Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
walichochemsha ni nini hasa mbona hakisemwi hapa?

Walichochemsha TD ndio kilichosababisha pia JF moderators kuwekwa kizimbani. Au labda ni coincedence tu kwamba vyombo vya habari sasa baada ya kufanikiwa kumuweka chini EL et al, sasa vinaanza kuikosea sirikali. Makubwa haya, mbona tutanyooka.
 
Mwanakijiji,

Hapa Tanzania Daima wamevunja sheria period... sababu zaweza kuja baadaye...

Kasheshe asante sana kwa uthabiti wa maneno yako. Ninazo sheria zote husika; ninayo sheria ya uchaguzi ya 1985 na mabadiliko yake na sheria ya magazeti ya 1976 (isiyo na mabadiliko). Kwa vile umesema "wamevunja sheria period".. naomba unisaidie ni kipengele gani cha sheria walichovunja ili tukubaliane; kwa sababu kama wamevunja sheria wanatakiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka na kuadhibiwa haya mambo ya kuitana kupeana maonyo na kurudisha fedha kisirisiri siyaungi mkono. Nisaidie basi ni ipi iliyovunjwa?

Sababu zaweza kuja baadaye

you must be thinking I'm nut! yaani mtu avunje sheria, useme kavunja sheria period.. halafu useme "sababu zinakuja baadaye"? Yaani mtu ameshahukumiwa (kwamba kavunja sheria) halafu mnatafuta ushahidi wa kuonesha kuwa kavunja sheria! I'm getting dizzy!
 
MKJJ unajua kwamba gazeti la leo la Tanzania lilikuwa na hadithi ya kusema JK amtosa Lowasa basi limepotea mitaani ? Kama ulikuwa hujui tuulize sisi wa Dar . Gazeti lilikuwa tupu kabisa na ile habari kwa ndani hapakuwa na kitu baadaye nimeingia mitaani kutafuta gazeti jingine nakuta halipatikani kokote .
 
sijakupata..
 
The government yesterday gave a three-day ultimatum to the publisher and editor of a Kiswahili tabloid, `Tanzania Daima`, to apologise or face punishment, for what it described as distorting information and grossly violating laws and code of ethics in its reports on the just-concluded by-elections in Kiteto Constituency, Manyara Region.

In a statement issued by the Tanzania Information Services (Maelezo) in Dar es Salaam, the government said the newspaper printed two editions with the same issue number (1179), on the same day, when reporting the election results, contrary to the Newspaper Act Number 3 of 1976.

In first edition bearing number 1179, printed on February 25, this year, the tabloid reported that Chadema`s parliamentary aspirant was leading by 71.8 per cent, and that the ruling CCM`s candidate scooped votes in one ward only.

According to the government statement, the elections results printed in the same newspaper issue reported that CCM had won Kiteto elections, scooping votes in 13 wards out of 15, as opposition (Chadema) leaders accepted the defeat.

``The newspaper had grossly violated the Newspaper Act of 1976 by printing a special edition without permission or informing the Newspapers Registrar. Tanzania Daima did not present copies of the two editions to the registrar as required by the law,`` said the statement.

On the other hand, the Tanzania Information Services said the tabloid distorted reports on the election results by publishing results without consulting the relevant authorities--National Election Commission (NEC).

Authorities said the newspaper breached code of ethics by printing and circulating information that confused members of the public on the election results, which could fuel civil unrest.

``On top of that, the editor of the newspaper was called by the registrar to clarify on the confusion, but refused to pay heed,`` said the statement.

``We are giving `Tanzania Daima` three days to apologise for distorting information, violating newspaper laws, information code of ethics and disrespecting order of the registrar?otherwise, the newspaper will be punished in accordance with the Act,`` said the statement.

In a quick response yesterday, Tanzania Daima Managing Editor, Absalom Kibanda, refuted claims that they printed two editions on the same day.

He explained that they printed some copies for up-country regions which showed that chadema was leading in seven wards out of 15, as the paper went to press at around 8.00 pm.

``We sent the copies, but continued to monitor the election trend in various wards. At around 11pm we got the election results, and other copies for Dar es Salaam that showed that CCM had won elections by scoping votes in 13 wards out of 15,`` said Kibanda.

``We asked Chadema leaders who accepted that chances to win the election were minimal. These were clearly reported in our reports. In fact, we did not print two editions but we were forced to produce copies for Dar es Salaam and upcountry customers, because of transport problems.``

The editor admitted that they failed to communicate with the registrar on the problem, but insisted that they published only one edition on that day and not two as claimed by Maelezo.

SOURCE: Guardian

Huku ndo kukurupuka kwenyewe.

Wanatafuta kila kisingizio kuwakalia watu.

Kwanza sheria hizi zilizo tungwa wakati wa TANU ndo tunazo zipigia kelele kila siku.

Kwa lugha nyingine Tamko la serikali linatukumbusha kwamba watanzania wote ni lazima tuamke kudai marekebisho makubwa ya katiba.

Hii katiba ni ile aliyo iacha Sir Richard Turnbull, ukiondoa viraka vya hapa na pale.

Kwa lugha nyingine SISIEMU bado wanaenzi sheria za Mkoloni ili kutawala wananchi huru katika nchi huru kwa mtindo ule ule wa Mkoloni.
Ndiyo maana Viongozi wa SISIEMU wakifika miaka 60 kustaafu ni mbinde na wengine wameanza jitihada za kuongeza muda wa kustaafu ufikie miaka 70 kwi kwi kwi kwi kwi!

Si mngefanya 90 kabisa ili mfanye kazi kwa kubwa ndani ya machela???? kwiii kwwiii kwiiii!

Nasikitika kusema Uhuru wa vyombo vya habari uko kitanzani, Serikali ya SISIEMU inatu blackmail kwa sheria za Muflisi zilizo pitwa na wakati ili kuendeleza Ideology za kifisadi.
 
Kila siku ninasema majeshi ya Upinzani yaachane na mambo ya kugombania na kupoteza mafeza kwenye harakati za uchaguzi ,mambo ambayo yamefungwa na sheria za TANU ,hakuna uchaguzi TANZANIA tusidanganyane tukadanganyika ,na hivi viti vya ubunge vichache vinavyopatikana au vinavyotolewa ni kama kumpa mtoto mdogo pipi na ujiti wake.
Kama mnataka ushauri wa bure basi majeshi ya upinzani na nguvu zake zote pamoja na rasilimali waliyokuwa nayo waielekeze katika mambo ya Sheria za Nchi katika wakati huu tulio nao wa utandawazi ,hakuna upinzani utakaofanikiwa kama vita na adui sheria havijadhibitiwa ,hivyo sera za vyama vya upinzani kuhusiana na mikakati na uongozi wa Nchi zisimamishwe na sasa ni wakati wa kubadilisha dira na kuelekeza majeshi katika kugombania mabadiliko ya sheria na KATIBA ya NCHI ili ziendane na wakati na anaesema hakuna sababu ya kubadilisha katiba kwa sasa huyo aisabiwe ni ADUI wa TAIFA la TANZANIA alaniwe vikali sana na ikiwezekana ahukumiwe kifungo cha maisha.
 
Hili suala la kubadili katiba limekuwa linapiganiwa na upinzani kwa miaka mingi sana -kama unakumbuka ule mkutano wa jangwani ambapo kiongozi mmoja alifikia hatua ya kuikanyaga katiba na akajikuta jela.

Tatizo ni kuwa wapinzani wakisema kitu hata kama kina manufaa kwa taifa wanapuuzwa na kudhihakiwa. Kazi kwelikweli Tanzania
 
Kila siku ninasema majeshi ya Upinzani yaachane na mambo ya kugombania na kupoteza mafeza kwenye harakati za uchaguzi ,mambo ambayo yamefungwa na sheria za TANU ,hakuna uchaguzi TANZANIA tusidanganyane tukadanganyika ,na hivi viti vya ubunge vichache vinavyopatikana au vinavyotolewa ni kama kumpa mtoto mdogo pipi na ujiti wake.
Kama mnataka ushauri wa bure basi majeshi ya upinzani na nguvu zake zote pamoja na rasilimali waliyokuwa nayo waielekeze katika mambo ya Sheria za Nchi katika wakati huu tulio nao wa utandawazi ,hakuna upinzani utakaofanikiwa kama vita na adui sheria havijadhibitiwa ,hivyo sera za vyama vya upinzani kuhusiana na mikakati na uongozi wa Nchi zisimamishwe na sasa ni wakati wa kubadilisha dira na kuelekeza majeshi katika kugombania mabadiliko ya sheria na KATIBA ya NCHI ili ziendane na wakati na anaesema hakuna sababu ya kubadilisha katiba kwa sasa huyo aisabiwe ni ADUI wa TAIFA la TANZANIA alaniwe vikali sana na ikiwezekana ahukumiwe kifungo cha maisha.

Hapa umechoma kwa ufasaha ndugu Mwiba .Katiba ndiyo jibu .
 
Mnyika, sasa huyo katibu kapona au vipi ? tupe basi updates kuhusu afya yake ! na hao wanaccm waliofanya hivyo hawajakamatwa ?? LOL
 
Kwa habari nilizopokea hivi punde, Katibu wa CHADEMA Kiteto- amekatwa mapanga na watu wasiojulikana kwa sababu ambazo bado naendelea kuzithibitisha kabla hatujatamka chochote. Lakini habari zingine nilizopokea hivi sasa ni kuwa sasa vyombo vya dola vimeanza kunyanyasa wananchi ambao walielekea kuunga mkono upinzani. Leo hii kwa muda wa zaidi ya masaa mawili sasa Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wilaya ya Kiteto amewekwa ndani bila sababu maalum. Yapo maeneo ambayo wananchi wanalalamika kunyimwa huduma kwa waliunga mkono upinzani. Huko ndipo tunapopelekwa kama taifa. Nimeweka suala hili hadharani mapema kabisa ili vyombo vya habari na taasisi za haki za binadamu mumulike yanayoendelea Kiteto. Nitaendelea kuwajulisha kadiri ninavyopata taarifa zaidi. Kuhusu nini CHADEMA tunafanya baada ya kupokea habari hizi; ni siri kwa sasa.

JJ

Halafu hawa ndio tunaambiwa kwamba wanafaa kwa usalama wa Taifa. CHADEMA wakiamua na wao kumkata kiongozi wa juu wa CCM mapanga si ndio 'amani' imepotea? Yatakuwa yale yale kama ya Wahutu na Watusi wataingia waliokuwemo na wasiokuwemo (Mungu apishilie mbali) lakini hali inaanza kutisha. Tumeona ya Wakenya walivyouana wenyewe kwa wenyewe, hata hawajakaa vizuri na sisi tunataka kuanza kuchinjana.
 
Kwa habari nilizopokea hivi punde, Katibu wa CHADEMA Kiteto- amekatwa mapanga na watu wasiojulikana kwa sababu ambazo bado naendelea kuzithibitisha kabla hatujatamka chochote. Lakini habari zingine nilizopokea hivi sasa ni kuwa sasa vyombo vya dola vimeanza kunyanyasa wananchi ambao walielekea kuunga mkono upinzani. Leo hii kwa muda wa zaidi ya masaa mawili sasa Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wilaya ya Kiteto amewekwa ndani bila sababu maalum. Yapo maeneo ambayo wananchi wanalalamika kunyimwa huduma kwa waliunga mkono upinzani. Huko ndipo tunapopelekwa kama taifa. Nimeweka suala hili hadharani mapema kabisa ili vyombo vya habari na taasisi za haki za binadamu mumulike yanayoendelea Kiteto. Nitaendelea kuwajulisha kadiri ninavyopata taarifa zaidi. Kuhusu nini CHADEMA tunafanya baada ya kupokea habari hizi; ni siri kwa sasa.

JJ

Labda ili tuendelee kuishi kwa amani, hatuna budi kukubali yaishe; yaani tuwazirie nchi maana ukiwapinga wanakutafuta, ukionesha mawazo yako kinyume nao wanaanza kujiuliza kwanini; na ukidiriki kuwanyoshea kidole wanang'aka! Hatuwezi kuishi kwenye nchi kama vile tumekopa. Hili naona bado nigumu. JJ tupatieni contacts Kiteto haya mambo yatafikia kikomo one of these days..! they sure will.

Upumbavu huu utatuisha lini watanzania? Huku ndani ya CCM mbona hamnazo wako wengi? Inakuaje hii jamani? CCM ni mabingwa wa kuhubiri amani na upendo kwenye majukwaa bila kusahau kukemea rushwa. Lakini hawa ndiyo mabingwa wa kupokea rushwa na kuvunja amani miongoni mwa jamii zetu. IGP Mwema upo au na wewe ni moja wa greenguards?

Polisi wametoa tamko lolote? Je, wale waliopigwa kabla ya uchaguzi kuna yoyote aliyeshitakiwa?

Kuna tofauti gani na warusha mishale wa Kenya?
 
Polisi wametoa tamko lolote? Je, wale waliopigwa kabla ya uchaguzi kuna yoyote aliyeshitakiwa?

Kuna tofauti gani na warusha mishale wa Kenya?

Nyie mbona mnahangaika na organ ileile?? polisi mahakama zipo pale kulinda madaraka yao yasipolwe na akina mbowe/mrema/maalimu Na si kukulinda wewe kwanza kama ingewezekana wangelipenda wewe masikini ungekufa mapema ama kuhama nchi ili wapate kuiuza vizuri.
Pili Mimi ningeonelea sisi wananchi hatuna sababu ya kushitakiana mahakamani/polisi Hakika tukikoseana tushaurianeni tu na mabaraza yetu ya asili na tusameheaneni huko mahakamani/polisi mhhhhh si mumemuona ndito alivyoua hadharani ,si mumemuona Balali walivyojitahidi kumficha.

Nyie akina mbowe/manyika/mrema kama kweli mna uchungu na nchi yenu na kama kweli mna nia thabiti na nzuri kwa watanzania basi tafuteni njia nyingine kwa BALLOT hakika hamtaweza.
 
Salamu zangu za pole kwa mhanga wa tukio hilo,Katibu wa CHADEMA Jimboni Kiteto. Poleni sana wanachama wa CHADEMA, wanamageuzi na watanzania wote kwa ujumla ambao tukio hili linatutia simanzi.Hakika damu na machozi ya watanzania hayataendelea kuidondokea ardhi ya mama yetu Tanzania, bila harufu ya uovu huu kumfikia Maulana.Inshala atatunusuru kama alivyowanusuru wana wa Israel utumwani Misri.
Binafsi naungana na wote wanaolaani kwa nguvu zote kitendo hiki cha kinyama, cha kipumbavu na cha uoga. Wahusika wote watambue kwamba wanayo kesi ya kujibu mbele ya umma wa watanzania na mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kitendo hiki ni aina nyingine ya UGAIDI, hivyo wahusika kama wametenda hivyo kwa sababu ya itikadi zao, hapa tunapata ushahidi mwingine kwamba tunalo kundi la itikadi za kigaidi humu humu Tanzania. Nia ya ugaidi wao ni kuwajengea watanzania hofu na kihoro wasiwaunge mkono wanamageuzi, ili watawala fisadi waendelee kuyakalia madaraka. Wamedanganyika, maana mbinu yao chafu haitawaletea mafanikio yadumuyo.
Hawajaanza leo,
  • Waliuliwa watanzania kule visiwani mwaka 2001, wanamageuzi hawakukata tamaa
  • Alivunjwa mkono Prof.Lipumba,harakati hazikukoma
  • Alimwagiwa tindikali Kubenea, magazeti bado yanafunua uozo
  • n.k
Zaidi sana wanachofanya bila kujua, ni kuongeza kurasa katika jalada la kesi yao. Watanzania hatusahau kama wengine wanavyodhani
  • Hata mwenzao mkaburu alifanya hayo hayo kule A. Kusini lakini haikuzuia saa ya ukombozi kuwadia
  • Kule Marekani waliuliwa akina Dr.Martin Luther na Malcom X, haikusaidia.
NDUGU ZANGU WATANZANIA,KAMWE UOVU HAUTASHINDA,ASIKATE MTU TAMAA HAPA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom