Pundamilia
I have never planned to be a career politician- take this from me. Kuna miaka ambayo nimejipangia ya kufanya siasa. Maisha ni zaidi ya siasa. Naamini utumishi wangu katika miaka hiyo, utakuwa umetosha kuwapisha wengine ili nao watumikie.
Kwa hiyo, kunifananisha na Kingunge aliyekuwa tuyari kusema uwongo kwa sababu tu ni Mwanasiasa ni kunitukana na kuharibu maana nzima ya siasa. Watu kama Kingunge ndio wanafanya siasa kuwa mchezo mchafu.
John hapa umepotoka, kukufananisha na Kingunge si kosa na wala siyo matusi. Mchango wa Mzee Kingung kwenye siasa ni mkubwa na wala sio wa kubeza kiasi hicho. Tafadhali consult your personal advisors on how to communicate and answer questions kutoka kwa watu mbalimbali. Mimi na wewe hatufahamiani lakini nina haki ya kujua wewe ni mtu wa namna gani ili niweze kujenga imani kuwa ni kiongozi wa namna gani. Hakuna njia nyingine yeyote ila ni kukuuliza maswali ambayo nina uhakika yanahitaji umahiri wa kuyajibu.
Na kwa kweli, i stand for principle, and certain values I am brought up with. If I will be forced to compromise my values, just because of politics, then I will quit politics in the first place. Naomba uyanukuu haya maneno yangu, uyahifadhi na uyatumie kunihumu nikienda tofauti. Ni muumini mzuri wa maneno ya Mwalimu kwamba ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi(ingawa suala la ardhi natofautiana naye kiasi), siasa safi na uongozi bora!
Maneno yako yananifanya niamue kutokujibu maswali yako kwa kina kwa kuwa naisoma dhamira yako katika maneno yako. Kitendo cha kutamka kwamba CCM ni chama cha watu na pia umenihukumu tayari kuhusu hulka yangu ya kisiasa.
John, kiongozi bora ni yule ambaye hakimbii wananchi, kwa hapa usinikwepe kwa kutumia dhana dhamira. Hiyo ni mbinu ya wanasiasa wa zamani au wale waoga. Please go to my questions unijibu na kama labda huna majibu ya papo kwa hapo unaweza kuniambia utanijibu baadae, lakini si vema kukwepa maswali kwa njia hiyo.
That said- Majibu kwa Maswali yako
1. Kosa la CHADEMA ni kuruhusu CCM kuiba uchaguzi- kwa kutoshinikiza kwa nguvu zote mapema sana mabadiliko ya mwenendo wetu wa uchaguzi. Lengo la 2008 tuliojiwekea ni mbali, shinikizo lingepaswa lianze kwa nguvu zote toka mwaka 2006. Pia uchaguzi wa ndani ya chama tulipaswa kuufanya toka mwaka 2007 ili kuwa na miaka mingi zaidi ya kuwaridhisha wakina Tomaso kabla ya mwaka 2010.
Hapa John, sikubaliani na wewe. Kwa mtazamo wako unaona kwamba wale wanaohoji udhaifu wa CHADEMA basi ni kina Tomaso na wanahitaji kuridhishwa tu. Nadhani hii si kauli ya uwajibikaji, sisi wananchi tunataka chama ambacho kitakuwa na kiko tayari kuwajibika kwa wananchi, si vema mkaona kila mawazo ya wananchi ambayo nitofauti na mawazo yenu basi huo ni 'usaliti' hapana, endapo mnataka dhamana ya uongozi wa nchi yetu inabidi mje na hoja za kimsingi na wala sio hoja za kutaka kuturidhisha.
Lakini kwa ujumla, mwelekeo tunaokwenda ni sahihi, na makosa hayo madogo, yanaweza kurekebishika 2008 mpaka 2010. Kosa lingine, ni kushindwa kuwafanya wananchi wachangie hizi harakati zetu kila mahali, kuna baadhi ya watu pamoja na kuwa wanapenda upinzani- lakini wanaona kuwa kama si wajibu wao kuufanya upinzani ushamiri. Wanaona kama ni wajibu wa viongozi wa upinzani wenyewe. Changamoto kwetu ni kufanya wote tuwe kwenye same page.
Hapa ndipo ninapochoka na siasa za wanasiasa wa nyumbani. Hampendi ku-admit weakness katika vyama vyenu especially katika kueleza makosa ambayo mmekwisha yafanya. Hili swali kwangu lilikuwa ni muhimu kujua kuwa wewe ni mwanasiasa wa aina gani, huenda unaimba mwimbo na kucheza mdundo mwingine. Tunahitaji wanasiasa ambao wako tayari kueleza kwa uwazi matatizo yaliyokuwepo katika chaguzi ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wa chama chenyewe. Kuna malalamiko juu ya namna ya uongozi wa juu wa Chadema unavyofanya kazi, kwa maana ya uwezo mdogo wa kisiasa alionao Mwenyekiti pamoja na vision yake yeye mwenye binafsi.
Kumekuwa na tabaka la watu ambao ndani ya chama hawaguswi kutokana nguvu zao kifedha ambao hao wanahodhi demokrasia ndani ya chama. Najua kwamba kwa mwanasiasa mwoga hawezi kuongea ukweli kwani huwa anajengwa na tamaa na ubinafsi ndani ya fikra zake, huogopa pengine atawajibishwa ndani ya chama au atanyimwa anayoyafaidi kwa sasa au nafasi yake ya kuteuliwa kuwania kiti cha ubunge katika jimbo fulani itakwenda na maji. Tunataka mabadiliko ya kweli na si vinginevyo
2. Kuhusu Kiteto, mimi sio mkazi wa Kiteto- lakini jua kwamba CHADEMA tuna diwani kwenye kata ya mjini kabisa Kibaya, diwani wetu kule amewatumikia wananchi vizuri toka 2005 ndio maana tunakubalika. Kimesera wakati wote amekuwa mstari wa mbele kuwatetea wanaKiteto hata baada ya kushindwa ubunge. Rejea sakata la wakulima ambalo hata LHRC ilijitokeza kulifuatilia.
Nilitaka kujua ni nini priorities za wananchi wa Kiteto, it is very simple na wala haihitaji kupiga kampeni kwa uchaguzi uliopita. Kama unavijua utupatie nadhani huenda hapo ndipo mlipokosea, inawezekana mmejitahidi sana lakini hamkudeliver hatimaye hamkueleweka na mkashindwa. Ninahitaji kujua ili niweze kutoa mchango wangu wa kusaidia nini kifanyike.
3. CHADEMA inahitaji reforms, hilo nakubali. We always strive to be better, and if we get there we will strive to be the best, ndio maana tumeshaanza reforms toka 2006. Soma thread ya CHADEMA must reform nimeeleza utekelezaji. Lakini sikubaliane tujireform kuwa kama CCM,
Mimi si mwana CCM, lakini nimeweza kushirikishwa katika mambo mbalimbali ya chama chao bila ya kuwa mwanachama. Na vivyo hivyo ningependa CHADEMA iwe na nafasi ya kuwashirikisha wananchi wengi bila ya kulazimika kuwa wanachama. Ikumbukwe kuwa wanachama wa vyama vya siasa ni wachache sana kulinganisha idadi ya wananchi wengine.
umesema CHADEMA ni chama cha mabwanyeye na kwamba CCM ni chama cha watu- lakini ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama cha demokrasia na maendeleo-utawala watu, lakini CCM ya leo si sawa na CCM ya Nyerere- CCM ya leo ni Chama Cha Mabwanyeye kama nitatumia neno lako mwenyewe
John, sisi wananchi tunaona hivyo kuwa chama chenu ni cha mabwanyenye na kama umeamua kutokulisemea hilo basi ninaamini kuwa ni zito kwako kuliongelea, lakini halina mjadala. Kuweni wa wazi ili tuwetayari kuwaunga mkono kwa dhati kama wananchi.
Karibu ujiunge na CHADEMA, tembelea
www.chadema.net kwa maelezo zaidi
Nadhani nafasi hii ya kuwa free from Chama cha siasa ndiyo nzuri kwani hainizibi mdomo wa kuongea, sitapenda kuwa katika mifumo ya siasa za kunifanya niseme hatuna matatizo kwenye uongozi wetu il-hali kumeoza.
Pundamilia
Nimerudia tena kusoma Maswali yako, na nimesoma tena Majibu yangu- na nimejiridhisha kwamba nilijibu Maswali yako yote uliyoyaibua. Na sijaona hoja yoyote uliyoitoa kudhirisha kwamba CHADEMA ni chama cha mabanyenye. Ukienda kule Karatu, Kigoma, Tarime nk ukasema maneno hayo; wananchi watakutazama tu- na ukaanza kuwaambia kwa CCM ndio chama cha watu, watakuangalia zaidi. Kumbuka wale mawaziri waziliozunguka ziarani kusema CCM na serikali yake zinajali wananchi waliowengi, kumbuka waliambulia majibu gani toka kwa wananchi.
Kuhusu Kingunge, mara ya kwanza nilipomuona ni kigeugeu ni wakati kabla sijaingia siasa- wakati huo nilikuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Dira ya Vijana(TYVA); bwana Kingunge alikuwa anajaribu kueleza jinsi gani ambavyo CCM ni chama cha ujamaa na kujitegemea- maelezo yake, wakati huo nikiwa sekondari- nimepata basic za kutofautisha kati ya uchumi wa soko; na uchumi wa dola kuhodhi njia za uzalishaji nk nilimshangaa sana. Lakini nilimshangaa zaidi kwa kuwa wakati nasoma shule ya msingi, huyu jamaa alionekana mbele yetu kama muumini mzuri wa misingi ya Nyerere. Kwa kweli toka siku hiyo, nikawa namwangalia kwa jicho tofauti kabisa.
Nikapata kituko kingine wakati wa uchaguzi mkuu 2005, alipokwenda maelezo kumsema Mbowe kuwa asimtaje Nyerere katika kampeni za CHADEMA- matokeo yake Wazee wenzake kama Profesa Baregu wakatoa kauli za kuonyesha kuwa amekuwa 'mtu mzima ovyo'.
Sasa mwaka 2007 ndipo nilipofunga ukurasa kabisa wa kumheshimu kama kiongozi(ingawa bado namheshimu kama ninavyoheshimu mtanzania mwenzangu yoyote mwingine); pale alipoibuka na kutetea ufisadi ambao leo umedhihirika. Nakumbuka wakati huo nilikuwa Arusha na tukatoa tamko lifuatalo:
TAMKO KUHUSU KAULI ZA KINGUNGE
Sisi, viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi
na TLP tuliokutana Equator Hotel tarehe 20 Septemba
2007 hapa Arusha tumeitafakari Orodha ya
Mafisadi(List of Shame) na tumejadili kauli za Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Siasa na Uhusiano wa
Jamii-Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru alizozitoa 18
Septemba 2007 na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya
habari Jumatano 19 Septemba 2007 na kwa pamoja
tumeazimia kutoa tamko lifuatalo:
Kingunge anapotosha umma, apuuzwe; wapinzani wanatetea
taifa
Tunaunga mkono uamuzi wa viongozi wetu wa kitaifa
kuanika wazi kwa umma orodha ya mafisadi; hii ni kwa
sababu rasilimali zinazofujwa ni za wananchi
watanzania, wanaoathirika kutokana na ufisadi ni umma
wa watanzania na wenye uamuzi wa mwisho wa
kuwawajibisha viongozi mafisadi ni umma wa watanzania.
Kwa kuzunguka nchini kueleza yaliyotokea bungeni(
hususani kusimamishwa kwa Mbunge Zitto Kabwe na
kupigwa danadana kwa hoja ya kashfa ya ufisadi ndani
ya Benki Kuu iliyokuwa iwasilishwe na Dr Wilbroad
Slaa) wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajeti
uliomalizika hivi karibuni, wabunge wa upinzani
wanatimiza wajibu wao kama wawakilishi wa kweli wa
wananchi. Kwa kuzunguka nchini kueleza kuhusu ufisadi
unaendelea nchini, viongozi wa upinzani wanatekeleza
wajibu wao wa kisiasa wa kuwazungumzia wananchi wote
wa Tanzania wanaoguswa na ufisadi bila kujali itikadi
ama uanachama; ikumbukwe kuwa vyama vya siasa sio
vyombo vya uchaguzi tu bali ni taasisi muhimu katika
jamii katika kuchochea uwajibikaji na maendeleo. Kwa
mantiki hiyo basi Waziri Kingunge anaupotosha umma
anaposema kwamba ziara za viongozi wa upinzani
zinatokana na hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005,
kambi ya upinzani kushindwa kumtetea Zitto bungeni,
wivu wa kuona CCM inatekeleza ilani yake vizuri, na
kwamba wanautumia vibaya mfumo wa vyama vingi.
Tunapenda kusisitiza kuwa Viongozi wa umma wanaokiuka
na/au kuvunja masharti ya katiba ya Jamhuri ya
Muungano na Sheria za Maadili ya Viongozi wa umma
lazima waanikwe hadharani na kuwajibishwa na yoyote
anayetoka kauli ya kubeza jitahada hizi ni vyema
watanzania wakampuuza. Kama viongozi wa upinzani
wanavunja sheria kwa kutoa uzushi na kufanya uchochezi
kama Waziri Kingunge anavyodai kwa nini serikali
haiwakamati na kuwapeleka mahakamani badala ya kutoa
matamko ya kulalamika?
Kauli za Kingunge ni msimamo wa Serikali?; Ikulu itoe
tamko!
Tumezijadili kauli za Waziri Kingunge na katika hatua
ya sasa tusingependa kuamini kama zinawakilisha
msimamo wa serikali kwa ujumla wake; hatutaki kuamini
kwamba kauli hizo ni msimamo wa pamoja wa Serikali
chini ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Mawaziri. Katika hatua ya sasa
tunazichukulia kauli hizo kuwa ni maoni binafsi ya
Bwana Kingunge mpaka hapo Ikulu itakapothibitisha
vinginevyo; hivyo kwa tamko hili tungependa ikulu itoe
ufafanuzi kuhusu kauli hizo. Lakini tunapenda pia
kutoa tahadhari kwamba inawezekana kauli hizi za Bwana
Kingunge amezitoa kwa nia ya kupoteza lengo tuanze
kuzijadili kauli zake badala ya kujadili orodha ya
mafisadi na hatma ya rasilimali za nchi yetu. Hivyo
tungependa kusisitiza kuwa ikulu ijibu hoja
zilizotolewa na viongozi wa upinzani ambazo zimemgusa
moja kwa moja Rais na serikali.
Anayelinda ufisadi ndiye anayekwamisha maendeleo na
huduma za kijamii
Tunashangazwa na uamuzi kauli ya Kingunge kwamba
uamuzi wa Viongozi wa Vyama na Wabunge wa Upinzani
kuzunguka nchini ni mkakati wa kisiasa wa kuitoa
serikali kwenye mstari wa kushughulikia maji, afya na
barabara. Tunapenda kumbukusha Waziri Kingunge kuwa
katika orodha hii ya mafisadi pekee zaidi ya shilingi
trilioni 1.3(1,300,000,000,000) ambazo kama
zingetumika vizuri ni wazi zingeweza kutumika
kuboresha maji, umeme na barabara bila kuendelea
kuwakamua zaidi wananchi masikini. Ukweli ni kuwa kwa
kuendelea kulea ufisadi serikali inajitoa yenyewe
kwenye mstari wa kutumia vyema kodi za wananchi na
rasilimali za taifa katika kushughulikia shughuli za
maendeleo na huduma za kijamii ikiwemo maji, afya na
barabara. Ni ukweli pia kwamba kwa kuwawajibisha
mafisadi viongozi wa upinzani wanatimiza wajibu wao wa
kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa ustawi
wa wananchi walio wengi.
Vyombo vya dola tayari vinayo orodha ya mafisadi;
vichukue hatua
Tunashangazwa na kauli ya Waziri Kingunge ya kuhoji
sababu za Viongozi wa Upinzani kushindwa kuziwasilisha
kwenye vyombo vya dola tuhuma walizozitoa dhidi ya
vigogo hao iwapo kweli wanao ushahidi wa
kuzithibitisha. Tunashangazwa na kauli hii kwa kuwa
tunaamini kabisa Waziri Kingunge anafahamu kabisa kuwa
sehemu kubwa ya tuhuma hizi zipo katika Ripoti za
Mkaguzi wa Serikali ikiwemo ile ya mwaka 2005/06 na
kwamba vyombo vya dola vinafahamu uwepo wa tuhuma hizi
lakini kwa zaidi ya miaka miwili vyombo hivyo
havijachukua hatua dhidi ya vigogo waliotajwa.
Tunaamini kwamba viongozi wa upinzani walichofanya ni
kuamua kushtaki kwa wenye mali walioibiwa ambao ni
wananchi wote wa Tanzania ili kwa pamoja tuweze
kuvitaka vyombo vya dola viweze kuchukua hatua.
Tunashangazwa na kauli hii ya Waziri Kingunge ya
kuwahukumu viongozi wa upinzani kwa kushindwa
kupeleka ushahidi kwa kuwa kauli hii inapingana na
kauli zingine ambazo zimewahi kutolewa na viongozi wa
serikali kuhusu tuhuma hizo hizo. Tunapenda
kumkumbusha Waziri Kingunge kwamba tayari Spika Wa
Bunge-Samuel Sitta alishasema kwamba anavipeleka
polisi vielelezo vyote vya ushahidi alivyotoa Dr Slaa
ili vichunguzwe. Pengine Kingunge angetoa hukumu hiyo
kwa Spika kwa kushindwa kupeleka vielelezo. Pia
ikumbukwe kwamba ni serikali hiyo hiyo iliyowahi kutoa
taarifa kwa umma kwamba tuhuma za ufisadi ikiwemo za
BOT zinachunguzwa na TAKUKURU. Kadhalika Waziri
Mkuu-Edward Lowasa alitoa kauli baadaye kwamba
Serikali iliyafahamu madai ya Kashfa ya ufisadi Benki
Kuu(BOT) kabla ya upinzani. Kwa upande mwingine, madai
ya kutaka kushughulikia rushwa kubwa kubwa ikiwemo za
kwenye mikataba yalianza kutolewa na Rais Kikwete
wakati akifungua Mkutano wa Kwanza kabisa wa Bunge
mwaka 2005. Lakini baadaye ni Rais Kikwete alinukuliwa
na vyombo vya habari akisema kwamba anawafahamu wala
rushwa na anawapa muda wajirekebishe; tulitarajia
Waziri Kingunge kama mshauri wa Rais wa masuala ya
siasa angemshauri apeleke ushahidi katika vyombo vya
dola na si kuwahukumu viongozi wa upinzani ambao
wametoa orodha ya mafisadi na ushahidi kutoka kwenye
taasisi za serikali yenyewe!. Na ni jukumu la vyombo
vya dola kuchukua hatua za kufuatilia baada ya orodha
ya mafisadi kuwekwa hadharani.
TAKUKURU inajipotezea imani yenyewe!
Tumeshangazwa pia na kauli ya Waziri Kingunge ya
kuwalaumu viongozi wa upinzani kwa kutokuwa na imani
na TAKUKURU. Kwa misingi ya kauli zao ambazo wamezitoa
katika nyakati mbalimbali, viongozi wa upinzani
wamekuwa wakikisisitiza kuwa TAKUKURU inajipotezea
yenyewe imani kwa wananchi kutokana na taarifa zake na
kwamba wamekuwa wakiipa changamoto TAKUKURU kuchukua
hatua. Mathalani TAKURU kuisafisha kampuni ya
RICHMOND.
.hakuna ushahidi wowote uliopatikana
kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wa
kamisheni watendaji wa serikali
.uchunguzi huo
umethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji na
ambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote
ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara
iliyosababishwa na udhaifu huo(Mwananchi 12/5/2007).
.baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamu
mwenendo wa mambo serikalini
(Tanzania Daima
12/5/2007). Maswali yaliyobaki mpaka hivi sasa ambayo
si TAKURU wala TAKUKURU ya sasa hawajayajibu ni pamoja
na: Ni kwanini Kamati ya Waziri Mkuu iliipa tenda
Richmond baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco
kuitaka bodi yake ya sabuni kutangaza upya zabuni hiyo
kwa kutimia zabuni za kimataifa? Richmond kuweza
kufahamu mwenendo wa mambo ya ndani serikalini sio
ishara ya rushwa ya kimadaraka? Ni kweli kama hakuna
hasara iliyosababishwa na uamuzi huu wakati ambapo
watanzania wamekaa bila umeme kwa miezi mingi bila
kupata umeme wa dharura waliotarajia wakati wa
dharura, Rais amekiri kwamba umeme ulichangia kushuka
kwa kasi ya ukuaji wa uchumi na hata kuongeza mfumuko
wa bei na mpaka leo bado megawatts 100 hazijatimizwa
na Richmond/Dowans? Tunapenda kumkumbusha Waziri
Kingunge kwamba Mkataba wa Richmond/Dowans pekee
umeligharimu taifa zaidi ya Bilioni 200 mpaka sasa
ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye elimu, afya na
barabara. Viongozi wa upinzani wanapohoji utendaji wa
TAKUKURU wanataka ichukue hatua za haraka
kushughulikia mafisadi na kuendelea kuwa Taasisi ya
Kuzuia na Kudhibiti Rushwa na si Taasisi ya Kulinda,
Kusafisha ama Kutetea Rushwa !
Wasomi na asasi za kijamii wako sahihi; Kingunge
amelewa madaraka
Tumefadhaishwa na kauli ya Waziri Kingunge kwamba
wasomi nchini wametathimini uamuzi wa Bunge wa
kumsimamisha Mbunge Zitto Kabwe kwa kutanguliza jazba
badala ya busara na kutilia wasiwasi uelewa wa makundi
ya kijamii kuhusu mantiki ya uzalendo. Hatutaki
kuamini katika hatua ya sasa kwamba huu ni msimamo wa
serikali kwamba wasomi na makundi ya kijamii
wametanguliza jazba na kukosa busara na uelewa katika
kuijadili adhabu aliyopewa Mbunge Zitto Kabwe na hoja
yake ya kutetea Rasilimali za nchi yetu hususani
madini. Tunaamini kwamba kauli hii ni maoni binafsi ya
Bwana Kingunge ambayo ni ishara ya kulewa madaraka
kutokana kungangania serikalini toka wakati nchi hii
inapata uhuru kwani hii si mara ya kwanza kutoa kauli
za kubeza-aliwahi kuibeza CHADEMA kwa kumtaja Nyerere
kwenye kampeni 2005 na hivi karibuni Julai 3, 2007
aliripotiwa na vyombo vya habari akitetea msimamo wa
Rais Kikwete wa kutumia nafasi yake kama rais
kudhoofisha upinzani kwa kufanya kampeni za CCM katika
mikutano ya kiserikali. Tunapenda kumbukusha Waziri
Kingunge maneno ya Shaban Robert kwamba elimu
ilipokuwa bado kujulikana mvi zilihesabika kuwa alama
ya hekima lakini fikra hizo wakati wake umeshapita
haupo na wala hauji tena. Kisichobadilika ni kwamba
mtu mzima bado anastahili heshima kutoka kwa mdogo .
Ni vyema Waziri Kingunge akafahamu kwamba wasomi kama
Profesa Issa Shivji na makundi ya Kijamii mathalani
Mtandano wa Jinsia(TGNP), Chama cha Wanasheria wa
Mazingira(LEAT), Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu(LHRC) walifanya tathmini yao kwa lengo la
kulinda maslahi ya taifa bila kujali itikadi.
Mafisadi zaidi waendelee kutajwa; serikali ijibu hoja
Hivyo tunapongeza na tutaendelea kuunga mkono jitahada
zote za vyama vya siasa, asasi za kijamii na hata watu
binafsi waliowataja na watakaoendelea kuwataja
viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au
washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna
mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au
fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa
Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa. Kadhalika
tunaunga mkono na kutoa mwito kwa vyama vya siasa,
asasi za kijamii na hata watu binafsi kuendelea
kuwawajibisha viongozi wa umma ambao kwa kutumia
nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma
wamefanya maamuzi ambayo yamesababisha taifa
limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na
kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za
kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma
walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika
sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine
yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya
Watanzania. Na katika haya tunataka serikali ijibu
hoja na si kupuuzia na kutoa kauli za kejeli kama "hao
ni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki ya
kutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" .
Waziri Kingunge na serikali kumbukeni kuwa watu
wachache wanaweza kudanganyika katika muda mchache
lakini watu wote hawewezi kudanganywa wakati wote.
Watanzania wa leo na kesho si watanzania wa jana na
juzi.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa (CHADEMA)
Na Mwenyekiti wa Kikao
Godbless Lema
Katibu Mwenezi Mkoa-Arusha(TLP)
Na Msemaji wa Ushirikiano wa Vyama vya Upinzani-Arusha
Mohamed Maabad
Mwenyekiti wa Wilaya-Arusha Mjini(CUF)
Na Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Vyama vya
Upinzani-Arusha
Ened Muro
Mwakilishi-Arusha(NCCR-Mageuzi)
Amos Kibanda
Katibu Mkoa-Arusha(CHADEMA)
Calist Lazaro
Mwenyekiti wa wilaya-Arusha Mjini (TLP)
Kwa hiyo ukitafakari haya yote, utagundua kwamba katika Wazee wanaostahili kutukuzwa kwa mchango wao kwa taifa bila kujali itikadi Kingunge hapaswi kuwepo- alikuwa na heshima nzuri tu kama kiongozi katika enzi za mwanzo za utumishi wake; amejiharibia na kujichafua! Neno Kingunge sasa ni synonimous na ukinganganizi wa madaraka kwa gharama yoyote na kwa njia zozote hata kwa kufanya siasa chafu!
JJ