Uchaguzi wa Kenya: Kilichokataliwa kilikuwa bora zaidi kuliko kilichotarajiwa kuwa bora

Uchaguzi wa Kenya: Kilichokataliwa kilikuwa bora zaidi kuliko kilichotarajiwa kuwa bora

Kilichofanyika leo ni bora uchaguzi na si uchaguzi bora kama ilivyokuwa ikitazamiwa na wengi.
Leo ulikuwa ni uchaguzi wa bora liende.
@ mwaswast
Kinachonishangaza ni hesabu ya waliopiga kura. Bwana Chebukati anasema ni 48% na idadi yao ni 6.5 millioni. Ila waliojiandikisha ni 19 millioni. Hebu tujiulize, hivi 6.5 millioni ni 48% ya 19 millioni? Jibu ni hapana! 6.5 millioni ni 34.2% ya 19 millioni. Yaani huyu Bwana ameanza kupika matokeo asubuhi na mapema

Only a third of Kenyans voted in the repeat presidential election
Low Voter Turnout, Violence Mar Chaotic Kenya Election Rerun
 
Hapa Tz kuna demokrasia gani bora?! Hizi ni akili matope kabisa[emoji35]

demokrasia ya kukopa ndiyo inayotupa shida Afrika. Kenya kwa desturi yao rais hawezi toka nje ya zile kabira za kichifu yaani GEMA.
lkn Tanzania walau kila kabila linaweza kuongoza nchi. makabila yote ni sawa. hamna kabila la watawaliwa au watwana na watawala. nitamkumbuka Nyerere daima.
 
The dead tell no tales.

Keep on waiting a reckon from the dead.
But a matter of fact is "he reported several times to the authorities regarding WASIOJULIKANA who wanted to snitch his breath".
 
Kwa matokeo yaliyotangazwa jana. Pamoja na mazingira jumla ya uchaguzi wa marudio. Nahitisha ya kwamba Kenya walikurupuka kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali. Maana uchaguzi huu wa marudio ulikuwa na kasoro nyingi za wazi, ikiwa ni pamoja na kuwa na hali ya hatari wakati wa kupiga kura (jambo ambalo si la kawaida maana uzoefu unaonesha ya kuwa vurugu hutokea baada ya kutangaza mshindi na si kipindi cha upigaji kura) na pia idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura. Kwa mtazamo wangu:
"Kilichokataliwa kilikuwa bora zaidi kuliko kilichotarajiwa kuwa bora"
 
kilichokataliwa kinaanza kuthibitishwa kwamba kilikuwa bora kuliko kilichotarajiwa kuwa bora.
majaji wameanza kuthibitisha hilo leo.
 
dalili za kujutia kile kilichokataliwa. wanalia kwa nini walikiacha.
 
Rasmi sasa. kumbe mahakama ya juu Kenya ilikuwa haijui inachokifanya. kama iliweza kuvunja matokeo ya uchaguzi wa urais kwa kasoro chache ambazo tunaweza sema ni za kibinadamu na zinaweza kuvumilika kwa maana haziharibu lengo la msingi, na kuvumilia hayo makubwa, nachelea kusema mahakama ya juu ya Kenya chini ya judge Maraga imeonesha mfano mbaya sana. hakuna jema ambalo tutajifunza. wameharibu bure fedha za umma na utulivu wa nchi. wanastahili lawama. kama ni hivyo ilikuwa ni bora sana kuukubali uchaguzi wa mara ya kwanza.
 
Back
Top Bottom