1. Mimi nimekuambia hakuna sheria inayoruhusu haya yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan hata kama Rais ni custodian wa ardhi yote. Kuwa custodian wa mali ya mtu, haina maana kuwa unaruhusiwa kufanya lolote na wakati wowote juu ya mali hiyo.
Lakini wewe
kavulata ndiye unayesema kuwa anafanya uharamia huo kwa mujibu wa sheria..!!
Sasa thibitishia jukwaa hili anatumia sheria ipi, ibara gani kuwafanyia wamasai wa Ngorongoro, Loliondo na jamii za wanavijiji wa maeneo mengi Tanganyika?
2. Unazumngumzia ya Hayati Julius K. Nyerere na vijiji vya ujamaa mwaka 1974 - 1975.
Kwa hili iko hivi:
➡Kwanza narudia hoja yangu niliyokuambia hapo awali, kwamba, huna taarifa za kutosha kwa kuwa hujasoma historia vizuri. Ukiwa huna information za kutosha utapotoka na utapotosha wengine pia. Ni wewe
kavulata..
➡Ya Julius K. Nyerere na vijiji vya ujamaa ni irrelevant kabisa na kinachofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan..
➡Program ya vijiji vya ujamaa ilikuwa ni kuwapanga watu waishi ktk mpangilio ili kuiwezesha serikali kuwahudumia vyema kama jukumu lako. Iliendeshwa kwa uwazi (japo kwa lazima) na sababu zilikuwa wazi kabisa na leo matunda yake yanaonekana japo Nyerere baada ya miaka kadhaa anakiri kuwa, sera yake hiyo ilikuwa ngumu na mbovu. Pamoja na hili, ktk utekelezaji wake hakuna mtu au kabila ambalo lilikuwa re - allocated kutoka ktk ardhi ya asili yake..!
➡Vijiji vya ujamaa vilikuwa havihamishi kabila au jamii fulani kutoka wilaya au mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. Kama unabisha na una mfano hata mmoja kupinga hoja hii, utoe na nitakuelewa..
➡Rais Samia anachokifanya ni EVICTION BY FORCE. Yaani kuwanyang'anya wananchi ardhi yao kwa kisingizio cha uwekezaji ukweli ukiwa ni viongozi hawahawa wakishirikiana na mabeberu kupora ardhi za watu kwa sura ya uwekezaji. Hizi ni sera za wakoloni na kikoloni 100%