Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Nawashangaa CHADEMA ,hivi wanafahamu maana ya upinzani ,hebu waulize mawakili kwanini mshitakiwa anatakiwa akatae kosa alilolifanya na kwa hali yoyote alikatae na alipinge.
CHADEMA kama chama cha upinzani kilitakiwa kisitoe kauli ya kuyakubali matokeo , kwani hiyo ni sumu ya kuwaua wateja wake ,kwa vyovyote vile ingelikataa kushindwa na kuweka kuwa uchaguzi ulikuwa na mizengwe na makosa kibao , automatic wafuasi wake wangelijisikia na kutembea kifua mbele kuwa uchaguzi na ushindi wa CCM una mashaka.
Lakini leo mfuasi wa Chadema na upinzani kwa ujumla hana mdomo mbele ya CCM maana wakubwa wamishasema na kukubali kushindwa ,wandugu hapa hakuna mashindano ya mpira au ngumi hapa ni mashindano ya SIASA ,hivyo unachotakiwa ni kupinga tu hata kama una uhakika ni kweli CCM imeshinda hutakiwi kabisa kusifu na hivyo hivyo ,Upinzani hautakiwi kuisifu Serikali wala kiongozi wake kwa kitu chochote ,maana unatakiwa utafute kosa lolote na hapo udidimize ,na kama hakuna kosa basi propaganda inabidi ichomekewe. Na hiyo ndio siasa.
Nikiwauliza UPINZANI na haswa Chadema ambao naamini walipewa kipau mbele na wenzao hivi mchakato wa upigaji kura Hapo KIteto haukuwa na kasoro hata moja kuanzia mwanzo hadi utangazwaji wake , na kubwa zaidi wakuu wake kucharangwa Mapanga na sime pamoja na bisibisi..........Vipi mnasema au mnakubali kuwa mmeshindwa kwa tamko la mwanzo tu mnabwaga manyanga na kukubali kuwa CCM ndio washindi halali wa Kiteto.
Siwezi kusema mengi lakini naona nimefahamika ,iwe mwiko kusifu Chama Tawala kwa lolote lile ,kila wanachokifanya basi kitafutiwe kosa ,kitungiwe kosa na kutembezwa kwa wananchi ,msikubali kabisa kuingia katika mitego ya kusifu utawala ,mtapoteza nguvu ya upinzani ,ndugu zanguni ulaya chama cha upinzani kuisifu serikali ni mwiko ,maana alieko serikalini akionekana kusalimiana na demu tu basi inakuwa ishu katika mambo ya kisiasa ,vipi hapa ambapo watu wamepigwa na kuchomwa sime mnarudi na kusema uchaguzi mmeshindwa ,inaonekana bado viongozi wa Upinzani wanajipendekeza kwa CCM ,wacheni mara moja au wapisheni watu wenye usongo na nchi yao ,Vipi mnaisifu Serikali iliyojaa ubadhirifu ,hawa hawafai kusifiwa hata chembe ni kupondwa tu kwa kila wanachokifanya.