Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

Kuna watu humu wanajipa moyo eti CHADEMA hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi.

Kama Kuna mtu anawaza hivo na anamanisha na ana amini Mawazo yake hayo yanaweza kuwa uhalisia, basi huyo ana tatizo kubwa sana kifikira.

Uchaguzi huu CDM iliyopalaganyika ikiwa inamtegemea mtu mmoja inakwenda kupambana na:
1. Rais Magufuli
2.Chama Cha Mapinduzi.
3.Watanzania

1.Rais Magufuli
Rais Magufuli tangu aingie Madarakani amekuwa akifanya baadhi ya Mambo ambayo yanakuwa reflected Kama ya kwake.Hali hii imemfanya pengine awe maarufu kuliko hata Chama chake. Magufuli amejijengea ufalme wake ndani ya mioyo ya Watanzania, siyo lazima akubalike na wote na hakuna anayetegemea iwe hivo, lakini ukweli umaarufu wake unamfanya yeye Kama yeye apate kura ambazo atapigiwa yeye Kama Magufuli, na nyingi ni zile za wasio na Chama.

Hizi kelele za mitandaoni dhidi ya JPM ukizifatilia ni za wale wale, hata thread humu ukiangalia wale wale ndio wanakoment, lakini waulize je Mama zao, Dada zao, wajomba zao, shangazi zao, Babu zao na Bibi zao wanaijua Facebook, wanaijua JF, wanaijua tweeter au Instagram. Jibu wanalo, je hoja ya Uhuru na maendeleo ya vitu inaeleweka kwa Hawa watu. Mtu ambaye hakuwahi kuona umeme( sizungumzii Maria Sarungi Wala Fatuma Katume, na Hawa hawafiki hata 5000) leo kauona umeme unaweza kumueleza asimchague Magufuli eti kwakuwa amemnyima Uhuru wakati anaenda kanisani, anapiga simu, anaenda sokoni anaenda shambani Bila wasiwasi akakuelewa?.

2. Chama Cha Mapinduzi
Dubwasha linalotisha, Dude hatari Barani Africa, dude ambalo Lina historia ya kuwaweka viongozi kadhaa wa Afrika Madarakani. Hili dude Lina vichwa, Lina Consultants, lina rasilimali watu na fedha za kutosha, Lina uzoefu wa kutosha katika anga hii ya siasa. Halafu Kuna mtu anawaza linaweza kushindwa na mtu anaitwa Tundu Lissu.

Hebu angalia muundo was CCM kuanzia hapo kwenye mtaa unaoishi, angalia kwa sasa kwenye eneo lako la nyumbani kumi muundo wa CCM, angalia WanaCCM hao katika muundo huo katika eneo Hilo la nyumba kumi walivyojipanga na wanavyoendelea kuzisanya kura kwa ajiri ya CCM. Sasa unaona, Kuna kura za Magufuli ambazo atazipata yeye na kura ambazo Chama Cha Mapinduzi kitazipata. Hali hii iliwahi kutokea mwaka 2005 ambapo Jakaya Mrisho Kikwete yeye Kama yeye alipigiwa kura na CCM nayo ikapata kura zilivyounganishwa mkwere akapiga 80%. Lakini 2010 watu wakawa hawana hamu naye, lakini Chama Cha Mapinduzi kikamtafutia kura. Akapiga 61% Kama sikosei, hizi zilikuwa za Chama.

Najua wengi mmejaa kwenye Social Media, hamupo field, hamuoni huo muundo ulivyo hatari. CDM is no where, katika level hizi, CDM ipo mgongoni kwa Lissu. Upande mwingine Kuna CCM Kuna Magufuli na Kuna CCM.

Sasa ukiangalia hali ilivo Sasa unaona kabisa atapigiwa parefu, lakini bahati mbaya hata upande wa Wabunge Mambo ni magumu mno. Majimbo ambayo siku za nyuma yalikuwa ni hoja isiyobishaniwa Sasa mwaka huu ni hoja nzito, Pale Mbeya Sugu amekamatwa Ke....nde, na Dr. Tulia, Lema ameshikwa Pu....bu, na Gambo, hapo Arusha, Mbowe jasho linatirtika hadi kwenye meno, Mzee wa Kondoo wa bwana anapumulia Kisogo Cha Halima. CDM ni Kama wapo kwenye furushi ambalo tarehe 28 linadondoka.

3. Watanzania
Sisi tunayo Kariba ambayo tumejengewa na Mzee Baba mwenyewe, Mchonga, Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere. Ni Kariba ambayo unaweza iita utakavyo kulinga a na muono wako, Njema sana, Mbaya, woga, au uungwana.

Watanzania tunapenda Amani Bila kujali gharama yake, Watanzania ni wavumilivu bila kujali gharama, Watanzania tunapenda uungwana sana, hatupendi Shari, lakini mbaya zaidi tunayo Imani Kali kuwa Mabeberu ni watu hatari, na watu wabaya sana. Lakini sisi ni wanafiki, Watanzania ukiwa na sisi tutakueleza hivi, ukitoka tunafanya tofauti, Tunakutanguliza halafu tunasikilizia, upepo ukibadilika tunaingia mitini!

Watanzania ukishaonyesha dalili za ushari, dalili za kuleta uvunjifu wa Amani au ukajinasibisha na Mababeru, au ukasingiziwa Mambo hayo, basi sisi Watanzania tunachofanya, tunakukwepa.

Tarehe 28 Watanzania bila kujali gharama, bila kujari Lissu anaahidi nini Watamkwepa, watajiepusha naye.
Msisahau hapa sijazungumzia swala la CCM kuwa Chama Dora!!

Nimevaa ngao🤣🤣🤣
Uliwaambia hawakusikia; wakumbushe tena kuwa majuto ni mjuukuu. Sasa hivi taktik yao ni kutaka wote tuwe ma-loser kama wao, na hatutaki!
 
Watanzania wa wapi unawasemea? au watanzania wako binafsi hapo ulipo? Tambua kuwa huu ni mwaka 2020 tayari watanzania wametaabika kwa mateso manyanyaso makubwa wana machungu hasira kubwa hawataki kusikia history za huko nyuma wanakuja kivingine kabsa kusaka Haki na uhuru toka kwa Mkoloni kaburu mweusi
Nadhani sasa umeelewa alikuwa anawasemea Watanzania gani.

Yes ni Hawa waliompa Lissu 13%
 
Uliwaambia hawakusikia; wakumbushe tena kuwa majuto ni mjuukuu. Sasa hivi taktik yao ni kutaka wote tuwe ma-loser kama wao, na hatutaki!
Wanazengo wamegoma Kama vile hawawaoni
 
Zile propaganda zenu mmeona zilipowafikisha!?
Mtu akitoa hoja mnadai analipwa, sijui anajikomba, sijui mnafiki sasa mmeona nguvu ya Buku 7!?
Ni kipigo cha mbwa koko, shubaaaaaamit
Mkuu hawa watu wamefundishwa hivo ndivyo walivyoteseka hata huko kwenye magroup ya WhatsApp ni hivo hivo
 
Chama hakiwezi kutunza raslimali zake halafu eti wanataka kuwape raslimali za taifa, si wataziparanganya kama matineja wakipewa credit card. Watu wehu kabisa hawa.
Hatari sana
 
Wako wapi wale wakufunzi wa lissu, wapige vigelele wa lissu, jamani jitokezeni utabiri umetimia uku kutoka kwa nabii
 
Jaman wanaojua process za kufuta chama cha siasa watuambie
 
Nadhani sasa umeelewa alikuwa anawasemea Watanzania gani.

Yes ni Hawa waliompa Lissu 13%

Hata mimi nimeelewa mkuu. Kumbe "watanzania" ni wale NECccm, ZECccm, brutal POLICEccm, TCRAccm, MIJIZIccm, na dada zao wote.

Bila kuwasahau wale MALAIKAccm wazima mitandao.

Kuwa na amani. Nimeelewa mkuu.
 
Hata mimi nimeelewa mkuu. Kumbe "watanzania" ni wale NECccm, ZECccm, brutal POLICEccm, TCRAccm, MIJIZIccm, na dada zao wote.

Vila kuwasahau wale MALAIKAccm wazima mitandao.

Kuwa na amani. Nimeelewa mkuu.
Hao hao mkuu mliowaambia waingie Barabarani wakagoma
 
Hata mimi nimeelewa mkuu. Kumbe "watanzania" ni wale NECccm, ZECccm, brutal POLICEccm, TCRAccm, MIJIZIccm, na dada zao wote.

Vila kuwasahau wale MALAIKAccm wazima mitandao.

Kuwa na amani. Nimeelewa mkuu.
"Chama kinachoshinda uchaguzi ndicho kinachotekeleza Ilani yake na kushika dola." Ukiona hayo ma-CC mengi kwenye kila taasisi, jua wananchi wameiridhia Sisiemu kwenye sanduku la kura.
 
"Chama kinachoshinda uchaguzi ndicho kinachotekeleza Ilani yake na kushika dola." Ukiona hayo ma-CC mengi kwenye kila taasisi, jua wananchi wameiridhia Sisiemu kwenye sanduku la kura.

Mtu akiliwa tunda si lazima kuwa aliridhia. Ndiyo maana pana kesi za ubakaji. Au siyo jombi?

Ni sanduku la kura au ni wizi wewe unafikia vipi hitimisho hapo bila ya kuwa referee aliyejuu huru?

Hayo ma-CCM unayoyaona wengine nao wanaona ni ya ubakaji mtupu.
 
Mtu akiliwa tunda si lazima kuwa aliridhia. Ndiyo maana pana kesi za ubakaji. Au siyo jombi?

Ni sanduku la kura au ni wizi wewe unafikia vipi hitimisho hapo bila ya kuwa referee aliyejuu huru?

Hayo ma-CCM unayoyaona wengine nao wanaona ni ya ubakaji mtupu.
"Sikilizeni, ndugu zangu. Pipoz! Pipoz! Pipoz! Tutashinda uchaguzi huu kwa Tume ya Uchaguzi hiihii." ~ Mr Mzungu

"Ninyi pigeni kura; kazi ya kuzilinda niachieni mimi, sawa?" ~ GB Limau, Arusha Mjini.
 
"Sikilizeni, ndugu zangu. Pipoz! Pipoz! Pipoz! Tutashinda uchaguzi huu kwa Tume ya Uchaguzi hiihii." ~ Mr Mzungu

"Ninyi pigeni kura; kazi ya kuzilinda niachieni mimi, sawa?" ~ GB Limau, Arusha Mjini.
Nemo ubakaji uliliona kwenye bandiko langu?

Tafadhali jiridhishe isije kuwa umechanganya madesa.
 
Back
Top Bottom