mama kubwa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 6,230
- 9,889
Kama una ushahidi na uyasemayo na ikathibitika mahakamani basi peleka madai yako huko.
Vinginevyo unamkashifu kiongozi alieapishwa rasmi kuwa raisi wa JMT.
Tena hili litaleta uwajibikaji WA kweli sio unawadanganya Wananchi WA Songwe kuwa huwaletei Maji Kwa kuwa wamechagua mpinzani wakati Kongwa kuna mbunge WA maisha WA CCM na wanakunywa matope.Defenetely, YES..
Lakini katiba mpya pekee haitoshi..
Dhamira safi ya MIOYO na NAFSI maarufu kama "UTASHI CHANYA WA KISIASA" are the added qualities kwa ajili ya ustawi wa jamii yetu...
Mbona nimeeleza hayo mambo mawili hapo juu?Nimeandika kwa muono wangu..
Wewe vipi, unasemaje? Kama hafanani naye, basi eleza anatofautiana naye kwa mambo gani?
Mbona nimeeleza hayo mambo mawili hapo juu?
Huo uhuru unaouzungumzia ndio huu huu wa kufungia mitandao ya kijamii.?kijana umepewa uhuru wa kutoa maoni katu usiutumie vibaya kwa kumsema vibaya Rais wetu. Kama humpendi hama nchi nendaa nchi zingine hukoo
Kijana usimfananishe Mungu na kiumbe dhaifu kama Magufuli.Mtoa mada MAGUFULI sio wa kushindwa na mtu mropokaji kama Tundu lissu ,hata MUNGU angekuja kusimamia uchaguz wa Tanzania bado MAGUFULI angeshinda kwa aslmia kwanzia 80,,,
Dhuluma ilianza leo ,Kila Chaguzi wanaibiwaga wao tu.Inakufundisha uwe na akili ya kuikataa dhuluma..
Kula like 1000Hayo yote ulosema si ya kweli na hawa watu wawili hawafanani hata kidogo.
Donald Trump anashindwa kutetea kiti chake cha uraisi kwa sababu mbili kubwa.
1. Ameigawa Marekani na kuifanya iwe na watu wenye chuki baina ya wao kwa wao.
Hiyo ni kwa kutoa kauliza mara kwa mara za kuwaunga mkono wazungu wenye msimamo mkali wa KKK.
2. Amezembea katika kuchukua hatua kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeua raia 235,000 wengi wao wakiwa wadengereko wenzetu.
Hawa ni wale walokuwa wakiokotwa mabarabarani na kuzikwa kama mizoga ya wanyama.
Wakati mwingine tukitoa maoni yetu tuondoe hisia kali tuegemee zaidi uhalisia.
Trump amebanduliwa😂😂[emoji1787][emoji1787][emoji1787]View attachment 1621520View attachment 1621521View attachment 1621522View attachment 1621523
Tokaa zako hujielewiHujielewi kabisa, hiyo sababu ya kwanza pekee ndio inamfunga kabisa huyo "role model" wako.
Hukuwahi kumsikia anavyoropoka akiwa Mwanza; "hawa walinichagua msiwafukuze barabarani" au "hawa walinichagua msiwavunjie nyumba zao" hata kama wamejenga kwenye hifadhi ya uwanja wa ndege.
Hiyo Corona nayo mmeamua tu kujitoa akili, huku kwetu haikuwa na madhara makubwa kama ilivyokuwa kwa nchi za wazungu, tuliishia kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa mask, unadhani wazungu hawakujua kutumia njia hizo? na kama mlikuwa mnaziamini hizo njia kwanini mkakimbilia Chato zaidi ya mwezi mzima!
Suluhu la haya yote ni katiba mpya
Tujenge nchi uchaguzi umeishaKijana usimfananishe Mungu na kiumbe dhaifu kama Magufuli.
Japo ni uhuru wako wa maoni, nami natumia uhuru wangu kukukosoa.
Mkuu, umesahau kutoa SULUHISHO. Nini kifanyike sasa, baada ya UDHALIMU kutamalaki nchini?Mfanano wa chaguzi hizi mbili:
1. Wote, Donald Trump (Republican) na John Magufuli (CCM) ni incumbent presidents waliokuwa wanatetea nafasi zao..
2. Wote ni maRais wasema ovyo na wasiopenda kulaumiwa kwa makosa yao..
3. Wote ni wapenda sifa na wakati mwingine kutaka sana kupenda "kuabudiwa"..
4. Wote ni wapenda kusema uongo na kulazimisha watu waamini uongo wao...
Utofauti wao;
1. Rais Donald Trump anatawala chini ya mamlaka na taasisi zenye uhuru mkubwa wa kumdhibiti, hafurukuti hawezi kuzitumia kumpendelea. Magufuli Pombe, ndiye anayezitawala, kuzielekeza cha kufanya mamlaka na taasisi za udhibiti kama polisi, NEC nk. Anazilamisha kumpendelea yeye na kuwakandamiza wapinzani wake..
2. Rais Trump ndiye anahaha kutafuta haki mahakamani kwa kudhani kuwa kuna wizi wa kura dhidi yake. Kwa Magufuli, hilo halipo, halikuwepo.!!
Nini Kinaendelea sasa?
1. Rais Trump Donald anaelekea kupoteza Mamlaka ya Urais wake. Mpaka sasa mpinzani wake Joe Biden (D) anaongoza kwa kura (Electoral College) 264 huku counting ya kura kwenye baadhi ya majimbo ukiendelea, Joe Biden akiwa anaongoza ktk kura hizo zinazoendelea kuhesabiwa sasa..
2. Donald Trump haamini kinachoendelea. Haamini kuwa pamoja na "maendeleo ya vitu" aliyowaletea wamarekani, cha ajabu wanamkataa kwenye sanduku la kura. Hajui amewakosea nini...!!
Kwa nini hapa Tanzania, Magufuli (CCM) tumeambiwa "ameshinda?"
1. Kwa hakika, kama uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 ungefanyika ktk mazingira ya uwazi kama USA, Magufuli asingeshinda na angepigwa kama ambavyo mwenzake Trump ananyongwa mchana kweupe..!
2. Tanzania na Magufuli wa CCM ili kujipatia ushindi "wenye mashaka" makubwa, ilibidi afungulie "giza totoro" ili kuruhusu mifumo yake ya "kumshindisha" ifanye kazi..
3. Kufungwa kwa mtandao wa internet; kuzuia zaidi ya mawakala 57,000 wa vyama pinzani katika vituo vya kupigia zaidi ya 80,000 kuwakilisha wagombea wao ktk vituo vya kupigia kura; kukamata baadhi ya wagombea wa vyama pinzani na kuwaweka ndani (selo za polisi) kabla na siku ya uchaguzi yenyewe nk nk ni miongoni mwa mikakati ya kumpa ushindi "fake" Magufuli na CCM kwa ujumla...!
................................................
US - Updates Presidential Election results as at 21:00EAT
View attachment 1621656
Georgia State with 16 Electoral Colleges votes is under "votes recounting"..
Obviously, Joe Biden (D) atashinda...
kwani IGP wa kule ni Sirro ?
Hahahaaa...labda tumuulize Nyani Ngabu, "IGP Sirro" wa Marekani ni nani?
..imekuwaje akamuacha Amiri Jeshi Mkuu akapigwa mueleka kwenye uchaguzi mkuu?
Hahahaaa.
Umenikumbusha kuna siku moja hivi wakati wa yale maandamano ya Marekani.
Kuna mtu nilikuwa nabishana naye humu kuhusu madaraka ya Rais wa Marekani.
Yeye huyo jamaa eti akasema kwamba Rais wa Marekani ndiye Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
Note: majeshi ya ulinzi na usalama.
Wewe sasa unafanya kufuru!Mtoa mada MAGUFULI sio wa kushindwa na mtu mropokaji kama Tundu lissu ,hata MUNGU angekuja kusimamia uchaguz wa Tanzania bado MAGUFULI angeshinda kwa aslmia kwanzia 80,,,
Hahahaaa...hata mimi ningekubishia.
..hivi si wanasema Raisi wa Marekani kila anapokwenda anatembea na kisanduku kina code za kufyatua makombora ya nuclear?
..sasa ina maana Trump anaweza kufyatua makombora ya Nuclear lakini mabomu ya machozi kusambaratisha wahuni wanaoiba kura hawezi kuamrisha?
..labda ndio maana Maraisi wa Marekani wanamalizia hasira zao kwa kina Gaddafi na Saddam Hussein, kwasababu ndani ya Marekani wanavutwa masikio.