyika tunawapa majukumu makubwa vyama vya siasa, kwa haya yanayoendelea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, tungekuwa tunajitambua tungeshanukisha kitambo, mtu unaporwa haki yako unalalamikia vyama vya siasa, shame on us!
 
Mimi nimeshatoa mawazo na nawajibika pia kuwa sehemu ya huo mchakato lakini viongozi ndiyo wawe dira yetu
 
Umesema ukweli, tatzo sisi Watanganyika tunawapa majukumu makubwa vyama vya siasa, kwa haya yanayoendelea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, tungekuwa tunajitambua tungeshanukisha kitambo, mtu unaporwa haki yako unalalamikia vyama vya siasa, shame on us!
Watanzania kwa sisi vyama vya upinzani tulivyopambana mpaka hapa tumejitahidi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…