Uchaguzi serikali za mitaa: Ambao hatujajiandikisha na hatuna mpango wa kujiandikisha tukutane hapa

Wacha tule buyu tu
 
Haha mkuu huendi hata kwa fimbo
 
Asipokuelewa basi tena
 
Naona uvivu hata nikijiandikisha sidhani kama kura yangu itasaidia maana matokeo yameshapangwa. kwanza kura zitapigwa siku moja kabla ya wengine wote hapo ndio kuna ukakasi siwezi piga kura
Aisee hadi wewe
 
Mimi sitajisumbua tena maana nina Passport na NaID
Na mvua hizi uache kulala zako ukapange foleni ya kupiga kura ambayo kwa vyovyote tu itapuuzwa
 
Yaani umeleta uzi jioni hii nagongewa odd. Naulizwa kama nimejiandikisha. Nikawajibu ndio. Wakasepa.
Aisee ndio wanapita nyumba kwa nyumba. Mimi wakiniuliza nawaambia sijajiandikisha na sitaki, nione watafanyaje
 
Mimi hata wazo tu sina.
Nipoteze muda kujiandikisha na kwenda kupiga kura ilhal matokeo yameshapangwa?
Bora nilale aiseh!
 
Wakajiandikishe tu maana Sjaona kipya ntakachogundua...
Maana mshindi tayari anajulikana na hata akichaguliwa tofauti baada ya miez sita anaunga mkono juhudi.
Wewe nilikuona jana kwenye kituo cha kuandikishia
 
Sasa hivi wanapita nyumba kwa nyumba!
 
mimi kilichonivunja moyo ni kauli ya rais aliposema haya wakat ana waapisha wakurugenz... NAKULIPA MSHAHARA NAKUPA GARI ZURI HALAFU UKATANGAZE WAPINZANI WAMESHINDA..... kauli hii umenifanya kuacha kujiandikisha tena napiga kampeni ya waziwazi kuhamasisha watu wasipige kura Kama yeye alivyowaambia Watanzania waziwazi kuwa wasitangaze wapinzani wameshinda
 
Huku tukielezana kwa nini hatujajiandikisha. Kwa upande wangu mimi naona uvivu....hivyo tu
Wale 'wazalendo' pia karibuni
Matokeo yanajulikana kwa hiyo kwenda kujiandikisha Ni kupoteza muda tu
 
Wote ambao hamtajiandikisha mpaka kufikia kesho mtachukuliwa hatua kali......Ice cream za ukwaju nyie.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…