Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Mnyika

Naona unaingia kwenye tundu la sindano ambalo watu wamekutegea. Jitahidi kutokujibu na kutolea maelezo kila kitu.

kumbuka hapa kuna wenye nia njema na wasio na nia njema kwako na kwa chadema. Kwa hiyo watapenda kujua unafanya au mnafanya nini ili nao wabuni njia za kukinzana nanyi. Usimpe nafasi mshindani wako kujua una silaha gani na unataka kufanya nini.

nitamsg jioni.

Unachosema wewe ni kwamba kwenye msafara wa mamba kenge hawakosi, nakubaliana na wewe kabisa!
 
Aljazeera

Asante ndugu yangu.

Chochote ninachosema hapa ni kile ambaocho ni unclassified, kiko kwenye public terrain sema tu watu hawana kwa kuwa ama sio wanachama wa kawaida au sio wafuatiliaji au kinasemwa kwenye mikutano ya hadhara bila kutoka kwenye vyombo vya habari.

Yoyote asitegemee kwamba nitatoa SIRI za CHADEMA hapa; wala SIRI zangu binafsi hapa-for that matter.

Hapa ni mjadala wa wazi wa umma, tunajadili yale mambo ya wazi. Na kwa kiasi kikubwa, tunatoa maoni yetu binafsi.

Hivyo usiwe na hofu kaka; ukiona baadhi maswali sijibu- si kwa sababu sina majibu. Ni kwa sababu sitaki kujibu, na sababu moja wapo ya kukataa kujibu ni kutokutoa SIRI.

Ukisoma kwa makini utaona mengi ya nisemayo kuhusu chama nayatoa toka tovuti ya Chadema kwa hiyo ni taarifa rasmi za chama zilizo tayari kwa umma.

JJ
 
Unachosema wewe ni kwamba kwenye msafara wa mamba kenge hawakosi, nakubaliana na wewe kabisa!

Teh teh teh. Kama upo! Kuna Kenge pia, na kwa kweli Kenge wakiwa wengi ndio maana mara nyingine mamba wanaamua kutoweka kabisa.

BTW: Leo walau nimeweka kijiwe hapa, leo ni siku yangu ya kuwa JF- natoweka na kurejea

JJ
 
sidhani kama kuorodhesha matumizi ya fedha za kampeni ndogo ndogo za chaguzi ni SHERIA, correct me if am wrong (even though am not sure) that being said, kama sio sheria kuwakilisha matumizi ya fedha za kampeni sioni ulazima wake, na IWAPO kama ni sheria basi naunga mkono hoja yako mnyika !

other thing is, i strongly DISAGREE kwamba uchaguzi mliibiwa, zitto nadhani aliibua kifua mbele na kusema sijui nini kuhusu daftari la kupiga kura, sasa namuuliza hiyo ishu ya daftari alikuja kulijua baada ya matokeo ya uchaguzi kutoka ama kabla ? naombeni mfute machozi yenu ya kenge hayo na mpunguze excuses, kubalini kwamba mmeshindwa and we move on lakini unaposema kwamba mmeonewa (AND YOU KNEW WHERE THE MISTAKE WAS PRIOR TO ELECTION refer: madai ya zitto (a)kwamba daftari la uchaguzi lilikuwa na walakini) MLIFANYA NINI ILI KUHAKIKISHA HATUA ZA KISHERIA ZINAFUATWA ILI KUHAKIKISHA MAMBO YANAKUWA MSWANO "? mimi napinga kabisa haya madai, na lazima tuyakemee kila pale mnaposhindwa chaguzi, and ndio mnaanda mind set kwa watu kwamba kila mnaposhindwa chaguzi basi ndio mmeibiwa ?? and above all, how did you know mliibiwa ??

kada!!
swala la kuweka hela ulizotumia kwa tanzania siyo sheria ila ni kitu kinachoitwa ''good practice''. usiposimamia hizo kanuni za fedha basi ujue mwaka 2010 watu wenye fedha za EPA na zile za kagoda watagombea hata urais na mimi nakuhakukishia kuwa hata kikwete na mvuto wake anaweza shindwa uchaguzi huo.

kuhusu swala la hatua za kuchukua kama daftari lina walakini sidhani kama ni muafaka kuzisema wakati ule wa uchaguzi. y? kwa sababu tendency ni kutoyachukulia haya malalamiko kwa uzito wake. imeshasemwa mara nyingi kuwa tume ya uchaguzi siyo huru na inafanya kazi kwa maelekezo ya serikali. sasa chadema wakalalammie wapi? option ni mahakamani lakini si unajua tena kesi za uchaguzi? za mnyika bado hata kuanza.

anyway option nyingine zilizopo ndio hatutaki kuzisema maana watu wa usalama wa taifa waliko huku JF wataripoti halfu tupelekwe mateso kama kina maxence de mello.
 
Kwa habari nilizopokea hivi punde, Katibu wa CHADEMA Kiteto- amekatwa mapanga na watu wasiojulikana kwa sababu ambazo bado naendelea kuzithibitisha kabla hatujatamka chochote. Lakini habari zingine nilizopokea hivi sasa ni kuwa sasa vyombo vya dola vimeanza kunyanyasa wananchi ambao walielekea kuunga mkono upinzani. Leo hii kwa muda wa zaidi ya masaa mawili sasa Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wilaya ya Kiteto amewekwa ndani bila sababu maalum. Yapo maeneo ambayo wananchi wanalalamika kunyimwa huduma kwa waliunga mkono upinzani. Huko ndipo tunapopelekwa kama taifa. Nimeweka suala hili hadharani mapema kabisa ili vyombo vya habari na taasisi za haki za binadamu mumulike yanayoendelea Kiteto. Nitaendelea kuwajulisha kadiri ninavyopata taarifa zaidi. Kuhusu nini CHADEMA tunafanya baada ya kupokea habari hizi; ni siri kwa sasa.

JJ
 
Hivi kuwa mpinzani Tanzania ni makosa?
Mbona kadhia sana?
 
Asante Mnyika kwa hii habari!

Hii story nilianza kusikikia fununu jana kuwa mafisadi ndani ya ccm wanataka kuendeleza ubabe dhidi ya upinzani na sasa naona wameamua kufanya kweli.

Endelea kutuhabarisha katika hili. Mara ya mwisho tulivyoweka picha za Kiteto, kina Pinda na wenzake wakafunga JF, sasa hii sijui watafanya nini!
 
Mnyika

Naona unaingia kwenye tundu la sindano ambalo watu wamekutegea. Jitahidi kutokujibu na kutolea maelezo kila kitu.

kumbuka hapa kuna wenye nia njema na wasio na nia njema kwako na kwa chadema. Kwa hiyo watapenda kujua unafanya au mnafanya nini ili nao wabuni njia za kukinzana nanyi. Usimpe nafasi mshindani wako kujua una silaha gani na unataka kufanya nini.

nitamsg jioni.

John
Naamini maoni uliyopewa hapo juu ni bora sana.
Na wabunge kama hawa wanaowekwa ni hasara tupu bungeni!!
 
Labda ili tuendelee kuishi kwa amani, hatuna budi kukubali yaishe; yaani tuwazirie nchi maana ukiwapinga wanakutafuta, ukionesha mawazo yako kinyume nao wanaanza kujiuliza kwanini; na ukidiriki kuwanyoshea kidole wanang'aka! Hatuwezi kuishi kwenye nchi kama vile tumekopa. Hili naona bado nigumu. JJ tupatieni contacts Kiteto haya mambo yatafikia kikomo one of these days..! they sure will.
 
Upumbavu huu utatuisha lini watanzania? Huku ndani ya CCM mbona hamnazo wako wengi? Inakuaje hii jamani? CCM ni mabingwa wa kuhubiri amani na upendo kwenye majukwaa bila kusahau kukemea rushwa. Lakini hawa ndiyo mabingwa wa kupokea rushwa na kuvunja amani miongoni mwa jamii zetu. IGP Mwema upo au na wewe ni moja wa greenguards?
 
wenzako wanapongezana kuwa Kikwete "ameleta amani Kenya" baada ya Annani na wenzake kushindwa. Naona kuna tafsiri nyingi sana za neno amani
 
Ama kweli ukishangaa ya PNU utayaona ya CCM,Mzee wa watu Koffi Annan katumia muda wake mwingi pale nairobi takribani mwezi mzima mpaka akakasirika akataka kuondoka,leo tunaambiwa Kikwete ndiyo kafanikisha,mmmmmh,ama kweli siasa safi za CCM alikwendanazo Nyerere,
 
Asante Mnyika kwa hii habari!

Hii story nilianza kusikikia fununu jana kuwa mafisadi ndani ya ccm wanataka kuendeleza ubabe dhidi ya upinzani na sasa naona wameamua kufanya kweli.

Endelea kutuhabarisha katika hili. Mara ya mwisho tulivyoweka picha za Kiteto, kina Pinda na wenzake wakafunga JF, sasa hii sijui watafanya nini!

Na kama huu ndio mwelekeo, basi utakuwa ni mwanzo wa ukombozi timilifu wa wananchi wa nchi hii. Maanake watu wataanza kujua adui hasa ni nani.
Kinachotakiwa tu ni uongozi imara unaoweza kusimamia mapambano hayo kwa dhati.
 
hakika hili laja na halitakawia,maana kama vyombo vya kuwalinda wananchi ndiyo vinatumika kuwadhalilisha na kuvunja haki zao,zaja siku polisi hhataishi mtaani maana atakuwa tayari ni adui mkubwa wa wananchi.Uadui mkubwa tunaouona DAR kati ya mgambo wa jiji na wamachinga muda si mrefu utahamia kwa polisi na wananchi,na hapa tutakuwa tumefika pabaya sana. Angalia blog ya michuzi yaliyojili jana kwa mgambo wa jiji.Mwema,siku zaja taratibu na hazitochelewa,moto utawaka.
 
Na kama huu ndio mwelekeo, basi utakuwa ni mwanzo wa ukombozi timilifu wa wananchi wa nchi hii. Maanake watu wataanza kujua adui hasa ni nani.
Kinachotakiwa tu ni uongozi imara unaoweza kusimamia mapambano hayo kwa dhati.

Na mbaya zaidi inakuwa pale ambapo vyombo vya dola vinageuka kuwa vyombo vya chama fulani cha siasa badala ya kuwa vyombo vya wananchi wote. Wakati John Komba kaingilia kampeni ambazo si zake mwezi jana, eti polisi "WALIMUOMBA" ashuke jukwaani na azime muziki na kuondoka! Angekuwa ni Mbowe, Mrema, Mtikila ama Lipumba kafanya faulo hiyo nadhani angelipukiwa na mabomu ya mchozi hadi akome.
Sasa itafikia wananchi tutachoka, sijui nini kitatokea hapo!
 
naona sasa hapa watu wamejaa theory kibaooooooooooo, eti watu wasimuulize mnyika kwa sababu wamemuwekea mtego, haya bana ! naona mnyika amekuwa sele-briti siku hizi !
 
wazee wakuu wa theory wako wapi,?? wenyewe utawasikia ccm hao wamefanya hivyo ! teh teh tehhehe.............am serious ! njoeni bana tuwasikie.
 
Na mbaya zaidi inakuwa pale ambapo vyombo vya dola vinageuka kuwa vyombo vya chama fulani cha siasa badala ya kuwa vyombo vya wananchi wote. Wakati John Komba kaingilia kampeni ambazo si zake mwezi jana, eti polisi "WALIMUOMBA" ashuke jukwaani na azime muziki na kuondoka! Angekuwa ni Mbowe, Mrema, Mtikila ama Lipumba kafanya faulo hiyo nadhani angelipukiwa na mabomu ya mchozi hadi akome.
Sasa itafikia wananchi tutachoka, sijui nini kitatokea hapo!

Wameuza nchi na wanatafuta sababu ya kuwaondoa wananchi kutoka kwenye maeneo yao kwa visingizio vya kuleta fujo!
 
Ama kweli ukishangaa ya PNU utayaona ya CCM,Mzee wa watu Koffi Annan katumia muda wake mwingi pale nairobi takribani mwezi mzima mpaka akakasirika akataka kuondoka,leo tunaambiwa Kikwete ndiyo kafanikisha,mmmmmh,ama kweli siasa safi za CCM alikwendanazo Nyerere,

Shukrani,
Si kukasirika tu. Annan alitukanwa na yule mama Martha Karua. Mpaka Bi Mandela akaona aibu akaanza kumpa lecture mwanamke mwenzake. We acha tu. Leo anakuja Vasco Da Gama akipeleka ujumbe wa vitisho kutoka kwa swahiba wake GB tunashangilia Kikwete amefanikisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom