Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
WanaJF,

Wakati nasoma hili tamko.... naomba niendelee baadaye... ila nimefurahishwa na point hii ndani ya taarifa ya CHADEMA

Mtakumbuka kuwa CHADEMA kwa niaba ya kambi ya upinzani kilimsimamisha Victo Kimesera, mgombea ambaye kwa uchunguzi wa vyombo huru vya habari ndiye aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya ushindi ingawa hata hivyo matokeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi hayakuweza kuakisi ukweli huo.

Hongereni chama makini, mnatumia waandishi wa habari kujua mshindi... wakati mkijua wazi vyombo vyetu vingi vinaandika vikiwa Dar es Salaam,,, na pia sio makini kama vya Kenya ambavyo pamoja na uandishi wao pia kulikuwa na independent research organisation kuhakiki mambo kwenye uwanja wa ushindani... no wonder matokeo ya Kenya yalishabihiana kabisa na matokeo ya uchaguzi wa Kenya!!!
 
WanaJF,

Wakati nasoma hili tamko.... naomba niendelee baadaye... ila nimefurahishwa na point hii ndani ya taarifa ya CHADEMA



Hongereni chama makini, mnatumia waandishi wa habari kujua mshindi... wakati mkijua wazi vyombo vyetu vingi vinaandika vikiwa Dar es Salaam,,, na pia sio makini kama vya Kenya ambavyo pamoja na uandishi wao pia kulikuwa na independent research organisation kuhakiki mambo kwenye uwanja wa ushindani... no wonder matokeo ya Kenya yalishabihiana kabisa na matokeo ya uchaguzi wa Kenya!!!

Naona umeamua kutumia mfano mmoja tu kuelezea upande wako wa namna unavyofikiri mambo yalikwenda Kiteto. Mwana JF mwenzetu alikuwa Kiteto wakati wa uchaguzi na tulikuwa tunapata habari zote kabla Pinda na wenzake hawajafunga JF.

Katika hili, maelezo ya Mnyika kuhusu vyombo vya habari yana credibility kuliko spin za ccm.
 
Nimesoma Tamko la CHADEMA, lakini kwa ujumla bila kuingia ndani... bado nawaomba wanaJF kuisaidia CHADEMA kiufundi na kimawazo... Kuna hoja nyingi zilizoingizwa huko kwenye taarifa ni nyepesi mno... mfano hoja ya waliosoma... unaweza ku-prove by contradiction Kitila unajua Hesabu Mwanangu...


Dar es Salaam kunaaminika kuna kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, au least wajanja je? Vyama vya Upinzani vina Majimbo mangapi?

Matumizi ya CHADEMA na CCM kwenye uchaguzi yataendelea kutofautiana kwa sababu mbali mbali... Kitila akienda Kijijini matumizi yake ni Makubwa kuliko... mwanakiji wa Kijiji kingine akitembelea kijiji kingine... uhakiki wa Sh. ngapi zimetumika kwenye vyama vyote viwili bado... ni siri ya vyama hivyo ikiwemo CHADEMA... kwa sasa nguvu ya kuongelea hili haipo kwa kuwa hakuna sheria....

Ningeshangaa sana kwenye uchaguzi kama huo kusitokee mambo yoyote kama haya yaliyoripotiwa na CHADEMA, yataendelea kuwa hapo milele... kwenye Jimbo la Zitto, Dr. Slaa... lakini muhimu chama kinachoshinda hakitasema lolote.

Taarifa hii imesheheni theory mithili ya taarifa iliyoandaliwa na mwanafunzi anayechukua shahada ya uhazili ya pale chuo kikuu cha...
 
Nimesoma Tamko la CHADEMA, lakini kwa ujumla bila kuingia ndani... bado nawaomba wanaJF kuisaidia CHADEMA kiufundi na kimawazo... Kuna hoja nyingi zilizoingizwa huko kwenye taarifa ni nyepesi mno... mfano hoja ya waliosoma... unaweza ku-prove by contradiction Kitila unajua Hesabu Mwanangu...


Dar es Salaam kunaaminika kuna kiwangu kikubwa cha wanaojua kusoma, au least wajanja je? Vyama vya Upinzani vina Majimbo mangapi?

Matumizi ya CHADEMA na CCM kwenye uchaguzi yataendelea kutofautiana kwa sababu mbali mbali... Kitila akienda Kijijini matumizi yake ni Makubwa kuliko... mwanakiji wa Kijiji kingine akitembelea kingine... uhakiki wa Sh. ngapi zimetumika kwenye vyama vyote viwili bado... ni siri ya vyama hivyo ikiwemo CHADEMA... kwa sasa nguvu ya kuongelea hili haipo kwa kuwa hakuna sheria....

Ningeshangaa sana kwenye uchaguzi kama huo kusitokee mambo yoyote kama haya yaliyoripotiwa na CHADEMA, yataendelea kuwa hapo milele... kwenye Jimbo la Zitto, Dr. Slaa... lakini muhimu chama kinachoshinda hakitasema lolote.

Taarifa hii imesheheni theory mithili ya taarifa iliyoandaliwa na mwanafunzi anayechukua shahada ya uhazili ya pale chuo kikuu cha...


Unasema mambo bila kutoa mifano ya nini kina contradiction hapa. Au ndiyo yale yale ya Kikwete kukataa kuwa hakuna wizi BoT kabla ya kukubali na kudai kuwa wizi ni wa pesa za watanzania na sio pesa za wafadhali!?!?!?!?!
 
Mwafrika wa Kike

Utajitahidiu ku-spin lakini ukweli utabaki pale pale kwamba tamko lenu linaendelea kuwaambia Watanzania kwamba bado uwezo wenu ni mdogo sana, tena bado sana... hatuoni ya kujifunza naomba muongezi kamati yenu ya ufundi.. report haijatulia imejaa nyepesi nyepesi...


Nawaomba tena mukae chini mujiangalie vizuri... mujikosoe ninyi wenyewe kwanza...
 
Mwafrika wa Kike

Utajitahidiu ku-spin lakini ukweli utabaki pale pale kwamba tamko lenu linaendelea kuwaambia Watanzania kwamba bado uwezo wenu ni mdogo sana, tena bado sana... hatuoni ya kujifunza naomba muongezi kamati yenu ya ufundi.. report haijatulia imejaa nyepesi nyepesi...


Nawaomba tena mukae chini mujiangalie vizuri... mujikosoe ninyi wenyewe kwanza...

Kujikosoa kunaendelea mkuu!

Nadhani kama unakumbuka kuwa mimi nilikuwa miongoni mwa waliokubali "kushindwa kiteto" hapa JF. Baada ya Kiteto na yale yaliyotokea kwa viongozi wa chama (kupigwa kama wezi) na kile alichofanya Komba, nimefikia hitimisho kwa CHADEMA na vyama vingine inabidi vibadili mwelekeo.

Jambo moja najua kwa hakika ni kuwa, tatizo linaweza kuwa sio la vyama vya upinzani - kwa sababu kama vingekuwa havina nguvu basi Komba na Msekwa wasingefanya walichofanya Kiteto.

Katika hili, bado nawashukuru hao viongozi wa CHADEMA wanaoweka maisha yao kwenye line ili Tanzania iendelee kuitwa nchi ya mfumo wa vyama vingi na Kikwete apate ahueni anapoendeleza safari zake.

Najua wengi huko ccm mngependa kuona wapinzani wakipotelea mbali na kufutika kwenye uso wa dunia. Swali je, baada ya hapo, nchi hiyo inaitwa Tanzania itaitwa ya chama kimoja au?

Otherwise, mawazo yako nimeyapokea Mkuu na natumaini kina Mnyika wanasoma hapa!
 
Tunatoa Pole kwa Katibu huyo wa Chadema kukatwa Mapanga....Pia tunalaani ukiukwaji mkubwa wa Haki za Kibaadamu. Ikiwa KUBENENA AMEPIGWA MAPANGA na wasiojulikana...katibu wa chadema na watu wasojulikana...matukio ya ujambazi yanayoendelea kila leo...Hivi SAID MWEMA bado Upo? Jiuzulu basi....kama hutaki take serious actions...Mnapenda kujifananisha na Mzee Mwinyi..Kumbe Hamuwezi....
Hadi sasa tunaingia usiku..hakuna update yaliotokea huko Kiteto?
kama kuna picha Tumeni basi...Mnyika ulisema utafuatilia.vipi sources zenu...[

POLISI MATUKIO MADOGO KAMA HAYO NDIO YANAYOZAA CHECHE....MATOKEO YAKE HAKUNA MTZ ALIETAYARI KUIONA NCHI INAELEKEA KENYA..../SIZE]
 
Problem is not CHADEMA, tatizo ni policy na uongozi mzima wa CHADEMA. I agree 90% with what JM said, i don't agree on management and policy of the party.

Nimeshakwambia kwamba CHADEMA kina sound kama chama cha Hon. Mbowe, and that back me off. I need to see more committement with in CHADEMA, so i can be more confidence to join the movement.

JM, how long ungozi unakaa madarakani ndani ya CHADEMA? Why kila mtu ndani ya CHADEMA ni mmesemaji mkuu? I need to know those few things.
 
John,
Kama nilivyosema hapo awali tafadhali usikwepe maswali toka kwa wananchi hii ni dalili mbaya ya kwamba huko tayari au unajenga tabia ya kukwepa kuwajibika.

Nimesoma pamoja na mambo mengi maoni uliyoshauriwa na wachangiaji wengine kuwa hapa unategwa na huenda labda utoe siri za CHADEMA, siamini kama kweli umekubaliana na hili kwani maswali yangu yalikuwa ya wazi na hayajataka utoe 'siri' za CHADEMA (kama zipo). Mimi ni mwananchi ambaye ninatimiza wajibu wangu wakutaka kujua kwa undani wa wale wanaotaka tuwape dhamana ya kuongoza nchi hii. LAkini endapo hapo ulipofikia ndiyo 'black and white' yako basi hapana shaka umenipa mwanga wa kujua wewe ni kiongozi wa namna gani. Kumbuka nilitaka kujua kama wewe ni mwanasiasa mpya au ni walewale.

Ninachokushauri usiwe mwoga na usijijengee dhana potofu kuwa kila swali lina kutafuta au kukuchimba. Sasa tunaishi katika ulimwengu tofauti, ulimwengu ambao unakutaka kuamini unayosema ni sahihi na kuyasimamia katika ukweli. Hizi siasa za uchundo haziwezi kuivusha nchi yetu katika matatizo yaliyopo. Usiogope kwamba labda utakosa kuteuliwa kugombea ubunge wa Ubungo endapo tu utasema kweli na kusimamia hayo unayoyasema.

Juu ya hoja zako kuhusu Mzee Kingunge nadhani kwa wasomaji makini wamepata picha yako kamili kuwa wewe ni mtu wa namna gani. Mimi ninakuona kuwa bado huja-mature kisiasa na huenda wewe sio mvumilivu pia, probably kuna mambo ambayo yanakusaidia kuficha hizo weakness zako kwa sasa. (Huu ni mtazamo wangu).

Ninakwambia haya uyachukulie kama ni changamoto, kwani anayekutakia mema hukwambia ukweli wakati wote, isije ikafikia mahali mambo yameharibika then wanajitokeza watu wengine wakasema tuliyajua lakini wakaamua kukaa kimya. Kwa hiyo kama utaamua kuniona mimi mwananchi ninayehoji kuwa ni 'Kenge' ni sawa tu kwani hicho ndiyo kipimo halisi cha viongozi wetu jinsi wanavyotuona sisi wananchi.

Kwa vile umekataa kueleza makosa mliyoyafanya ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wa chama chenu katika chaguzi zilizopita basi mimi ninayaweka bayana makosa yenu kama ifuatavyo:

Chama chenu kilishindwa kusoma wakati na mahitaji ya kweli ya watanzania katika uchaguzi mkuu uliopita. Kwa pamoja mlikubali hoja za Mwenyekiti wenu chama kitumie sehemu kubwa ya resources zilizokuwepo kwa ajili ya uchaguzi kwa kutafuta kiti cha Urais ambacho kwa tathmini ya haraka hakukuwa na utafiti wa kutosha ulionesha kwamba mgombea wa CHADEMA angeshinda kiti hicho.

Resources hizo zingeweza kutumiwa vizuri kwa kuweka mkazo wa kupata wabunge wengi ambao hasa ndiyo mahitaji ya kweli ya wananchi. Ninyi kama viongozi mlishindwa kumwambia 'Mfalme yuko uchi' kwa tamaa ya kupata uteuzi wakugombea majimbo mliyoyataka ama kuweza kunufaika kupitia udhaifu wa Kiongozi wenu. Hili kosa litaendelea kuwatafuna hadi pale mtakapokiri juu ya hili, la sivyo CCM can be seen as a lesser devil.

Kipindi baina ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi Mdogo wa Kiteto chama chenu kimeonesha kugubikwa na maswali yasiyokuwa na majibu ya moja kwa moja na hata kupelekea kupunguza imani kwa nyie hasa ambao mnataka dhamana ya kuongoza nchi hii.

Kwanza,
Uteuzi wa Viti vya maalum vya ubunge toka CHADEMA. Uteuzi wa viti hivyo ulizua malalamiko ya chinichini ambayo yalionesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi na demokrasia ya kweli. Iweje viongozi na mabwanyenye yenye fedha zao ndani ya chama ndiyo waamue nani apewe kiti cha ubunge maalum? Hivi tunajenga nchi ya namna gani pale mtu moja anaposema lazima mwanangu apewe kiti kimoja na mwingine alazimishe anayemtaka yeye kwa sababu zake lazima apewe? Hilo ni doa na kasoro za wazi nilazima chama chenu kijiangalie na kujisafisha hapo, vinginevyo tunaona hamko kwa ajili yetu bali ni kwa ajili ya wachache na wateule.

Pili,
Uteuzi wa mgombea wa Kiteto, umeonesha kurudia makosa au mwendelezo wa yale yaliyopo ndani ya chama chenu. Uteuzi wa Kimesera umetokana na mtazamo wa kibwanyenye kwamba kuna watu ndani ya CHADEMA ndiyo wenye sauti kuliko wanachama wengine. Kimesera siyo mgombea bora, kwa mara nyingine tena mliamua kufumba macho kwa makusudi kwa sababu tu ametaka kugombea na hakuna wa kuweza kuchallenge hilo, hii haikubaliki, you have to change kama kweli mnataka ridhaa ya wananchi.

Namalizia kwa kusema kuwa si usaliti kuongea weakness za CHADEMA.
 
..siku si nyingi itabidi kenya waje "kuleta amani" tanzania!

hata sisi tukae mkao wa kula.siku si nyingi hata wakenya watazalia tanzania ili kuleta maendeleo. swali langu kwa mnyika, je ndio hivyo mnakaa dar es salaam, wakati ndugu hao mmeisha watumia vya kutosha. ninadhani kuna haja ya kulivalia njuga maana huyu jamaa kafia vitani. ikiwezekana helicopter hiyo irudi tena kuonyesha kuwa hamitumii tu wakati wa uchaguzi tu bali hata wakati wa majonzi.
 
hakika hili laja na halitakawia,maana kama vyombo vya kuwalinda wananchi ndiyo vinatumika kuwadhalilisha na kuvunja haki zao,zaja siku polisi hhataishi mtaani maana atakuwa tayari ni adui mkubwa wa wananchi.Uadui mkubwa tunaouona DAR kati ya mgambo wa jiji na wamachinga muda si mrefu utahamia kwa polisi na wananchi,na hapa tutakuwa tumefika pabaya sana. Angalia blog ya michuzi yaliyojili jana kwa mgambo wa jiji.Mwema,siku zaja taratibu na hazitochelewa,moto utawaka.

Mambo yakibana baadaye si ndo wanakuja kutuambia kuwa wao ni "BANGUSILO" hatutapenda kusikia kauli za kijinga kwa mtu mzima kwani bado una uwezo wa kukataa kutumiwa sasa. Huo ubangusilo hatutaki uujue baada ya kuwaumiza watanzania ujue sasa kabla hujatenda,
 
Binafsi nilipoiangalia ripoti mara ya kwanza nikaona ina mapungufu kadhaa. nilivyo angalia nani kaandaa ripoti ktk signature sikulaumu sana. ila Chadema walitakiwa kuipitia hio ripoti kabla hawajaipublish...

Sipendi kuyarudia waliotoa wenzangu...ila kimoja ambacho cha upinaadamu kuwa Chadema walipaswa kuweka THANKS kwa vyama vingine ambavyo kwa namna moja au ingine walipeka majeshi(inputs) yao kule kiteto. Hili Halimo ktk RIPOTI hio. Hii kuonesha mshikamano ambao umeenza kuoneshwa ktk kipindi cha hivi karibuni.

Ieleweke CCM hawashindi kwa kwa sera...lkn YAPASA as Upinzani kuwa Makini ZAIDI, na hata pale tunaposhindwa basi tutoe sababu zinazoingia AKILINI...unaweza ukaweka sababu 2 muhim tosha... Kuliko kuweka page 10 kujaza USANII.
 
Ni kuwa nimekaa kimya kwa muda tangu kipindi cha mwezi wa pili,

Taarifa za kuaminika ni kuwa jana majira ya saa nane mchana mkuu wa wilaya ya Kiteto alienda kituo cha polisi Kiteto na kuhoji ni kwa nini hadi sasa viongozi wa CHADEMA Kiteto hawajakamatwa? sijui kama kuna amri ya kuwakamata ama laa.

Pili , ni kuwa viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitishwa sana na viongozi wa kiserikali wa CCM wakiwaambia kuwa watakiona cha moto kwani wao walikuwa vimbelembele.

Tatu,wafanyakazi wa Halimashauri ambao walionyesha kutokukubaliana na maagizo ya kupindisha uchaguzi wa Kiteto wameanza kupata vitisho na hata wengine kuambiwa kuwa watahamishwa mara moja na wengine kuambiwa watafukuzwa kazi ,mmojawapo ni aliyekuwa anafanya kazi kitengo cha maliasili na utalii ,kaitwa leo asubuhi na kutishwa sana .

Mapambano haya ni magumu sana na haswa kwa wananchi ambao ni innocent kuna haja ya kuungana nao na kuwapa moyo zaidi.

Nimeongea na Katibu wa CHADEMA ambaye amelazwa kwa kukatwa mapanga anaongea kwa taabu sana hivyo akiweza kusimulia basi tutayaweka yote hapa upenuni.

Sina taarifa kama serikali imefungua kesi kwa wale wote waliowajeruhi viongozi wa CHADEMA hadi sasa na hili linaendelea kuwapa hofu wananchi kuwa kumbe CCM wanaweza kupiga watu na kuwaumiza vibaya ila hakuna hatua zinazoweza kuchukuliwa juu yao ,hili nalo kuna haja ya kulipigia mayowe na sio kelele tena maaana hawasikii hawa jamaa.
 
Ni leo hii kuna mtu kasema kwamba Wapinzani warudi kwenye Vijiji na Kata . Nilisema kwamba siasa za vijijini ni ngumu sana .Sasa kabla hakujakucha mmesha ona kwamba kazi ni kubwa .JK nadhani bado yuko Kenya anashangilia na IGP atasema hawajapata taarifa .Pinda bado anapewa heshima za kijadi watanzania wanaumia na Katiba ya Nchi inakiukwa damu inamwagika .Kisa madaraka .
 
The government yesterday gave a three-day ultimatum to the publisher and editor of a Kiswahili tabloid, `Tanzania Daima`, to apologise or face punishment, for what it described as distorting information and grossly violating laws and code of ethics in its reports on the just-concluded by-elections in Kiteto Constituency, Manyara Region.

In a statement issued by the Tanzania Information Services (Maelezo) in Dar es Salaam, the government said the newspaper printed two editions with the same issue number (1179), on the same day, when reporting the election results, contrary to the Newspaper Act Number 3 of 1976.

In first edition bearing number 1179, printed on February 25, this year, the tabloid reported that Chadema`s parliamentary aspirant was leading by 71.8 per cent, and that the ruling CCM`s candidate scooped votes in one ward only.

According to the government statement, the elections results printed in the same newspaper issue reported that CCM had won Kiteto elections, scooping votes in 13 wards out of 15, as opposition (Chadema) leaders accepted the defeat.

``The newspaper had grossly violated the Newspaper Act of 1976 by printing a special edition without permission or informing the Newspapers Registrar. Tanzania Daima did not present copies of the two editions to the registrar as required by the law,`` said the statement.

On the other hand, the Tanzania Information Services said the tabloid distorted reports on the election results by publishing results without consulting the relevant authorities--National Election Commission (NEC).

Authorities said the newspaper breached code of ethics by printing and circulating information that confused members of the public on the election results, which could fuel civil unrest.

``On top of that, the editor of the newspaper was called by the registrar to clarify on the confusion, but refused to pay heed,`` said the statement.

``We are giving `Tanzania Daima` three days to apologise for distorting information, violating newspaper laws, information code of ethics and disrespecting order of the registrar?otherwise, the newspaper will be punished in accordance with the Act,`` said the statement.

In a quick response yesterday, Tanzania Daima Managing Editor, Absalom Kibanda, refuted claims that they printed two editions on the same day.

He explained that they printed some copies for up-country regions which showed that chadema was leading in seven wards out of 15, as the paper went to press at around 8.00 pm.

``We sent the copies, but continued to monitor the election trend in various wards. At around 11pm we got the election results, and other copies for Dar es Salaam that showed that CCM had won elections by scoping votes in 13 wards out of 15,`` said Kibanda.

``We asked Chadema leaders who accepted that chances to win the election were minimal. These were clearly reported in our reports. In fact, we did not print two editions but we were forced to produce copies for Dar es Salaam and upcountry customers, because of transport problems.``

The editor admitted that they failed to communicate with the registrar on the problem, but insisted that they published only one edition on that day and not two as claimed by Maelezo.


SOURCE: Guardian
 
Kama mamefanya kosa waombe msamaha na kama hawajafanya kosa hawana haja ya kuomba msamaha, simpo.
 
Do we still use the old laws of one party state and ujamaa to govern? no wonder they (Sirikali) are troubled by internet!

Good old days, pne had to apply for special permission to print a second edtion, this was done by Uhuru, Daily News and Mfanyakazi do not forget Ngurumo.

We live in modern days where phrase "extra extra hear all about it" are what keep the public informed and not waiting for taarifa rasmi kutoka Maelezo (our own AP/Reuters) on issues.

The media platform has changed, it is competition on who reports what first!
 
Kama mamefanya kosa waombe msamaha na kama hawajafanya kosa hawana haja ya kuomba msamaha, simpo.

Hivi mtu akisema fulani ameshinda kwa asilimia 70; kwa matokeo ambayo ameyapokea mpaka wakati fulani ana kosa gani? Kwa matokeo ya zile kata chache za mjini ni kweli CHADEMA ilikuwa ikiongoza. Hebu tuwekewe hapa hiyo habari ya Tanzania Daima inayolalamikiwa na serikali tuijadili. Tanzania Daima si ilikuwa na waandishi Kiteto wakati wa uchaguzi?

Asha
 
Haya Bwana,Mie nilifikiria kuhusu ili baada ya Td kuonekana kumetetea Lowassa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom