Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Tunawapongeza CCM kwa kushinda hicho kiti pia tunawapongeza CHADEMA kukubali matokeo. Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Kama mlivyozunguka wakati wa Zito sasa muanze mapema. Ushindi upo lakini kwa kazi na si katika sahani. Tujenge nchi yetu kwa kuongeza nguvu kwa upinzani CCM kujisahihisha ni kini macho.

Mkuu Msavila,

Heshima mbele, maneno yako ni mazito sana na ndio maneno ya maendeleo kwa taifa, upinzani wasiakate tamaa na sisi CCM tusibweteke bali tuonyeshe kuwa we deserve kushinda, na kama kuna matatizo yetu ya kawaida kwenye chaguzi za Afrika, yalikuwepo yashughulikiwe ili yasirudiwe tena, bado majimbo mawili Mwibara, na Biharamulo, kwa hiyo one down, two to go, tuendelee na kampeni za uchaguzi zaidi,

Isipokuwa hongera CCM kwa ushindi huu, na pia Chadema/upinzani kwa kukubali kushindwa bila matatizo, sasa tusonge mbele ndio siasa za ki-utu uzima.

Lakini naomba kuuliza hivi si nilisikia kuwa upinzani wameweka mgombea mmoja au?
 
CCM haihitaji kupewa hongera! Hongera kwa lipi walilofanya? Tusipokuwa na tabia ya kuwaadhibu wanasiasa wa vyama ambavyo vinawadharau wapiga kura basi ni bora tunyamaze tu! hatuna haja ya kulalama kwamba maisha magumu, kashfa nzito nzito kila kukicha n.k.. Kwa nini tulalamike wakati tukipewa nafasi ya kuwaadhibu wale wanaotudharau wapiga kura, wale wanaoficha ukweli wa mambo ndani ya serikali, wale ambao wanakuwa mabilionea wakati asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi maisha ya dhiki kubwa ndio hao hao tunawachagua tena na tena na tena!

Eti CCM nambari one! CCM nambari wani kwa lipi hasa? Labda nambari wani kwa kuwaruhusu wageni wanufaike na rasilimali zetu wakati sisi wenyewe hatuoni mafanikio yoyote ya rasilimali hizo. Nambari wani kwa kuingamiza Tanzania. Leo hii bei ya umeme imepanda kwa kasi kubwa sana na wahusika waliosaini mikataba ya IPTL, Richmond, songo songo, Net group ni hao hao CCM ambao kila kukicha wanasaini mikataba isiyo na maslahi kwa nchi yetu. Ni hao hao CCM waliosaini mikataba ya madini ambayo haina maslahi yoyote kwa Watanzania.

Tumesikia kashfa nzito za BoT, EPA, KCM, Rada n.k. lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyekamatwa au kufilisiwa mali zake. Pamoja na balozi wa Marekani kwa niaba ya nchi yake kusema hadharani kwamba nchi yake ipo tayari kuisadia Tanzania kumrudisha Balalli nchini ili akajibu tuhuma mbali mbali za BoT dhidi yake, hadi leo hii hakujatamkwa chochote cha kufuatilia msaada huo uliotolewa na Marekani, lakini inapotokea nafasi ya kuonyesha hasira zetu dhidi ya CCM tunaimba CCM ni nambari wani na kuwarudisha tena bungeni ambako wanachapa usingizi tu huku wageni wakitajirika na rasilimali zetu!

Ndugu zangu sasa ni wakati wa kuweka pembeni itikadi zetu na kuweka mbele maslahi ya Tanzania bila kujali wewe ni wa chama kipi. Haya mambo ya kutoa pongezi zisizostahili hayaisadii Tanzania yetu bali yanazidi kuiangamiza maana CCM hawakustahili kabisa kushinda uchaguzi wa Kiteto kutokana na kashfa mbali mbali zenye uzito wa hali ya juu. Kutoa pongezi pamoja na ufisadi mkubwa unaoendelea ndani ya nchi yetu nao ni aina ya ufisadi.

Tukiwa tunatoa hongera za kushinda uchaguzi bila kuchanganua kama CCM ilistahili kushinda basi tunawapa makucha mafisadi waendelee na ufisadi wao. Maana CCM watasema tizama haya manunga nyembe tumegubikwa na kashfa chungu nzima tena zenye uzito wa hali ya juu lakini bado yametuchagua! Hivyo hata tuvurunde namna gani haya manunga nyembe yatapita huku na kule na kuimba CCM ni nambari wani na kutuchagua tena! Kama kweli mnaipenda Tanzania kwa mapenzi ya dhati na kuitakia Tanzania na wananchi wake mema, basi sasa hivi sio wakati wa kutoa pongezi bali ni wakati wa kusononeka na kujiuliza kulikoni!
 
NAOMBA UELEWE KUWA WANANCHI WA KITETO WALIKUWA WANAMCHAGUA MBUNGE ATAKAYE WAWAKILISHA BUNGENI, HIZO KASHFA UNAZOZISEMA WANAZIFAHAMU SANA TU.
WALICHOFANYA NI KUMCHAGUA MTU AMBAYE ATAWAWAKILISHA VEMA BUNGENI NA SI VINGINEVYO. KUMBUKA WANANCHI WA KITETO SI MBUMBUMBU KAMA UNAVYODHANI.

MZEE WANGU KIMESERA WANAKITETO WALISHAMKATAA SIKU NYINGI TU NA ALIKWENDA KWENYE UCHAGUZI AKIJUA KABISA HUKUMU YAKE ILISHAPITISHWA SIKU NYINGI.

KAMA NILIVYOSEMA HAPO AWALI KIMESERA
WAS NOT THE BEST CANDIDATE BUT JUST A CANDIDATE.

Kimesera kakataliwa...lipi alilofanya hadi akataliwe! haijulikani!

CCM pamoja na kashfa kibao za BoT, rada, Magari ya jeshi, Richmond, Mkapa gate lakini bado inakubalika kwa wapiga kura! Maskini Tanzania wacha tuendelee kuwa maskini wakati wageni na mafisadi wachache wakineemeka kupitia migongo yetu. Wananchi walizijua kashfa za CCM lakini bado wakaona umuhimu wa kuwachagua tena CCM! Halafu mnakuwa mstari wa mbele kulalama ugumu wa maisha unaongezeka kila kukicha!
 
nnashindwa kuelewa pale upinzani unaposhindwa kuheshumu matashi ya wananchi na kuwafanya wapuuzi wajinga na wavivu wa kufikiri.

kigoma mjini? mbona wananchi waliwapa upinzani, pemba matajiri ? mbona wamewapa upinzani?

jee huko CCM haijagawa kanga ? acheni hizo za kuwadharau.

CCM wamesimama vizuri na hata bungeni mbali ya kuwa serikali ni ya CCM wanaibana kuona uwajibikaji unakuwepo.

au Mwakyembe upinzani na baaadhi ya member? tuwe wakweli wenye kufatilia habari za bunge jee CCM haisimamii mahitaji ya majimbo yao?

wananchi wanayajua yote hayo.

wajipange watani na maneno yao hayo wayaache au tutayatumia kuwamaliza kabisa.

tunatamani upinzani imara utusaidie ktk kujenga nchi ila kwa masikitiko ni wachache walio makini
 
Kama sio wapinzani kupiga kelele bungeni kuhusiana na kashfa za BoT na hatimaye nchi wafadhili zikiwemo US, Canada, Holland, UK n.k. kuishinikiza serikali kuhusiana na kashfa nzito ya BoT hiyo tume ya Mwakyembe ingeundwa!? Acha hizo!

CCM walishapinga kwamba ndani ya BoT hakuna tuhuma zozote bali ni wapinzani kutafuta umaarufu wasiokuwa nao na Balalli akatamka mbele ya kadamnasi kwamba, "sijiuzulu ng'o" maana hakuna tuhuma zozote ndani ya BoT, au umesahau!?

Duh! watu bwana mnajifanya mmeshasahau ukweli wa mambo ulivyokuwa, leo mnaipigia debe CCM inasafisha mambo siyo tena wapinzani waliopiga kelele kila kona na hadi nchi za wafadhili baada ya kusoma kashfa hizo katika magazeti mbali mbali hasa THIS DAY kuzivalia njuga kashfa hizo. Au mnasahau usemi wa Sitta kupeleka ushahidi polisi ili wakachunguze na hatimaye kumfungulia mashtaka Slaa kwa kusema uongo kuhusiana na tuhuma za BoT?
 
Jamani:

Naomba tutofautishe ushabiki wa burudani za michezo (Simba/Yanga) na siasa.

Siasa ni maisha yako ya kila siku. CCM kisiwe chama cha mapenzi kama klabu ya mpira. Na mtaji huo ni kwa vyama vingine vya siasa.

Mbunge wa Tanzania analipwa zaidi ya dollar 2000 kwa mwezi na kila siku anatumia zaidi ya kima cha chini cha mfanyakazi wa Tanzania. Na kipindi chake cha uchaguzi kikiisha analipwa mafao makubwa kuliko mafao ya professor wa chuo kikuu.

Inaonekana watu mnashangilia jezi wanazovaa wabunge lakini sio kazi zao.
 
Tukiwa tunatoa hongera za kushinda uchaguzi bila kuchanganua kama CCM ilistahili kushinda basi tunawapa makucha mafisadi waendelee na ufisadi wao. Maana CCM watasema tizama haya manunga nyembe tumegubikwa na kashfa chungu nzima tena zenye uzito wa hali ya juu lakini bado yametuchagua!

Mkuu Bubu,

Heshima mbele, CCM sio chama cha mafisadi, isipokuwa kuna baadhi ya viongozi ambao ni mafisadi, sasa haitufanyi wote tuwe mafisadi, Mwakyembe sio fisadi, Seleli sio fisadi, Mama Kilango, sio fisadi na wote ni kutoka CCM, sio cuf, kwa hiyo wananchi wanaelewa hilo na wamethibitisha kwa kura zao walizozipiga, tunasema kuwa tuna matatizo mengi mojawapo ikiwa la viongozi wabovu wachache, lakini sio CCM nzima yenye tatizo, asilimia kubwa tuko clean, inagwa pia mkuu i get your point, lakini tu tatizo unaielekezea to the wrong people.
 
Mbunge wa Tanzania analipwa zaidi ya dollar 2000 kwa mwezi na kila siku anatumia zaidi ya kima cha chini cha mfanyakazi wa Tanzania. Na kipindi chake cha uchaguzi kikiisha analipwa mafao makubwa kuliko mafao ya professor wa chuo kikuu.

Mkuu haya mafao hulipwa kwa pande zote mbili, sio wabunge wa CCM tu, kama kuna tatizo kwenye hili, basi tungesikia wabunge wa opposition wakikataa hela na mashangingi, wabunge wetu ni lazima walipwe vizuri ili kuwaepusha kuingia taamaa za kurubuniwa na mafisadi.
 
Jamani:

Naomba tutofautishe ushabiki wa burudani za michezo (Simba/Yanga) na siasa.

Siasa ni maisha yako ya kila siku. CCM kisiwe chama cha mapenzi kama klabu ya mpira. Na mtaji huo ni kwa vyama vingine vya siasa.

Mbunge wa Tanzania analipwa zaidi ya dollar 2000 kwa mwezi na kila siku anatumia zaidi ya kima cha chini cha mfanyakazi wa Tanzania. Na kipindi chake cha uchaguzi kikiisha analipwa mafao makubwa kuliko mafao ya professor wa chuo kikuu.

Inaonekana watu mnashangilia jezi wanazovaa wabunge lakini sio kazi zao.

Na hili ndio litaiangamiza Tanzania. Hospitali zetu hazina vitanda, madawa hakuna, madaktari wanaondoka kwenda nchi ambazo wanalipwa mishahara mizuri, barabara zetu nyingi bado ziko katika hali mbaya, ajira kwa wananchi wengi hakuna, hawa wenye ajira mishahara ni midogo mno tunasaini mikataba ya madini yetu na kuambulia asilimia tatu tu na wageni kuchukua 97% mikataba inafanywa siri kwa wenye rasilimali zao! Viongozi wanatumia nyadhifa zao kuwa mabilionea na kuwakashifu Watanzania kwamba tumejawa wivu na wavivu wa kufikiri, kashfa nzito nzito za mabilioni ya pesa kila tukiamka.

Vyote hivi ni sababu nzuri ya kuwaadhibu CCM kwenye chaguzi, lakini bado wanashinda! halafu Watanzania bila hata kujua wanachopongeza kufuatia ushindi wa CCM wanaibuka na kutoa pongezi ukiwauliza mnawapa pongezi CCM kwa ushindi wao kwa lipi hasa walilolifanya la kustahili pongezi? wana'ngaa macho!

Kwa kweli inasikitisha sana. Mwalimu alitamka CCM sio mama yake na aliwahi kutamka kwamba CCM kumejaa wahuni wenye uroho wa utajiri, labda angekuwa hai angesaidia kuwafumbua macho Watanzania walio wengi ambao wanapiga kura hata bila kutafakari kwa nini wanapiga kura! Kwao wao CCM siku zote ni nambari one! hata ifanye madudu ya namna gani bado tu ni nambari wani! Mungu isaidie Tanzania!
 
Mkuu Bubu,

Heshima mbele, CCM sio chama cha mafisadi, isipokuwa kuna baadhi ya viongozi ambao ni mafisadi, sasa haitufanyi wote tuwe mafisadi, Mwakyembe sio fisadi, Seleli sio fisadi, Mama Kilango, sio fisadi na wote ni kutoka CCM, sio cuf, kwa hiyo wananchi wanaelewa hilo na wamethibitisha kwa kura zao walizozipiga, tunasema kuwa tuna matatizo mengi mojawapo ikiwa la viongozi wabovu wachache, lakini sio CCM nzima yenye tatizo, asilimia kubwa tuko clean, inagwa pia mkuu i get your point, lakini tu tatizo unaielekezea to the wrong people.

Mkuu asilimia kubwa pamoja na kuwa mko clean lakini hamna sauti ya kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CCM. Sauti zenu zimezimwa na mafisadi ndani ya CCM. Hivi ni wana CCM wangapi wanafurahia hizi kashfa nzito nzito karibu katika kila kona ya serikali? Hao wote uliowataja hawana sauti ndani ya CCM au bunge la CCM, ndio maana Lowassa alipowaambia kwamba wasihoji mkataba wa Richmond nao wakamtii bila kutia neno! huo ndio ukweli wa mambo. Mafisadi ni wachache lakini ndio wameiweka CCM mifukoni mwao na kuonekana ni chama cha mafisadi.
 
kweli sie ni wadanganyika haswa na sio watanzania kwani pamoja na uelewa wetubado tumelalia vyombo vya habari kwani vyama vya upinzani vimezidi kuwa butu. hivi ni nini hasa kinawashinda hawa wapinzani since we have so called fredom of speech kutumia vyombo vya redio na magazeti kutangaza kifo cha Chama cha mafisadi badala ya kuachia magazeti yakaandika mambo ya ngono na kufumaniwa na wingi wa ujinga.............well wadanganyika wenzangu inasikitisha jinsi gani tunavyo geuzwa malofa na hawa dhulumati ccm kwani wenzetu wa vijijini ambao wanajuwa bado mchonga ni rais......yaaani sijuwi niandikeje kwani ni hasira na aibu .anyway MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WADANGANYIKA WAKE.
 
Nakubaliana nawe asilimia 100.Dae Es Salaam watch your language.Hukatazwi kushangalia CCM lakini hapa si mahala pa kufanya mambo ya muhimu kama mpira wa miguu.Siasa hizi zinagusa maisha ya watu kabisa na si kuleta kejeli za JK kuwaita wapinzani watani wa jadi .This I find it always low .Siasa si kama mnavyo taka tuelewe.Tuongee issue hii bila kuonyesha kwamba jambo la mzaha tu.Hakuna mzaha hapa maana wana siasa ndiyo wanao amaua Watanzania wa Kiteto na kwingineko waishi vipi kwa hali .Kushindwa kupo na kushinda kupo.Lakini ningalikuwa wewe nisingaliweza kushangalia ushindi ambao hata damu za watu zimemwagika , Serikali na polisi wameingilia ka ku force ushindi .Mkuu wa Mkoa Shekifu alikuwa huko muda na yule mwingine toka Iringa nk .Tunajua CCM walitaka hili jambo to foos us kwamba wanakubalika .Kama wanakubalika basi wabadilishe vipengele vya katiba na hatimaye Tume ya Uchaguzi iwe na watu wote maana wa serikali wameshindwa kuwa wakweli bali kuibeba CCM sawa na Polisi na wengine wote .

Komba kafanya vurugu za wazi kabisa hajachukuliwa hatua hata moja lakini angalifanya Slaa ama Zitto ungalisikia matangazo na kipigo na kesi Mahakamani.Bado una akili timamu unataka kuleta suhabiki ? You can do this lakini nenda kule Tazama, IPP Media, Rai nk .

Tunakubalia Chadema kushindwa lakini isiwe ushabiki wa kijinga na kutufanya kjuongea kama sisi wote ni wapuuzi no .

Lunyungu unakisa na Dar? una-quote mwingine unamtaja Dar, kulikoni?
 
kushindwa kwa wapinzani kwenye majimbo tofauti kunatokana na ueleo mdogo wa wananchi, na hii inatokana na kuwa Tanzania ni kubwa na vyama vya upinzan havina pesa ya kutosha kufika sehemu zote za vijijini pia kuelimisha wananchi.
ukiona pemba majimbo yote yanachukuliwa na upinzani ni kwa sababu, upinzani umepiga kambi kule pemba, na kila mwananchi tayari ameshaelimishwa na ameelimika vya kutosha kujua jinsi ya kupiga kura.
kwa hali inavyokwenda, wapinzani wana hali ngumu kushinda majimbo ya vijijini kwa sasa, na wanachoweza kufanya ni kuhakikisha wanachukua majimbo yote ya mijini kwenye uchaguzi ujao.
 
Nakubaliana na wewe, bado elimu ya uraia ni ndogo vijijini na watu wanatishwa na yanayotokea kwa majirani, tumesikia pcha za machafuko ya Kenya zimetumika pia.
Pili wapinzanzani nao wanapaswa kuwapa moyo watanzania hao kuwa wanaweza wapo walioprove wrong!! kuna vichwa kama akina Zito na wenzie ni wazi bado pia siasa zetu ni kushabikia Chama na sio juhudi au uwezo wa mtu ni pale tu mtu huyo napoweza kuwa shujaa wa kujieleza na watu wakamuelewa.

Wabillah Tawfiq
 
Ndugu Watanzania;

Naomba kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA.

Tukumbuke hiki chama kilionekana kama chama cha tatu kwenye uchaguzi wa 2005; sasa hivi asilimia kubwa ya Watanzania Bara wanaamini kabisa kwamba upinzani wa kweli uko CHADEMA; Lazima tukubali kwamba pamoja na kwamba kura hazikutosha lakini CHADEMA wame-send strong message.

Sasa mapendekezo yangu... ni kwamba wanaCHADEMA kazeni boot safari bado ndefu... Mzee Mwanakijiji, Mpaka kieleweke, Mwafrika wa Kike, Kitila, John Mnyika, Zitto, Slaa etc... endeleeni badilisheni gear, wekeni gear kubwa...

Lakini hili hapa ni muhimu... tena sana... Zanzibar... chonde chonde, hiki chama ni kikubwa tunahitaji kionekane kule Zanzibar, hata kama ni kwa kuchukua wanachama wa CCM au CUF, au Jahazi asilia... chonde chonde... hatutaki yatokee ya CUF, wabunge almost wote wanatoka sehemu moja ya muungano hili sio jambo bora hata kidogo.
 
Nimeshawai kusema huko zamani sana CHADEMA inatumia system ya mwenda wazimu, nikasema CUF will never ever win general election. Leo nasema tena, CHADEMA will never run Tanzania hata kwa dakika moja kama wataendelea kutumia 1960s tacticts. Why did i said that?

Mwaka 2007 katikati nilitoa wito kwa Zitto na John Mnyika kuandaa solid strategy ndani ya chama chao na kuachana na hii system ya zimali moto. Nikasema kinachoicost CHADEMA sio bad policy zao, ila ni Mh. Mbowe na wenzie. Hawa watu wana run 1961 campain in 2008 then una expect kushinda.

Nilisema few things can be done kuongeza nguvu ndani ya upinzani, nitarudia the same thing. Kwanza kabisa upinzani unaitaji stategic plan ya long term na sio zimali moto strategy waliyotumia kwenda kiteto. Pili, upinzani unatakiwa uachane kabisa na kufocus sana na kampeni za urais, bali inabidi wa create grassroot movement kuanzia shina hadi shina, kata hadi kata, tarafa hadi tarafa, wilaya hadi wilaya then mkoa hadi mkoa. Hii movement itabainisha ni nini policy za upinzani, hii movement not only itawausisha wananchi moja kwa moja na siasa, bali itaweza kuinvolve kwenye maswala ya kijamiii, kiuchumi na kisiasa kwenye center point hizo za uchumi wa nchi

Upinzani inabidi wawe na msemaji mkuu na waache hizi habari za kila mtu kwenda kwenye media na kufungua mdomo wake kwa opinion zake. Kama upinzani watatumia grassroot movement then tutaongeza namba ya viongozi wa upinzani kwenye serikali za mitaa, tutaongeza namba ya upinzani kwenye bunge then tunaweza kuomba kubadili katiba which is the center point.

Watanzania sio wajinga, watanzania hawana idea upinzani ni nini, wanaogopa madhara yaliotokea nchi jirani yasitokee Tanzania, hivyo ni jukumu la upinzani kurestore trustee ya Watanzania. Kutumia startegy ya kwenda kwenye campain kwa helikopta i think is rediculous, sababu who cares kuhusu helicopter? People want to know ni jinsi gani watapata maji, ni jinsi gani watoto wao watapata elimu, ni jinsi gani watapata tiba pindi wanapoihitaji. So, i don't understand why upinzani don't get it.

Unajua nini maana ya mjumbe wa nyumba kumi? That is a grassroot movement, kwamba CCM wamesogeza msaidizi wao katika kila nyumba kumi. sasa kusubiri week mbili kabla ya uchaguzi ndio mnamchukua Zitto, Dr Slaa na wengine i guess ni kuwachosha wabunge hawa.
 
Nimeshawai kusema huko zamani sana CHADEMA inatumia system ya mwenda wazimu, nikasema CUF will never ever win general election. Leo nasema tena, CHADEMA will never run Tanzania hata kwa dakika moja. Why did i said that?

Mwaka 2007 katikati nilitoa wito kwa Zitto na John Mnyika kuandaa solid strategy ndani ya chama chao na kuachana na hii system ya zimali moto. Nikasema kinachoicost CHADEMA sio bad policy zao, ila ni Mh. Mbowe na wenzie. Hawa watu wana run 1961 campain in 2008 then una expect kushinda.

Nilisema few things can be done kuongeza nguvu ndani ya upinzani, nitarudia the same thing. Kwanza kabisa upinzani unaitaji stategic plan ya long term na sio zimali moto strategy waliyotumia kwenda kiteto. Pili, upinzani unatakiwa uachane kabisa na kufocus sana na kampeni za urais, bali inabidi wa create grassroot movement kuanzia shina hadi shina, kata hadi kata, tarafa hadi tarafa, wilaya hadi wilaya then mkoa hadi mkoa. Hii movement itabainisha ni nini policy za upinzani, hii movement not only itawausisha wananchi moja kwa moja na siasa, bali itaweza kuinvolve kwenye maswala ya kijamiii, kiuchumi na kisiasa kwenye center point hizo za uchumi wa nchi

Upinzani inabidi wawe na msemaji mkuu na waache hizi habari za kila mtu kwenda kwenye media na kufungua mdomo wake kwa opinion zake. Kama upinzani watatumia grassroot movement then tutaongeza namba ya viongozi wa upinzani kwenye serikali za mitaa, tutaongeza namba ya upinzani kwenye bunge then tunaweza kuomba kubadili katiba which is the center point.

Watanzania sio wajinga, watanzania hawana idea upinzani ni nini, wanaogopa madhara yaliotokea nchi jirani yasitokee Tanzania, hivyo ni jukumu la upinzani kurestore trustee ya Watanzania. Kutumia startegy ya kwenda kwenye campain kwa helikopta i think is rediculous, sababu who cares kuhusu helicopter? People want to know ni jinsi gani watapata maji, ni jinsi gani watoto wao watapata elimu, ni jinsi gani watapata tiba pindi wanapoihitaji. So, i don't understand why upinzani don't get it.

Unajua nini maana ya mjumbe wa nyumba kumi? That is a grassroot movement, kwamba CCM wamesogeza msaidizi wao katika kila nyumba kumi. sasa kusubiri week mbili kabla ya uchaguzi ndio mnamchukua Zitto, Dr Slaa na wengine i guess ni kuwachosha wabunge hawa.

ndugu yangu zitto na mnyika mko wapi? fungeni mkanda ili mtanga yaishe upesi.

nyie mlikuwapo kwenye uwanja wa mapambano njooni mtueleze sababu zilizopelekea wananchi kukukacheni.

na njooni mtupe analysis zenu tunakusubirini kwa hamu wapiganaji wenzetu.

mchango wenu unakubalika japo tunatofautiana bali tunakubaliana kuwa hii ni nyumba yetu na ss ndio wajenzi njooni watani tubadilishane mawazo
 
Kimesera kakataliwa...lipi alilofanya hadi akataliwe! haijulikani!

CCM pamoja na kashfa kibao za BoT, rada, Magari ya jeshi, Richmond, Mkapa gate lakini bado inakubalika kwa wapiga kura! Maskini Tanzania wacha tuendelee kuwa maskini wakati wageni na mafisadi wachache wakineemeka kupitia migongo yetu. Wananchi walizijua kashfa za CCM lakini bado wakaona umuhimu wa kuwachagua tena CCM! Halafu mnakuwa mstari wa mbele kulalama ugumu wa maisha unaongezeka kila kukicha!

VIPI BUBU ATAKA KUSEMA, UNAKUWA KAMA MZEE WA KIRARACHA, UNAAMINI KUWA HIZO NDIYO HOJA TOSHA ZA WANANCHI WA KITETO KUTOCHAGUA CCM? HEBU FANYA UTAFITI HUENDA WATU WA KITETO WANA VIPAUMBELE TOFAUTI NA HIVYO UNAVYOFIKIRIA WEWE.
 
Nimeshawai kusema huko zamani sana CHADEMA inatumia system ya mwenda wazimu, nikasema CUF will never ever win general election. Leo nasema tena, CHADEMA will never run Tanzania hata kwa dakika moja kama wataendelea kutumia 1960s tacticts. Why did i said that?

Mwaka 2007 katikati nilitoa wito kwa Zitto na John Mnyika kuandaa solid strategy ndani ya chama chao na kuachana na hii system ya zimali moto. Nikasema kinachoicost CHADEMA sio bad policy zao, ila ni Mh. Mbowe na wenzie. Hawa watu wana run 1961 campain in 2008 then una expect kushinda.

Nilisema few things can be done kuongeza nguvu ndani ya upinzani, nitarudia the same thing. Kwanza kabisa upinzani unaitaji stategic plan ya long term na sio zimali moto strategy waliyotumia kwenda kiteto. Pili, upinzani unatakiwa uachane kabisa na kufocus sana na kampeni za urais, bali inabidi wa create grassroot movement kuanzia shina hadi shina, kata hadi kata, tarafa hadi tarafa, wilaya hadi wilaya then mkoa hadi mkoa. Hii movement itabainisha ni nini policy za upinzani, hii movement not only itawausisha wananchi moja kwa moja na siasa, bali itaweza kuinvolve kwenye maswala ya kijamiii, kiuchumi na kisiasa kwenye center point hizo za uchumi wa nchi

Upinzani inabidi wawe na msemaji mkuu na waache hizi habari za kila mtu kwenda kwenye media na kufungua mdomo wake kwa opinion zake. Kama upinzani watatumia grassroot movement then tutaongeza namba ya viongozi wa upinzani kwenye serikali za mitaa, tutaongeza namba ya upinzani kwenye bunge then tunaweza kuomba kubadili katiba which is the center point.

Watanzania sio wajinga, watanzania hawana idea upinzani ni nini, wanaogopa madhara yaliotokea nchi jirani yasitokee Tanzania, hivyo ni jukumu la upinzani kurestore trustee ya Watanzania. Kutumia startegy ya kwenda kwenye campain kwa helikopta i think is rediculous, sababu who cares kuhusu helicopter? People want to know ni jinsi gani watapata maji, ni jinsi gani watoto wao watapata elimu, ni jinsi gani watapata tiba pindi wanapoihitaji. So, i don't understand why upinzani don't get it.

Unajua nini maana ya mjumbe wa nyumba kumi? That is a grassroot movement, kwamba CCM wamesogeza msaidizi wao katika kila nyumba kumi. sasa kusubiri week mbili kabla ya uchaguzi ndio mnamchukua Zitto, Dr Slaa na wengine i guess ni kuwachosha wabunge hawa.

I AGREE WITH YOU 100%. KATIKA MOJA YA POSTINGS ZANGU NIMESEMA KUWA KUNA TATIZO NDANI YA CHADEMA (UPINZANI) AMBAPO TABAKA LA KIBWANYENYE NDIYO LILILOSHIKA HATAMU NA NIKASEMA KUWA HATA MWENYEKITI NI TATIZO KWANI ANATOKANA NA TABAKA HILO LA KIBWANYENYE NA NDIYO WALIOMUWEKA HAPO.

NIKASHAURI KUWA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIFIKRA YAFANYIKE ILI KUILETA CHADEMA KATIKA SURA YA CHAMA CHA WANANCHI HASA. KWAHIYO KWA MIKAKATI KAMA AMBAYO UMEITAJA HAPO JUU NI WAZI KUWA CHAMA HIKI KITAKUWA KINAJISHUGHULISHA NA MAISHA YA KILA SIKU YA WANANCHI BADALA YA MAISHA YA SIKU ZA UCHAGUZI.
NI KWELI CCM IPO KWA WANANCHI 24/7. HIVI HUTUJASIKIA KUWA MTU NA MKEWE WAKIGOMBANA USIKU HUPELEKANA KWA MJUMBE WA NYUMBA KUMI HATA KAMA WAGOMVI HAO NI WANACHAMA CHADEMA? KWANINI?
 
VIPI BUBU ATAKA KUSEMA, UNAKUWA KAMA MZEE WA KIRARACHA, UNAAMINI KUWA HIZO NDIYO HOJA TOSHA ZA WANANCHI WA KITETO KUTOCHAGUA CCM? HEBU FANYA UTAFITI HUENDA WATU WA KITETO WANA VIPAUMBELE TOFAUTI NA HIVYO UNAVYOFIKIRIA WEWE.

Sina haja ya kufanya utafiti wowote. Ukweli wa jinsi CCM inavyoiangamiza nchi uko wazi na sidhani kama hizo kashfa kibao hazigusi maisha ya wananchi wa Kiteto. Vipaumbele gani tofauti walivyokuwa navyo zaidi ya kuboresha maisha yao ya kila siku!? 😕
Labda unaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kutufahamisha vipaumbele vyao tofauti na vya Watanzania wengine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom