Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi ni ndugu na rafiki wa karibu wa Dr. Mwigulu. Huyu bwana hujinasibu alimaliza kidato cha nne. Lakini ukweli ukweli hatakiwi kujisema hivyo kwa kuwa alikuwa darasani na kakangu mimi na aliambulia Daraja la Sifuri - kitu ambacho huwa hakisemi kabisa.
Dr. Mwigulu alimtumia huyu kuiba kura na wakajisahau hadi kura za JPM akaziiba nyingi kuliko hata idadi ya waliopiga kura. Ajabu sana! Huyu bwana hakutakiwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri yetu kwa sababu kwanza huwa hawezi hata kuwasilisha hoja vizuri, hana weledi wa kusimamia vikao vya madiwani wetu na hata uwezo wa kujibu baadhi ya hoja hana kabisa. Walifanya vigisu na Mwigulu wake wakaengua wagombea wote wazuri ambao pengine wangetokea watu wazuri wa kuongoza Halmshauri yetu. Mwigulu kaweka Timu yake pale akifikiri kuwa 2025 atapenya kirahisi. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ambaye pia anatokea nyumbani kwao Mwigulu tayari ameshachokwa - huyu bwana Samweli ndiyo alikuwa kinara wa wizi wa kura 2020. Alishiriki moja kwa moja kutengeneza kura za Mwendazake na kupanga timu ya madiwani wafuata upepo.
Madiwani wa Viti Maalumu karibia wote amewaweka yeye na Mwigulu kuanzia yule Dayana Masangya, Esther Yonah, nk.
Kwa kweli kwa hali ilivyo kwa sasa Iramba haina uongozi makini wa kisiasa kwa sababu ni uongozi uliowekwa na Dr. Mwigulu kwa ajili ya kuutumia kama daraja la kuvukia ili kutimiza ndoto zake. Hakuna uwezekano wowote kama Iramba itasonga mbele sasa.
Rai yangu ni kumsihi Dr. Mwigulu kutubu na kujutia wizi alioufanya wakati wa Uchaguzi wa Mwaka 2020 - amepata nafasi aitumie vizuri na kuwaletea maendelea WanaIramba na isiwe ubabaishaji kama ambavyo hawa madiwani wameanza kuonesha. Mwigulu anaenda kuongoza miaka 15 kama Mbunge lakini kwa jimbo letu hamna lolote la maana ambalo kalifanya ambalo linampa uhalali wa kuendelea kuongoza jimbo hili. Ameshachokwa na ndiyo maana mbinu imekuwa ni kuiba kura tu. Mwaka 2025 hatukubali ijirudie labda atumie uchawi!