Uchaguzi TLS ulikuwa kati ya Sheria na utulivu wa nchi

Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
 
WATANZANIA THEIR FIRST PRIORITY NIYOIONA KWAO NI UHAI.

Mtanzania yuko radhi alale njaa ila ana uhai basi anavumilia tu.

Ndio maana mtanzania saidia fundi ukimhambia hapa kuna kibarua cha alfu 10 na kule kuna maandamano basi ataenda kwenye kibarua,
why ? Kwa sababu kwenye kibarua kuna uhakika wa uhai ila kwenye maandamano kuna uhakika wa maumivu ya kuhatarisha uhai.
 
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
HApa tanzania sheria tulizonazo ni za muda mrefu sana na inadaiwa zinawauruza masikini.

Sasa je mbona shsria hizi zinazodaiwa kuwaburuza masikini zipo muda mrefu na wewe inasema sheria za kuburuza masikini huweka utulivu kwa muda(mfupi)tu ?

AU unataka kukubi kwamba sheria ikiburuza masikini kwa muda mrefu basi haiwi sheria mbaya kwani sheria mbaya hudumu kwa muda mfupi tu kama ya tanzania inavyodaiwa ?
 
Nafikiri hujaelewa nilichoandika, napinga sheria hizo.
Changamoto ni kwamba, watunga sheria ikianzia kwa draftsman, wamekariri na wana fikra za kikoloni za kumdhalilisha, kumtesa na mwafrika masikini. Wamekariri na kufuata sera za kikoloni practically kwa asilimia kubwa. Ukombozi wa wananchi walio wengi upo kwenye baadhi ya maandishi na maneno na siyo kwenye utendaji.
 
Wagombea Uraisi wa TLS uchaguzi umemalizika,tuvunje makundi jengeni taasisi yenu Hakuna haja ya kugombea fito wakati mnajenga nyumba moja.
 
Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
Huwezi kumpa haki mtu mjinga, mvivu, mzururaji mwenye njaa asiyelipa kodi. Kule China, Urusi haki ya kwanza anayohakikishiwa mtu ni uhai na usalama wake tu baaasi, mengine lazima ufanyekazi halali na uonekane ukifanyakazi. Wazungu hawakufikia pale walipo kwa kupeana haki. Waliswagana kufanyakazi kwa masaa mengi bila kujali jinsia na umri hadi wakapata mitaji unayoiona sasa. Nchi zao zimejengwa na watumwa, uporaji na ujira mdogo. Na uporaji huo unaendelea mpaka sasa. Mfano, pale Marekani baada ya kutangaza "haki" wafanyabiashara karibu wote wamehamisha viwanda vyao kwenda Asia na Afrika ili wakapate cheap labors kwenye uzalishaji na kurudisha bidhaa Marekani. Wanaendelea kupora kwa njia nyingine. Kama Rais Magufuli asingwe waswaga watumishi wa umma kuhamia Dodoma kwa nguvu hadi apate fedha za kuwalipa watumishi na kujenga majengo ya wizara zote mpaka leo hii Makao Makao Makuu yasingehamia Dodoma.

Nchi zetu hizi ziko kwenye hatua ya kuswagana bado badala ya kuwasikiliza wakoloni wetu wanachotaka na kusema, ni waongo wametudanganya. Wacha mama Samia awashwage watanzania kwanza ili tupate barabara, reli, maji, umeme, elimu na matibabu ya uhakika kwanza. Nitakubaliana na wanasheria (TLS) kama watasaidia kwenye kuwaswaga watu na vijana wote wanaopiga bao na pool na kunywa pombe mchana siku za kazi na kuwafunga watu wote bila kujali cheo anaekula fedha za wananchi. Yaani watu wooote tufanyekazi kwanza na tulipe kodi zetu wooooooote hata yule anaeuza mchicha gengeni au kupaka wanawake rangi ya kucha, kisha ndio tudai haki zetu na kuwaadabisha wanaotuibia na kuibia wengine.
 
Shida kubwa watanzania wengi wanavyo vitu vya kupoteza ambavyo hawakubali kuviacha kiboyaboya wakifa au kuwa wakimbizi. Watanzania wengi wana ardhi, makazi, familia, mifugo, bodaboda, gari, baiskeli, biashara ama kazi ya kuajiliwa. Nchi nyingi zinazokubwa na machafuko zina watu wengi sana wasiokuwa na cha kupoteza (property less). Hivyo watanzania wengi wanaiona na kuihitaji kesho yao. Kama mtamminya sana machinga kesho atapanda gari kurudi kwao Nanjilinji kufuga bata. Hii ni tofauti na nchi nyingine ambazo hawna alternatives. Lakini hata sisi hapa kama siku altenavives zitakwisha kwa watanzania (yaani ardhi imekwisha yoote, pa kuegesha bodaboda, kupanga viazi chini pakiisha ndiyo watakusikiliza.
 
Elimu ndio silaha yenye kuweza kutukomboa. Haya malalamiko kila mahali ambapo mtanzania anaweza kupatumia kulalamikia hayana msaada wowote ule.
 
Sheria zinazotoa haki zikifuatwa husababisha Amani na utulivu wa kudumu.
Kuwaburuza masikini, wajinga na wenye njaa huweka utulivu wa muda tu.
sheria na haki sio kila kitu. Kumlazimisha mtoto amke asubuhi kwenda shule hata kama yeye hataki sio kudhurumu haki yake mtoto? Je, mzazi amuache alale kama yeye mwenye hataki shule?. Usitumie sheria kama kichaka cha kisiasa.
 
Naimani Sasa walengwa mmeanza kuhaha.
Na vp hao wananchi wamesema wapi hayo unayojaribu kupigia Ramli.
Subiri awapime SUTI mbuzi nyie,msiopenda kutenda haki.

Mmefikiwa.
#Mwambukusi4life.
 
Haki ni zaidi ya kuishi.
 
Katika kada ambazo hazina manufas kijamii,moja wapo ni sheria.
Wanasheria ni "kundi la wasomi" ambalo linapaswa kutukwamua sisi na wanasiasa wetu wa Afrika kwa kutuambia ukweli tunakwama wapi kufanya maendelea. Ni mikataba ipi, sheria zipi na tabia zipi za nchi na nje ya nchi zinatufanya tuwe masikini na namna ya kuondokana nayo. Watuambie kwanini bidhaa zetu zinakosa masoko kimataifa,
 
Chadema wamewekwa ndani lakini wanachama wako doro. Viongozi wanafanya kazi waliotumwa na wanachama wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…