Naona kuwa njia moja kubwa ya kutafuta ushindi kwa upande wa CHADEMA ilikuwa ni helikopta. Yaani waTanzania wamekuwa mbumbumbu kiasi cha kuweza kudanganywa na helikopta? Laiti chadema wangeelekeza nguvu zao kwingine zaidi ya kutegemea helikopta labda matokeo yangekuwa kwingine. Nikimaanisha kuwa, CHADEMA ingewekeza katika kuonyesha maendeleo yepi na kwa mifano si kwa maneno na kabla ya kukurupuka na helikopta dakika za mwisho wakitegemea kuwa, kwa kuwa wanazunguka na helikopta basi ndio chombo cha kuwaletea ushindi. Inashangaza sana, kwani sidhani kama waliona kuwa wanaojazana kwenda kuilaki helikopta ni watoto na wengi si wapiga kura. Na isitoshe hata yaongewayo na huyo aliekuja na helikopta hawayasikilizi, wao huwa wako na issue ya helikopta. Si "washamba" wa helikopta?
Na hili la rigging tumelisikia miaka nenda miaka rudi, linakuwa kama nyimbo. Mimi nauliza hivi, hivi nyumbani kwako kila siku unaibiwa na kudhulumiwa na wewe unapiga kelele tu baada ya kudhulumiwa na kuibiwa miaka yote, huchukuwi preventive security measures? au unategemea "ngoja wamalize kuiba nipate ushahidi"? nashindwa kuelewa.
Kama mambo yenyewe ndio hayo, kitaeleweka tu.
Me, I have a big feeling kuwa most ya viongozi wa CHADEMA si CHADEMA kweli na bado ni wale wale system. Wanadanganya wananchi tu.
Mtaalamu mwingine wa propaganda na kuhamisha mijadala. We unajua kuwa CHADEMA imetumia helikopta siku mbili za mwisho za Kampeni; siku zingine zote 19 fedha zilielekezwa kwenye mikakati mingine ya kampeni chini kwa chini. Helikopta ambayo iliwapa kiwewe CCM mpaka nao wakakimbilia kukodi helikopta, lakini kwa bahati mbaya CCM walikuwa wakizomewa na helikopta yao
Viongozi gani wa CHADEMA hao ambao bado ni system? Au ni mkakati mwingine wa kuwatia hofu wananchi wasiwaamini viongozi wao?-Wagawe uwatawale.
Kwa kiteto tumefanya preventive measures nyingi sana ndio maana umeona tumepata hayo maelfu ya kura- in fact, watanzania wanapaswa kumpongeza Kimesera kwa kupata kura zote hizo katika mazingira kama hayo ya uchaguzi. Ni kama timu ambayo, mpinzani wako refa wake, washabiki kila mtu uwanjani, isipokuwa wachezaji wako tu. Ukifungwa mbili kwa moja tena kwa goli la kuotea, unastahili pongezi kwa kweli.
Sasa CHADEMA tunafanya nini ili kuzuia hali hizo wakati ujao; Soma Msimamo wetu hapa ambao ni sehemu ya hilo tamko.
Msimamo wa CHADEMA kuhusu mchakato mzima wa Uchaguzi
Kufuatia mwenendo mzima wa uchaguzi Kiteto na Mwelekeo wa Taifa kwa ujumla CHADEMA tunachukua hatua zifuatazo;
Kuhusu Viongozi waliopigwa
Tunaitaka serikali ifikishe suala hili mahakamani haraka iwezekanavyo. Na endapo watachelewa tutaisimamia wenyewe.
Na kwa kuwa IGP Said Mwema alitangaza kuunda kikosi cha uchunguzi wa kadhia hii tunamtaka aweke wazi matokeo ya tume aliyounda kufuatia vurugu na kupigwa kwa viongozi wa CHADEMA. Hasa kwa kuwa moja ya silaha zilizotumiwa ni kemikali ambayo mpaka sasa haijajulikana.
Lakini pia tunasikitika kwamba mpaka sasa wadau wa Demokrasia nchini kama wanaharakati wa haki za binadamu, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wameonekana kutojali unyama waliofanyiwa viongozi wa CHADEMA , unyama ambao unaweza kupelekea machafuko ya kisiasa katika nchi yetu.
Kuhusu CCM kuvamia mikutano ya CHADEMA
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania kuwa tumekwisha fungua kesi polisi Kijungu na mpaka sasa hatujui polisi inasubiri nini kumkamata Mkurugenzi wa TOT, Mh Komba. Lakini zaidi tunashangaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijaeleza lolote kuhusu uvunjaji wa taratibu za uchaguzi wa makusudi kwa kiwango hiki. Tunaitaka serikali ichukue hatua haraka kabla hatujachukua hatua wenyewe kwakuwa hatuwezi kukubali suala hili liishe kirahisi. Tunavipongeza vyombo vya habari kwa namna walivyolipa uzito suala hili.
Matumizi ya fedha za Kampeni
CHADEMA tumekuwa na utamaduni wa kuweka waazi matumizi yetu ya fedha za kampeni kwa lengo la kushinikiza mfumo wazi wa matumizi ya fedha za kampeni.
Tunarudia tena kuitaka serikali kutunga sheria ya lazima kuwepo mipaka ya matumizi ya fedha katika kampeni na uwazi katika matumizi ya fedha za kampeni. Ufisadi unaoliangamiza taifa hili ni matokeo ya matumizi makubwa ya fedha katika kampeni kiasi cha kusababisha pesa kushinda sera katika uchaguzi.
Kwa msingi huo tunapenda kuwataarifu watanzania kuwa CHADEMA katika uchaguzi huu tumetumia shilingi milioni 48, milioni 15 ikiwa ni mchango wa chama na milioni 33 ikiwa ni michango ya wanachama. Lakini kwa taarifa tulizonazo, CCM imetumia zaidi ya bilioni 1 katika uchaguzi mdogo wa Kiteto huku sehemu kubwa ikitumika kutoa rushwa. Kwa mfano; CCM ilimnunua kijana Omari wa kata ya Matuti kwa shilingi milioni 2. Na ikamlipa Mwenyekiti wa CHADEMA kijiji cha mbigiri baiskeli na shilingi laki 5 ili aingie CCM. Wakati huo huo ilikuwa na magari si chini ya 50, pikipiki, na walikuja na fuso imejaa baiskeli mpya.
Kuhusu TAKUKURU
Kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya kampeni hizi ziligubikwa na vitendo vya rushwa na baadhi ya matukio ya utoaji rushwa yalifanywa na viongozi wa CCM na serikali kwenye mikutano ya hadhara na tukayafikisha TAKUKURU. Tunaitaka TAKUKURU itoe taarifa imefikia wapi kuhusu uchuguzi wake kwa uchaguzi wa kiteto mapema iwezekanavyo.
Kuhusu Sheria ya Uchaguzi
Kwa kuzingatia mwenendo wa sasa ambapo kampeni chafu zinafanywa kutumia umasikini wa wananchi kuwanyima haki yao ya kupiga kura kwa mradi wa kununua shahada za kupigia kura, CHADEMA tutahamasisha Umma Sheria itungwe kuhakikisha kuwa kupiga kura ni lazima, na kwakuwa kinachofanyika sasa ni kuzuia watu wasipige kura kwa kununua shahada zao, CHADEMA hatuoni sababu ya kwamba ili mtu apige kura ni lazima awe na shahada. Tunataka mabadiliko ya sheria ili kupiga kura kutokane na mtu kuwemo kwenye daftari la wapiga kura tu. Na kwamba wasio jua kusoma na kuandika wapige kura za wazi ili kudhibiti tatizo la kutumia fursa ya wasio jua kusoma kupoka haki zao za kikatiba za kuchagua kiongozi wanaye mtaka.
Kuhusu Tume Huru
Mwisho tunapenda kurejea Rai yetu kwa serikali kuhusu Tume huru ya Uchaguzi kwa uchaguzi mkuu na ule wa serikali za mtaa. Tunajua serikali na CCM inafaidika na mfumo mbovu tulionao ndio maana haitaki kutekeleza hoja hii. CHADEMA inatangaza rasmi kuwa mwaka huu ni mwaka wa Madai ya tume huru ya uchaguzi. Tutatumia kila mbinu kuishinikiza serikali kuunda tume huru ya Uchaguzi, na kwa kuanzia tumewaelekeza wanasheria wetu kuanza mchakato wa kufungua kesi mahakani. Watendaji wa serikali wasiwe sehemu ya tume. Tunataka mfumo mzima urekebishwe. Tutafungua kesi ya kikatiba kudai tume huru ya uchaguzi.
Imesainiwa na;
Jafari Kasisiko-Mwenyekiti Mkoa wa Kigoma
Kny; Kamati ya Kampeni
Machi 1, 2008.
Kwa herini, mpaka wakati mwingine
JJ