Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.Kuna wakati watanzania wa kawaida wanashindwa kuchagua kipi Bora kati ya Sheria kwa upande mmoja na amani na utulivu kwa upande wa pili. Mh. Mwabukusi, Rais mteule wa TLS anahubiri Sheria Sheria Sheria Sheria mwanzo mwisho kwenye taifa ambalo watu wake wanajiona kuwa wako huru, Wana amani na utulivu. Mwabukusi anataka kuwaambia watanzania kuwa hapanaaa, hamko huru, hamna amani na hamna utulivu twendeni tukatafute amani na utulivu kupitia TLS.
Kwa maoni yangu mm amani na utulivu wetu hautokani na Sheria peke yake, bali ni pamoja na utamaduni, mazoea, uvumilivu, woga, sera, hulka ya watanzania na sheria.
Twendeni polepole na hiki kilichopo ambacho kinatuhakikishia kuimaliza Leo yetu na kutufikisha kesho na keshokuta kuliko watu wa Congo, Sudan, Somalia au Palestine na Israel. Present is known and secure.
Watu wetu Bado ni maskini sana kiuchumi na kielimu, hakuna sheria na demokrasia inayoweza kufua dafu 100% katikati ya watu maskini, wajinga na wenye njaa. Lazima tuinue elimu yao na kuondoa njaa zao kwanza kabla ya kuwaletea demokrasia na Sheria. (Abram Maslow's)
WATANZANIA THEIR FIRST PRIORITY NIYOIONA KWAO NI UHAI.Tundu Lissu kanusurika kufa lakini hakuna mwananchi aliyeandamana kupinga kitendo hicho cha kinyama. Hii inaonuesha kuwa wananchi wanazo shida zao nyingine kabisa na zile anazosema lisu na wenzake. Mbowe alikuwa mahabusu kwa zaidi ya miezi 6 hivi, lakini hakuna mwananchi aliyemwagika barabarani kupinga kitendo hicho. Hii ni kionuesha kuwa kile anachotetea sio kile kinachowasokota wananchi.
HApa tanzania sheria tulizonazo ni za muda mrefu sana na inadaiwa zinawauruza masikini.Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
Nafikiri hujaelewa nilichoandika, napinga sheria hizo.HApa tanzania sheria tulizonazo ni za muda mrefu sana na inadaiwa zinawauruza masikini.
Sasa je mbona shsria hizi zinazodaiwa kuwaburuza masikini zipo muda mrefu na wewe inasema sheria za kuburuza masikini huweka utulivu kwa muda(mfupi)tu ?
AU unataka kukubi kwamba sheria ikiburuza masikini kwa muda mrefu basi haiwi sheria mbaya kwani sheria mbaya hudumu kwa muda mfupi tu kama ya tanzania inavyodaiwa ?
Fafanua ili nieweUkombozi wa wananchi walio wengi upo kwenye baadhi ya maandishi na maneno na siyo kwenye utendaji.
Huwezi kumpa haki mtu mjinga, mvivu, mzururaji mwenye njaa asiyelipa kodi. Kule China, Urusi haki ya kwanza anayohakikishiwa mtu ni uhai na usalama wake tu baaasi, mengine lazima ufanyekazi halali na uonekane ukifanyakazi. Wazungu hawakufikia pale walipo kwa kupeana haki. Waliswagana kufanyakazi kwa masaa mengi bila kujali jinsia na umri hadi wakapata mitaji unayoiona sasa. Nchi zao zimejengwa na watumwa, uporaji na ujira mdogo. Na uporaji huo unaendelea mpaka sasa. Mfano, pale Marekani baada ya kutangaza "haki" wafanyabiashara karibu wote wamehamisha viwanda vyao kwenda Asia na Afrika ili wakapate cheap labors kwenye uzalishaji na kurudisha bidhaa Marekani. Wanaendelea kupora kwa njia nyingine. Kama Rais Magufuli asingwe waswaga watumishi wa umma kuhamia Dodoma kwa nguvu hadi apate fedha za kuwalipa watumishi na kujenga majengo ya wizara zote mpaka leo hii Makao Makao Makuu yasingehamia Dodoma.Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
Shida kubwa watanzania wengi wanavyo vitu vya kupoteza ambavyo hawakubali kuviacha kiboyaboya wakifa au kuwa wakimbizi. Watanzania wengi wana ardhi, makazi, familia, mifugo, bodaboda, gari, baiskeli, biashara ama kazi ya kuajiliwa. Nchi nyingi zinazokubwa na machafuko zina watu wengi sana wasiokuwa na cha kupoteza (property less). Hivyo watanzania wengi wanaiona na kuihitaji kesho yao. Kama mtamminya sana machinga kesho atapanda gari kurudi kwao Nanjilinji kufuga bata. Hii ni tofauti na nchi nyingine ambazo hawna alternatives. Lakini hata sisi hapa kama siku altenavives zitakwisha kwa watanzania (yaani ardhi imekwisha yoote, pa kuegesha bodaboda, kupanga viazi chini pakiisha ndiyo watakusikiliza.WATANZANIA THEIR FIRST PRIORITY NIYOIONA KWAO NI UHAI.
Mtanzania yuko radhi alale njaa ila ana uhai basi anavumilia tu.
Ndio maana mtanzania saidia fundi ukimhambia hapa kuna kibarua cha alfu 10 na kule kuna maandamano basi ataenda kwenye kibarua,
why ? Kwa sababu kwenye kibarua kuna uhakika wa uhai ila kwenye maandamano kuna uhakika wa maumivu ya kuhatarisha uhai.
Elimu ndio silaha yenye kuweza kutukomboa. Haya malalamiko kila mahali ambapo mtanzania anaweza kupatumia kulalamikia hayana msaada wowote ule.Kuna wakati watanzania wa kawaida wanashindwa kuchagua kipi Bora kati ya Sheria kwa upande mmoja na amani na utulivu kwa upande wa pili. Mh. Mwabukusi, Rais mteule wa TLS anahubiri Sheria Sheria Sheria Sheria mwanzo mwisho kwenye taifa ambalo watu wake wanajiona kuwa wako huru, Wana amani na utulivu. Mwabukusi anataka kuwaambia watanzania kuwa hapanaaa, hamko huru, hamna amani na hamna utulivu twendeni tukatafute amani na utulivu kupitia TLS.
Kwa maoni yangu mm amani na utulivu wetu hautokani na Sheria peke yake, bali ni pamoja na utamaduni, mazoea, uvumilivu, woga, sera, hulka ya watanzania na sheria.
Twendeni polepole na hiki kilichopo ambacho kinatuhakikishia kuimaliza Leo yetu na kutufikisha kesho na keshokuta kuliko watu wa Congo, Sudan, Somalia au Palestine na Israel. Present is known and secure.
Watu wetu Bado ni maskini sana kiuchumi na kielimu, hakuna sheria na demokrasia inayoweza kufua dafu 100% katikati ya watu maskini, wajinga na wenye njaa. Lazima tuinue elimu yao na kuondoa njaa zao kwanza kabla ya kuwaletea demokrasia na Sheria. (Abram Maslow's)
sheria na haki sio kila kitu. Kumlazimisha mtoto amke asubuhi kwenda shule hata kama yeye hataki sio kudhurumu haki yake mtoto? Je, mzazi amuache alale kama yeye mwenye hataki shule?. Usitumie sheria kama kichaka cha kisiasa.Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
Haki ni zaidi ya kuishi.Haki kubwa kuliko zote ni haki ya kuishi. Tanzania haki hiyo ipo kubwa sana. Nchi kubwa kama China yenye watu robo ya Dunia huwezi kuiendesha kwa demokrasia. Mtawala wao anawajibika kuwapa watu wake haki ya kuishi, kula, kuvaa na kulala. Nchi kama DRC, Kenya, Rwanda, Sudan, Ethiopia, somalia, south Africa na hata Uganda na Rwanda wanatamani hali yetu hiihii na hivihivi tulivyo Leo, Mwabukusi anaweza kutamani kuwaletea watu kiasi kikubwa cha demokrasia ya kufikirika TU ambayo haipo duniani kote. Wale wenzangu tulioishi nchi za magharibi tunajua kuwa hata huko hakuna demokrasia pana mno kwenye mambo serious ya nchi. Vijana wengi hasa wanaume wamejaa magerezani, akina Snowden wanasakwa wauawe.
Tusichague Sheria na demokrasia dhidi ya amani na utulivu.
Wanasheria ni "kundi la wasomi" ambalo linapaswa kutukwamua sisi na wanasiasa wetu wa Afrika kwa kutuambia ukweli tunakwama wapi kufanya maendelea. Ni mikataba ipi, sheria zipi na tabia zipi za nchi na nje ya nchi zinatufanya tuwe masikini na namna ya kuondokana nayo. Watuambie kwanini bidhaa zetu zinakosa masoko kimataifa,Katika kada ambazo hazina manufas kijamii,moja wapo ni sheria.