Hatimaye nimefanikisha tena.
Mwaka jana kuna vijana walikuwa wananitisha eti hawatanipa kura zao kwenye nafasi niliyokuwa nayo ya uenyekiti wa mtaa, na baadhi waliniamsha usiku wa manane na nikichelewa kuamka wanasema eti walinipa kura zao niwanyenyekee.
Asante Magu, sasa wananchi hamtutishi na mikwara yenu,tumerudi madarakani, na huto tu kura twenu hatutuhitaji, mtupishe na mkome,mmetutesa sana miaka michache hapo nyuma, oooh! fanya kazi,vinginevyo tutakuondoa kwa kura, fyoko fyoko, sasa kwa taarifa yenu, huto tukura twenu mkae nato, tumepita bila kupingwa na hamuwezi kutufanya lolote
Mnatamba eti mamlaka yanatoka kwa wananchi, shwaini, asilimia 99 tumepita bila nyie
Sijakupangisha foleni unipigie kura wala sijauza sera yoyote kwako wala kukupa ahadi ya uchaguzi a.k.a ilani yangu, usiniulize mambo ya mabarabara,maji,afya na elimu na mengineyo, unaniuliza kwani ulinipigia kura? Niliuza Sera yoyote kwako? Unanibana kwa lipi mwanaizaya wewe? Akina mama mnaodundwa na waume zenu mnajaa milangoni kwangu usiku kisa mlinipa kura,mkome, safari hii wanamtaa na wanavitongoji na vijiji hamjatupa kura zenu,mkome kutusumbua
Ntarudi
Kigumu Chama cha mapinduzi