Malinzi bado anatufaa sana ktk soka letu. Amefanya mengi mazuri, me ntabainisha machache hapa.
1. Mpira wa miguu sasa unachezwa wilaya zote nchini
2. Amefanikiwa kurudisha ligi kuu ya wanawake
3. Chini ya uongozi wake, tz sasa inawaamuzi zaidi ya 40 wenye beji ya fifa
4. Ameboresha ubora wa mashindano ya kombe la shirikisho kwa kutafuta udhamini na mshindi wa kombe hlo ndio muakilishi wa nchi kombe la shirikisho
5. Serengeti boys wamecheza afcon kwa ubora kabisa
Kuna mengine mengi, leo acha niishie hapa. Tumpe nafasi nyingine ili atekeleze yale machache yaliyobaki. Kama tulivyo binadamu wengine, naye anamapungufu yake. Lakini faraja yangu kubwa ni kuwa, mapungufu yanarekebishika. Ni kumueleza tu kuwa umekosea hapa na pale...