Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Si vibaya, mwanzo mwanzoni, kuweka wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ndani na nje ya Tanzania. Lakini, ni mfuatiliaji mkubwa wa siasa za dunia nzima, nikianza na za kwetu hapa Tanzania. Pia, ni mfuasi wa hoja na mkosoaji wa maigizo na vihoja vya kisiasa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakaribia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa. Katika nafasi mbili za juu kabisa-Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti panaonekana patakuwa na mchuano mkali. kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni mchuno kati ya Ndugu Freeman A. Mbowe na Wakili Msomi Tundu A.M. Lissu.
Kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ushindani mkubwa utakuwa kati ya Ezekiel Wenje na John Heche. Wote hawa wamewahi kuwa Wabunge na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Tena, wote ni wa kanda ya Ziwa-Mwanza na Mara. Faida aliyonayo Heche ni kukua na kukuzwa ndani ya CHADEMA. Alianzia BAVICHA na kuwa Mwenyekiti huko.
Ndani ya CHADEMA, kuna wanachama na viongozi mbalimbali wanaendelea kujitokeza kumuunga mkono Mbowe au Lissu kwenye nafasi ya Mwenyekiti. Kuunga mkono au kutokuunga mkono ni haki ya kikatiba, kikanuni na kiutamaduni-haki ya kuwa na maoni huru. Lakini, mgombea kumuunga mkno mgombea mwingine tena kwa nafasi tofauti inatafakarisha.
Kitendo cha Heche, anayegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, kumuunga mgombea wa Uenyekiti Tundu Lissu ni 'kujichora' kama 'mgombea mwenza' wa Lissu. Nini kitatokea kama Lissu atashinda na yeye kushindwa? Ataungana na Wenje kumsaidia Lissu? Je, yeye akishinda na Lissu akashindwa, atafanya kazi na Mbowe? kwa maoni yangu, haikuwa sawa kwa Heche kujipa nafasi ya mgombea mwenza wa Lissu.
Wagombea wa nafasi hizi kuu ndani ya CHADEMA, hakika, ni heavyweight wa CHADEMA. Kwa kauli zinazoendelea za baadhi ya wagombea kuhusu mchakato wa uchaguzi na matokeo yake, ni wazi kuwa mpasuko ndani ya CHADEMA hautaepukika. Utakuwa dhahiri au wa sirini. CHADEMA haitabaki kama ilivyo sasa!