Uchaguzi Urais, USA - 2020: Anavyopigwa Donald Trump (R) katika Ballot Box, ndivyo ambavyo alikuwa anapigwa John P. Magufuli (CCM)..

Uchaguzi Urais, USA - 2020: Anavyopigwa Donald Trump (R) katika Ballot Box, ndivyo ambavyo alikuwa anapigwa John P. Magufuli (CCM)..

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Mfanano wa chaguzi hizi mbili:
1. Wote, Donald Trump (Republican) na John Magufuli (CCM) ni incumbent presidents waliokuwa wanatetea nafasi zao..

2. Wote ni maRais wasema ovyo na wasiopenda kulaumiwa kwa makosa yao..

3. Wote ni wapenda sifa na wakati mwingine kutaka sana kupenda "kuabudiwa"..

4. Wote ni wapenda kusema uongo na kulazimisha watu waamini uongo wao...

Utofauti wao;
1. Rais Donald Trump anatawala chini ya mamlaka na taasisi zenye uhuru mkubwa wa kumdhibiti, hafurukuti hawezi kuzitumia kumpendelea. Magufuli Pombe, ndiye anayezitawala, kuzielekeza cha kufanya mamlaka na taasisi za udhibiti kama polisi, NEC nk. Anazilamisha kumpendelea yeye na kuwakandamiza wapinzani wake..

2. Rais Trump ndiye anahaha kutafuta haki mahakamani kwa kudhani kuwa kuna wizi wa kura dhidi yake. Kwa Magufuli, hilo halipo, halikuwepo.!!

Nini Kinaendelea sasa?
1. Rais Trump Donald anaelekea kupoteza Mamlaka ya Urais wake. Mpaka sasa mpinzani wake Joe Biden (D) anaongoza kwa kura (Electoral College) 264 huku counting ya kura kwenye baadhi ya majimbo ukiendelea, Joe Biden akiwa anaongoza ktk kura hizo zinazoendelea kuhesabiwa sasa..

2. Donald Trump haamini kinachoendelea. Haamini kuwa pamoja na "maendeleo ya vitu" aliyowaletea wamarekani, cha ajabu wanamkataa kwenye sanduku la kura. Hajui amewakosea nini...!!

Kwa nini hapa Tanzania, Magufuli (CCM) tumeambiwa "ameshinda?"
1. Kwa hakika, kama uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 ungefanyika ktk mazingira ya uwazi kama USA, Magufuli asingeshinda na angepigwa kama ambavyo mwenzake Trump ananyongwa mchana kweupe..!

2. Tanzania na Magufuli wa CCM ili kujipatia ushindi "wenye mashaka" makubwa, ilibidi afungulie "giza totoro" ili kuruhusu mifumo yake ya "kumshindisha" ifanye kazi..

3. Kufungwa kwa mtandao wa internet; kuzuia zaidi ya mawakala 57,000 wa vyama pinzani katika vituo vya kupigia zaidi ya 80,000 kuwakilisha wagombea wao ktk vituo vya kupigia kura; kukamata baadhi ya wagombea wa vyama pinzani na kuwaweka ndani (selo za polisi) kabla na siku ya uchaguzi yenyewe nk nk ni miongoni mwa mikakati ya kumpa ushindi "fake" Magufuli na CCM kwa ujumla...!
................................................

US - Updates Presidential Election results as at 21:00EAT
Screenshot_20201107-214343.png

Georgia State with 16 Electoral Colleges votes is under "votes recounting"..

Obviously, Joe Biden (D) atashinda...
 
Tushauri sasa tufanyeje? Na walioshindwa huku waende mahakamani au waandamane?
 
..Donald Trump ni Amiri Jeshi dhaifu na bwege sijapata kuona.

..Inawezekana vipi Joe Biden afanye kampeni muda wote na hatujasikia hata mara moja amepigwa mabomu ya machozi, au kuswekwa mahabusu?

..Amiri Jeshi Mkuu gani asiyeweza kutumia DOLA kubaki madarakani?
 
Hayo yote ulosema si ya kweli na hawa watu wawili hawafanani hata kidogo.

Donald Trump anashindwa kutetea kiti chake cha uraisi kwa sababu mbili kubwa.

1. Ameigawa Marekani na kuifanya iwe na watu wenye chuki baina ya wao kwa wao.

Hiyo ni kwa kutoa kauliza mara kwa mara za kuwaunga mkono wazungu wenye msimamo mkali wa KKK.

2. Amezembea katika kuchukua hatua kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeua raia 235,000 wengi wao wakiwa wadengereko wenzetu.

Hawa ni wale walokuwa wakiokotwa mabarabarani na kuzikwa kama mizoga ya wanyama.

Wakati mwingine tukitoa maoni yetu tuondoe hisia kali tuegemee zaidi uhalisia.
 
Kule jeshi ni independent, halihusiani na siasa. Kazi yao ni kulinda raia na maslahi ya America.
 
..Donald Trump ni Amiri Jeshi dhaifu na bwege sijapata kuona.

..Inawezekana vipi Joe Biden afanye kampeni muda wote na hatujasikia hata mara moja amepigwa mabomu ya machozi, au kuswekwa mahabusu?

..Amiri Jeshi Mkuu gani asiyeweza kutumia DOLA kubaki madarakani?
Kwa jicho la tatu nimekuelewa mkuu.
 
Hayo yote ulosema si ya kweli na hawa watu wawili hawafanani hata kidogo.

Donald Trump anashindwa kutetea kiti chake cha uraisi kwa sababu mbili kubwa.

1. Ameigawa Marekani na kuifanya iwe na watu wenye chuki baina ya wao kwa wao.

Hiyo ni kwa kutoa kauliza mara kwa mara za kuwaunga mkono wazungu wenye msimamo mkali wa KKK.

2. Amezembea katika kuchukua hatua kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeua raia 235,000 wengi wao wakiwa wadengereko wenzetu.

Hawa ni wale walokuwa wakiokotwa mabarabarani na kuzikwa kama mizoga ya wanyama.

Wakati mwingine tukitoa maoni yetu tuondoe hisia kali tuegemee zaidi uhalisia.
Hujielewi kabisa, hiyo sababu ya kwanza pekee ndio inamfunga kabisa huyo "role model" wako.

Hukuwahi kumsikia anavyoropoka akiwa Mwanza; "hawa walinichagua msiwafukuze barabarani" au "hawa walinichagua msiwavunjie nyumba zao" hata kama wamejenga kwenye hifadhi ya uwanja wa ndege.

Hiyo Corona nayo mmeamua tu kujitoa akili, huku kwetu haikuwa na madhara makubwa kama ilivyokuwa kwa nchi za wazungu, tuliishia kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa mask, unadhani wazungu hawakujua kutumia njia hizo? na kama mlikuwa mnaziamini hizo njia kwanini mkakimbilia Chato zaidi ya mwezi mzima!
 
Back
Top Bottom